EWURA yatangaza Bei mpya za Mafuta kwa Mwezi November 2026. Petroli imepanda Tsh 28 wakati Diesel zaidi ya Tsh 42

EWURA yatangaza Bei mpya za Mafuta kwa Mwezi November 2026. Petroli imepanda Tsh 28 wakati Diesel zaidi ya Tsh 42

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza Bei mpya za Mafuta, Petrol, Diesel na Mafuta ya Taa, zitakazotumika kwa mwezi Novemba 2026.

Bei mpya zinaonesha kuendelea kusuasua kwa Bei za Mafuta, maana kwaka Jana (2025) mwezi kama huu, Dar es Salaam Lita moja ilitangazwa Tsh 2,700 ya Petroli ila kwa sasa ni Tsh 4,100.

Kwa Dar es Salaam, Lita Moja ya Petroli itakuwa Tsh 4,083 wakati Diesel itakuwa Tsh 4,128 tu.

Kigoma na Katavi, mjiandae na Tsh 4,300 kwa Lita.

Asanteni.

Taarifa kwa Umma kuhusu Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta, Tanzania Bara, zitakazoanza kutumika kua.jpg
Taarifa kwa Umma kuhusu Bei Kikomo za Bidhaa za Mafuta, Tanzania Bara, zitakazoanza kutumika k...jpg

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo, Jumatano, Novemba 4, 2026, huku bei za petroli, dizeli na mafuta ya taa zikipanda ikilinganishwa na mwezi Oktoba.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei kikomo za rejareja kwa Dar es salaam ni shilingi 4,083 kwa lita ya petroli, shilingi 4,128 kwa dizeli na Shilingi 4,117 kwa mafuta ya taa. Kwa Tanga, lita ya petroli itauzwa kwa bei kikomo ya shilingi 4,149, dizeli shilingi 4,194 na mafuta ya taa shilingi 4,183.

EWURA imeeleza kuwa licha ya bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kushuka kidogo mwezi Oktoba ikilinganishwa na Septemba, kuendelea kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati kumeongeza gharama za usafirishaji na bima, hivyo kuongeza gharama za uagizaji wa mafuta nchini.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa soko la dunia na kuchukua hatua kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa mafuta pamoja na kuwapunguzia Wananchi makali ya bei.
 
Back
Top Bottom