Ex wangu anaona status zangu licha ya kufuta namba zake kila mahali na ku unfollow Social Media

Ex wangu anaona status zangu licha ya kufuta namba zake kila mahali na ku unfollow Social Media

Mr sule

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2021
Posts
606
Reaction score
1,110
Habari wangu.

Kuna ishu naomba msaada, sijuwi ndio mambo yamebadili siku hizi kwenye whatsApp.

Nilisitisha mahusiano na aliekuwa mpenzi wangu. Nilifuta namba yake na picha zake zote. Lakini ajabu bado nikiweka status anaona na jina inajitokeza lile alioandika kwenye whatsaap yake. Imetokea mara tatu nyakati tofauti.

Siku nyingine baada ya kuona status yangu nilitaka nimuulize lakini naona hii namba haijaseviwa. Nashindwa kumuuliza cos ndio attention anayosubiri kuona text yangu.

Niliamua ku unfollow lakini bado tu anaona, nikafuta picha zake zote, lakini bado tu anaona, nimegoogle kutaka kujua jambo hili linawekanaje, bado sijapata majibu ya kuridhisha.

Nilitaka niweke hasiwe anaona status zangu, lakini mimi nataka nisiwe na namba yake kabisa, kublock haitonisaidia cos bado namba yake itakuwepo kwa watu nilioblock.

Nimejaribu mtu mwingine, lakini mambo ni tofauti, nifuta namba yake hawezi kuona status yake.

Naomba msaada, au ndio features mpya za whatsapp au kuna kitu gani amefanya.

Nime restart simu yangu maybe kuna mahali kafanya mchezo lakini wapi.

Msaada sipendi aone status zangu.
 
Back
Top Bottom