EWURA yatangaza kupanda kwa bei ya mafuta leo Septemba 6, 2023

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano September 06, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi September 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3213 kwa lita, dizeli Tsh. 3259 na mafuta ya taa 2943.

EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi September 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi 21%, gharama za uagizaji wa mafuta hadi 62% ikilinganishwa na mwezi August 2023 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+).

Itakumbukwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi uliopita zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano August 02, 2023 saa 6:01, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ilikuwa ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 na mafuta ya taa 2668.

Ipande tu maana mikutano ya CHADEMA imezidi
 
Huu ni udhaifu wa kuanzia kwa januar, aliponusa akaona pua inabana akaomba poo.

Hii nchi inakuja kushindikana muda siyo mrefu.

Mchele bado ni 2500 sembe na ngano vilishuka kufika 1600 sasa vinapaa kule.kule.

Ngoja niishie hapa.
 
Biteko kaangushiwa jumba bovu
Ameingia hiyo wizara lini? Mume wa spika ndio Boss wa Ewura.

Wenye vituo vya mafuta wanajuwa mapema tu bei inapanda uliza watu wa Tabora na Kigoma wana muda gani hawana mafuta yamefichwa kusubili bei mpya.

Swali wafanyabiashara wanajuwaje bei itapanda na siyo kushuka?
 
Huu ni udhaifu wa kuanzia kwa januar, aliponusa akaona pua inabana akaomba poo.

Hii nchi inakuja kushindikana muda siyo mrefu.

Mchele bado ni 2500 sembe na ngano vilishuka kufika 1600 sasa vinapaa kule.kule.

Ngoja niishie hapa.
We mama tafadhali last night tu nimenunuwa mchele stock ya home kwa bei ya sh 3000 kwa kilo na hii ni bei ya muda mrefu tu, labda mchele wa vitumbuwa ndio bei hiyo.
 
This mus stop..

Hakuna haja ya kutesa wananchi bila sababu....
Udalali sio kitu kizuri kwa taifa lolote changa kama la kwetu.
Hiyo sio biashara ni uhuni....

Na kama EWURA wameshindwa waache twende kiholela kuliko kuwa na a buch of people paid by tax payers money doing nothing and or protecting the interests of cartels......

Mnaharibu image ya nchi kwa vitu visivyo na maana..

Kwahiyo hata umeme kukatika mara kwa mara ni short supply ya soko la Dunia?
Exactly [emoji817]...
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano September 06, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi September 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3213 kwa lita, dizeli Tsh. 3259 na mafuta ya taa 2943.

EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi September 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi 21%, gharama za uagizaji wa mafuta hadi 62% ikilinganishwa na mwezi August 2023 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+).

Itakumbukwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi uliopita zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano August 02, 2023 saa 6:01, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ilikuwa ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 na mafuta ya taa 2668.

Huyu ndiye Mme wa Spika Tulia Ackson anasema tusiwe na hofu mafuta yapo ambaye ndiye mkurugenzi wa Ewura.

Wewe unadhani Tulia ataruhusu hoja ya mafuta iende Bungeni na Mume wake Spika ajadiliwe ?
FB_IMG_1693963258290.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom