EX wako unamuombea maombi gani na kwanini?

Nilikua nae tangu nikiwa na 17years tukipeana ahadi ya kuoana [emoji24][emoji24][emoji24] nilikaa nae mpaka nilipomaliza chuo nikarudi nyumbani ambako ni mkoani kwani chuo nilisomea dar
Nilikaa nyumbani Kwa muda wa miezi sita ila sikuona dalili yoyote ya ndoa nikaanza kutafuta kazi nikapata kazi dar japo ilikua ya mshahara mdogo nikahamia dar nikaanza kufanya kazi.
Siku moja akanipigia simu niache kazi dar nirudi mkoani tuanze mambo ya harusi na kama ni kazi amenitaafutia,basi nikaaga kazini nikaja mkoani nikaanza kukaa home huku naenda kazini.
Nilifanya kazi mwaka mzma hajawahi kukanyaga nyumbani nikamwambia nimeamua kuacha kazi nikae nyumbani Mpaka siku atakapokuja home ajitambulishe ndo ilikua ticket ya kuniacha...Niliachwa mchana kweupe nikaja kugundua alishazaa na mtu mwingine.
Mwaka jana kamchukua mwanamke anaishi nae na anamtoto sasa[emoji24]
Nikifikiria muda niliopoteza sina hamu
 
Una ex mmoja babe Chakorii ?
Huyu ninaemzungumzia hapa aiseh amenifundisha vingi mno,alinipeleka ulimwengu mwingine,alinionesha namna mwanaume anavyopaswa kumjali mwanamke.itoshe kusema alikuwa ni kiumbe wa pekee.

Kwanini namhesabu huyu..ni kwa sababu kulikuwa kuna mapenzi na kwa mazingira tuliyokutana nayo kwa kipindi kile kama sio upendo basi amgenitumia na kunipiga chini lakini badala yake mwamba aliniyanyua,akasimama kidete na mimi kuona nanyanyuka.Joanah itoshe kusema Mungu wa mbinguni atume jeshi lake likamlinde kwenye kila ncha ya dunia.

Hawa na sasa hivi ninawahesabu kama fuckmates.we https://jamii.app/JFUserGuide,off we go.

Wasasa wanakuwa pengine wanavutiwa na muonekano tu,au unafanya kazi sehemu fulan,au una tako,mguu,rangi nzur,sauti nzuri na mengineyo.so hakuna mapenzi bali kuna ngono tu.so wengi nimeahawajaribu kwa namna ninayoijua mimi nimeona wanapenda mtu kitu.hakuna mapenzi ya dhati.

So tunakulana utamu ukiisha tunatemana kila mtu anaenda kuota sehemu nyingine.kama tunapendana kweli basi tunaingia kwenye mikakati kufanya maisha.
Sipendi unafiki wala kuzuga huo ndo ukweli
 
Ameeeeen.
 
Duuuuu poleeeeh sana.
 
Nakubali kipendhiiii.
 
Asipate wa kumsugua mashavu kama nlivyokua namsugua mimi
 
Simlaani wala nini ila namuombea asinikumbuke kwa chochote maana alikuwa ni majanga tu kwangu. Demu anaamka asubuhi hapigi mswaki na anakunywa chai na kul chakula cha mchana bila hata kupiga mswaki, atamaliza kula atakwenda kwa majirani kutafuta umbea, hapo hajaoga wala kupiga mswaki na hana habari yeyote ya kusafisha mwili wake. Nilimgombeza mpaka nikachoka, nilipomuacha ndipo ananiambia atajirekebisha na atakuwa anaoga mara tatu kwa siku na ataanza kupiga mswaki. Toka nimfkuze na majanga yake, nyumba yangu sasa inanukia vizuri utafikiri ndiyo imetoka kupigwa deki ama kuna malaika fulani anaishi nami.
 
Ooooh!pole sana kwa kumpoteza huyo jamaa
 
Kila nikiswali namuombea DUA Sana....

Namuombea dua nyingi,yeye ,mumewe na wanawe....aaaamin!

Namuombea dua apate afya njema,fedha nyingi,mafanikio makubwa na uhai mrefu .....

WATU HUKUTANA KWA SABABU....

#KaziIendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…