Hakuna watu wanaishi kwa matumaini makubwa kama wafuasi wa Raila. Kila IEBC wanapotoa matokeo utawasikia "bado ni mapema sana, subiri kidogo, kuna ngome zetu bado, huoni asilimia zinapanda, na maneno mengine meeengi kama wagonjwa wa ndui"
Yani nikiwasililiza nacheka tu. Kwanza hawaamini kama wamechezea "vitasa vya uso" hadi muda huu. Walitegemea matokeo ya awali waongoze but imekuwa kinyumeche. So wamepagawa. Pili wanaamini eti kuna ngome zitawapa ushindi, wanasahau kuwa Kenyatta nae ana ngome zake pia.
Tatu kuhusu percentage wanasema Raila anapanda. Hii ni kwa wasiojua hesabu tu ndo watashangaa. Lakini kwa anayejua hesabu sio jambo la kushangaza. Hata Anna Mghwira siku ya kwanza alipata asilimia zero then akaanza kupanda polepole hadi zero nukta kadhaa. Na logic ni kuwa kura zinapokua chache aliyeongoza anakuwa na percentage kubwa lakini percentage inapungua kadri kura zinavyozidi kuongezeka.
Kwa mfano kura zikiwa 10 mimi nikapata kura 9 na ww moja, it means nimepata 90% na wewe 10%. Lakini kura zikawa 1000 nikapata 700 na wewe 300 means nitakua na 70% na wewe 30%. So sio jambo la ajabu. Probability ya percentage kuongezeka au kupungua kwa kadri kura zinavyozidi kuhesabiwa ni jambo la kawaida. Hii ni topic ya "probability" form 2 A. Vijana wa Raila hamkusoma hii?
We hujiulizi inakuaje Raila percentage zinaongezeka ila anazidi kuachwa kwa gap kali la kura. Matokeo ya awali Uhuru alikua na laki 3 na Raila laki 2 plus, means tofauti ya kura laki moja plus. Baadae Uhuru 500K+ na Raila 300K+ means tofauti ya kura 200K+. Badae Uhuru 900K+ na Raila 600K+ means tofauti ya kura 300K+. Badae Uhuru 1.7M+ na Raila 1.3M+ means tofauti ya kura 400K+. Sasa hivi Uhuru 3.3M+ na Raila 2.6M+ means tofauti ya kura 700K+.
Hii ina maana kwamba kila matokeo yanapotangazwa Raila anazidi kuachwa nyuma kwa kura nyingi sana. Mwanzoni kabisa alikua na gap ya kura laki moja. Lakini sasa hivi ana gap ya kura laki 7. Halafu wafuasi wake wanabana pua kama Hamorapa eti "Raila anapanda". Anapanda kwenda wapi? Labda darini.
Jiandaeni kisaikolojia kupambana na hali zenu wazee. [HASHTAG]#UhuruTanoTena[/HASHTAG].!