EX ananiomba pesa. Ushauri wenu please

Sasa mbona kama amegonga mwamba
 
Huyo anaakili timamu ndio maana uliweza kuwa na uhusiano naye,hivyo ushauri mhudumie kama alivyokuhudumia wakati ule,kiroho safi tuu,maisha ndio haya haya.Ukiona anayetoa uhai wa mwenzake au yake hajui utamu wa maisha.
 
Alpha Male hasemi "mimi ni Alpha Male".

Ukishasema "Mimi ni Alpha Male" tayari wewe si Alpha Male.
 
Huyo anaakili timamu ndio maana uliweza kuwa na uhusiano naye,hivyo ushauri mhudumie kama alivyokuhudumia wakati ule,kiroho safi tuu,maisha ndio haya haya.Ukiona anayetoa uhai wa mwenzake au yake hajui utamu wa maisha.
Unapoint kwenye maneno yako
 
Tanzania dhambi zinakuwa kitu cha kawaida.

Dhambi zako unaomba ushauri kwa jamii?.
 
Mimi ninaye mmoja ananikubali sana lakini mimi ndo nilizingua mpaka leo huwa anatamani turudi kama zamani na akiwa na shida huwa namsaidia lakini sio mara zote kwa sababu nimetoka naye mbali sana.

Ipo hivi huyu dada nilianza nae mahusiano toka o-level mpka nikamaliza chuo(2013-2019) na kipindi hicho chote tumekuwa wapenzi na marafiki pia, ni moja ya wanawake niliowakuta sealed kabsa na nikaanzisha naye safari ya mapenzi kwa miaka zaidi ya 6...

Kilichonifanya niachane naye ni kuwa mbali kwa muda mrefu, mimi nilipata kazi mkoa Y nilipotoka chuo wakati huo yeye akiwa Dar mwaka wa kwanza chuo X... Basi penzi likapoa hatimaye likafa mimi nikapata pisi nyingine maisha yakaendelea.

Si unajua fimbo ya mbali haiui nyoka, ndo tukapotezeana lakini bado kila mtu alikuwa na feelings kwa mwenzake, huwezi amini yule manzi alikuwa anaomba pesa kwa bwana ake anakata ticket ya ndege kuja mkoani ili anisalimie tu kwa kigezo eti amenimiss na mimi ndo nilimfundisha mapenzi na hawezi kunisahau kamwe😂.

Kufupisha story kama ni watu mliochana kwa mazuri wewe mtumie tu hela wala hakuna shida yoyote.
 
Ukishajisema "mimi ni Alpha Male" hayo ni matangazo ya biashara tu.

Kwa kanuni Alpha Male hatakiwi kujisema hivyo.
Kanuni ya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…