EWURA: Nchi ina hifadhi ya Mafuta inayojitosheleza, Petrol inatosha kwa siku 19 na Diesel siku 18

Ni hatua nzr, ningeomba mzungeke Hadi sheli za ndani zaid kama huko geita, kilombero, katavi Kuna ujinga mwingi sna muwajibishe hata kufutia leseni maana wanakwamisha nchi
 
Your browser is not able to display this video.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (EWURA) Dkt. James Andilile amesema hayo na kufafanua kuwa Petrol iliyopo inatosheleza matumizi ya siku 19 na Dizeli ipo ya kutumika kwa siku 18.

Aidha, EWURA imevifungia kwa miezi 6 Vituo 2 vya Mafuta ambavyo ni Camel Oil na Mtemba vilivyopo Msamvu na Turiani Morogoro huku Kituo GBP cha Ipuli Tabora kikifungiwa kwa muda usiojulikana baada ya kutuhumiwa kuficha Mafuta.

Takwimu za Mahitaji ya Mafuta Nchini zinaonesha Tanzania inatumia Lita Milioni 4.5 za Petroli kwa siku na Dizeli Lita Milioni 6.6 kwa siku.
 
View attachment 2739153

Kazi ipo huku Tz.
Kazi tunayo.
 
Ni aibu na fedheha msomi wa PhD mwenye nyadhifa aliyotunukiwa kuongoza taasisi kubwa ya namna hiyo alafu anakuja kuzungumzia swala la siku dhidi ya uhifadhi wa mafuta mbele ya hadhira na dunia kwa ujumla ikiwa inakutazama, kukusoma na kukusikiliza.... teh! teh! Eti siku
Dahh! Sisi bado sana! Alafu kuna mjinga anasema jeshi letu ni la sita (6) duniani... vitu nyeti kama hivyo ambavyo nchi inatakiwa iwe navyo sisi vimetushinda.

Amini Nawaambieni... kama mna watoto wenu bora muwapeleke Majuu tu huku ni kwa hovyo sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…