sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Hasa kwa wale vinganganizi kutwa nzima kufatilia kama mwanaume ana mtoto nje, ukiupata ukweli ujipange kisaikolojia!! ni heri ukae kimya umwache mme wako kama alivyo wewe kaa kimya tu maisha yaendelee
(1) Mwanzo alikua anawasiliana na huyo Mama wa mtoto kimya kimya,hakutaka ujue, alikua anaogopa kukuudhi, lakini ukishajua basi atampigia na ukimuuliza atakuambia “Nilikua namjulia hali ya mtoto!” Ukikasirika atakununia kuwa humpendi mwanae.
(2) Alikua anahudumia kimya kimya, hata kama pesa kapeleka huko atakopa ili usijue. Ila baada ya kujua, takuambia, msahara nimemlipia mwanangu ada, sina pesa nyingine. Ukilalamika utasikia, “Mwanamke una roho mbaya inamaana hutaki nimsomeshe mwanangu!”
(3) Alikua hajawaambia ndugu zake, au aliwaambia lakini walikua wanamuona mtoto kisiri. Ila ukishajua, atakuambia kabisa natamani nimpeleke mtoto kwa Mama amjue, ukilalamika utasikia “Inamaana hutaki ajuane na ndugu zangu, acha roho mbaya…” hata ndugu watakuchukia kwakua ni damu yao.
(4) Asingeweza kumleta kwako kwakua hamjui, hata kama hapendi mazingira ya huko kwa Mama yake, lakini ukishajua atakuambia nataka kumleta, ukikataa atakuambia “Hapa ni kwangu huwezi kunipangia, una roho mbaya kama nikiwa hao hutaki aje kujuana na ndugu zake nikifa itakuaje!”
(5) Alikua hampost siku yake ya kuzaliwa, akienda kumsalimia anaendakimya kimya. Lakini ukishajua ataenda kumslaimia, siku ya kuzaliwa atampost na huyo Mama mtoto naye atapost kukuumiza roho ukilalamika utasikia “Kwani wewe unakosa nini hapa ndani, mbona unaroho mbaya!”
AKILI KICHWANI, USITUMIE MOYO KUFIKIRI!