TANZIA Ex. SACP. Jacob Massawe Mwaruanda afariki Dunia

IGP Simon Nyakoro Sirro ametangaza msiba wa Ex. SACP. Jacob Mwaruanda uliotokea jana Februari 15, 2022 katika Hositali ya Benjamini Mkapa, Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Sirro ameeleza taratibu za mazishi za marehemu ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa zinaendelea kwa kushirikiana na familia.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Kisasa na kuhusu ratiba ya mazishi taarifa rasmi itatolewa baadaye.

View attachment 2120757
Kwani alishastaafu Mzee Mwaruanda?
 
Haukumwelewa alichosema. Nafafanua - sote tutakufa, tutendeane wema. Polisi wasinyanyase wengine kana kwamba wao hawatakufa... Kama hilo nalo halieleweki, basi unahitaji msaada kuvuka barabara.
wewe nani wakuishi milele?
 
Hata kama sote tutakufa ila kuna madingi wengine huwa tunawaombea wafe haraka kutokana na dhuluma na unyanyasaji walio fanyia wengine, na hata kwnye bible kitabu cha Daniel kuna hii kitu 'mene mene tekel upharsin' ambayo kimsingi ni full retaliation …..
 
wewe nani wakuishi milele?
Kwani nimekwambia kwamba nitaishi milele? Ukatili wanaofanya kwa watu wasio na hatia wanadhani kuwa hawatakufa. omba yasikukute usiingie mikononi mwa hao watu tuna maumivu makali wametutia hasara sana vuta picha unaingia lock up pale counter unasachiwa unaacha mil 2 unakuja kutoka lockup unataka mil 2 wanakuruka wanasema haukuacha pesa yotote😔😔
 
Kila mtu atakufa. Sioni sababu ya kubeza kifo cha mtu mwingine wakati ni suala la kila mmoja kwa wakati wake. Yeye ametangulia wa kujiuliza ni wewe uliebaki duniani ukifikiri wewe ni Malaika.
 
Kwani nimekwambia kwamba nitaishi milele? Ukatili wanaofanya kwa watu wasio na hatia wanadhani kuwa hawatakufa. omba yasikukute usiingie mikononi mwa hao watu tuna maumivu makali wametutia hasara sana vuta picha unaingia lock up pale counter unasachiwa unaacha mil 2 unakuja kutoka lockup unataka mil 2 wanakuruka wanasema haukuacha pesa yotote😔😔
amekufa hiyo mil 2 imerejea?
 
Haukumwelewa alichosema. Nafafanua - sote tutakufa, tutendeane wema. Polisi wasinyanyase wengine kana kwamba wao hawatakufa... Kama hilo nalo halieleweki, basi unahitaji msaada kuvuka barabara.
ukiona umetendewa hivo ujue na wew kuna pahala ulimkosea mwingine hivo KARMA akawajibika mda huo.

ukumbuke malipo ni hapahapa kaburini ni pumziko tu. hivo kwa kauli yake haimaanishi kakomeshwa ila kapumzika na wewe uliye hai msoto haujaisha nani ana nafuu?
 
Haya mkuu. Endeleeni tu kutuua. Mungu atatulipia...
ukiona umetendewa hivo ujue na wew kuna pahala ulimkosea mwingine hivo KARMA akawajibika mda huo.

ukumbuke malipo ni hapahapa kaburini ni pumziko tu. hivo kwa kauli yake haimaanishi kakomeshwa ila kapumzika na wewe uliye hai msoto haujaisha nani ana nafuu?
 
"Msiba upo kwake Kisasa, karibu na Pub ya Alberto"

Taasisi hii inapaswa kusomesha watumishi wake. Jeshi la polisi ambalo halijui hata majina rasmi ya maeneo ya nchi hii haliwezi kudhibiti jinai kwa sababu halitajua misitu waliojificha majambazi.

Kisasa karibu na Pub ya Alberto iko Malawi ???????
 
Back
Top Bottom