EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017

EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017

Dadeki, saa kumi na mbili na dakika thelathini na tatu ndo nimepiga kura yangu! Son of the soil, nimeshatimiza wajibu wangu kwa nchi yangu, shukran zote ni kwa Maulana!

Hongera tume ya uchaguzi na mipaka IEBC mmejipanga vyema sana! Diwani wangu Ustadh Kanchory mwenyewe, tumepatana nikitoka akanisalimia na kupiga bonge la smile, aisee ni kama ameshinda Sportpesa vile! Anajua nishampa zake tano tena!

Jubilee hoyee!

Kiswahili kimenyooka hivi
 
Wewe ni Mkenya kweli??? Nani amekuandikia hiki kiswahili??
Si tumewakaribisha wenyewe uswahilini kwa nini wasijue Kiswahili. Nina Rafiki Mganda alikaa Tanzania pale Kinondoni. Huyu Bwana ukikutana naye mswahili kabisa hata vile viingereza vyao hana ni Kiswahili asubuhi hadi jioni. Acha wakiongee hiyo ni sawa tu mradi wakiongee vizuri tu bila kukichafua.
 
Kura nishaipiga. Kuna wale ambao huenda kwenye kituo cha kupigia kura bila kujua yule watakayemchagua. Hawa ndio huwachelewesha wengine.
 
Nawapongeza azam kwa kutuletea live habari za uchaguzi kenya.

Lakini nmesikitishwa na kitendo cha mtangazaj wao mmoja ivony kama sijakosea jina kuvaa socks za miguuni mkononi. Halafu akaamua kutoboa sehemu ya kutolea vidole gumba...

Ina maana hawajamuona kuwa amefanya kitu cha kipuuzi?kwa nini avae socks ? Kama ni baridi ingawa nmeshangaa watu wengi wamevaa kawaida. Basi kwa nini hakununua socks maalum kuliko kuvaa kituko kama hicho? Azam ina maana mmeshindwa kumwambia upuuzi huo?lazima ajue hiyo siyo comedy
Pambana na hali yako mkuu!
 
Pole nilijibu pasipo penyewe. Hii ilimhusu bwana254 hapo juu. Yeye aliitumia kabisa Jina la Yesu kumtakia kushindwa Mgombea wa NASA. Kwako ilijibiwa kimakosa. Pole ndugu! Asante kwa uvumilivu.
Pamoja sana mkuu.

Peace and love!!
 
[QUOTE="BUBE, post: 22724000, member: 31216"

umharibu kura[/QUOTE]
 
Lazima bibi apige kura!
20638366_10207307326600663_6907974460439008617_n.jpg.jpeg
 
Watanzania tunapenda kufuatialia mapungufu ya kijinga tunaacha maswala ya msingi.

Ivona ni mtangazaji wa kimataifa.
Ivona hafahamu siasa za Kenya hivyo kuripoti kwake lazima kuwa na mapungufu.
 
Mimi ni mkenya jombaa! Sasa hivi nina alama kwenye kidole, kuashiria nimetimiza haki yangu kama mkenya. Kiswahili ndo lugha tunayoienzi mkuu! MK254, uko wapi,kura ulishapiga au vipi?
Nimempigia Babaaaa sasa nasubiri kushangilia niko umbali mita 7000
 
Pia hyu seneta wetu toka chama cha miau miau lazma apite..jembe la ukweli
 
Nimempigia Babaaaa sasa nasubiri kushangilia niko umbali mita 7000
Umeeka tick kwa Raila na X kwa Uhuru? Hii ni muhimu sana kwa wafuasi wote wa NASA, usipofanya hivo hutaweza kulinda kura yako! Itaibiwa aisee!
 
Back
Top Bottom