Habari za asubuhi bandugu.Ni siku nyingine tena ambayo Mimi nimegoma kabisa kujishirikisha na ujenzi wa taifa,nataka nijenge nyumba yangu.
Msaada unahitajika mwenye kuwa na utaalamu wa kuchora ramani na BOQ Yake ya residence house please PM ipo wazi.
N.B:uwanja una 30 M *20 M
Nawasilisha
nikupongeze kwa maamuzi ulioamua kuchukua.
nikushauri machache
1. njia bora zaidi ya kupata architect ni kupitia recomendation kutoka kwa mtu unaethamini ushauri wake.
2. ukiwa na muda kutana na hata architects wawili au watatu ili uweze kupata mtazamo wao, uzoefu wao, uone kazi zao kama ikiwezekana ata ukatembelea moja ya kazi yake site ukaona namna alivyo involved na anavyo elewa kazi yake.
3. kuna levels tofauti za elimu, ujuzi na uzoefu nikuwekee makundi baadhi wa chini kabisa ni wanafunzi walio miaka ya kumaliza shule au waliomaliza recently hapa tegemea unafuu na exposure ndogo, kuna walio practice kwa miaka michache chini ya mitatu hapa tegemea uzoefu mzuri na uelewa wa ujenzi kwa vitendo na idadi flani ya miradi, kuna wenye uzoefu na waliosajiliwa hapa baadhi wana makampuni au wako attached na makampuni hapa wanaweza kua na gharama kdg na uzoefu wa kutosha wanafahamu sheria na wanaweza weka tija kubwa kwenye kazi yako, na kuna high end professionals, hawa wanamiliki makampuni labda wana experience ya miaka 10+ hawa kwa kazi ndogo hawatakufaa. nakushauri u opt kati ya wenye uzoefu wa mtaani atleast 2+ years au waliosajiliwa.
4. jitaidi kufahamu unachotaka, mahitaji yako ya nyumba ya namna ipi, unabudget gani, unajenga kwa phases kwa income lumpsum na timing gani, una mpango wa kuhamia au utajenga polepole, una kiwanja kina status gani? nk ili ukiwa na maongezi nae basi uwe clear na what you really need
5. akueleweshe clearly kazi inafanyika kwa gharama gani, malipo ni kwa ustaarabu upi, je ana deliver nini na wakati gani yani anamajukumu gani, unaweza pia uliza maswali ya kichokozi kama, cost ni laki 4 kwa nini sio laki 5 au 7 uone uelewa wake wa mambo ukoje.. nk. pia akueleze hatua za ujenzi zikoje na yeye atawajibika wapi? (maandalizi ya michoro, vibali, material sourcing, sourcing ya mafundi, planning ya ujenzi, usimamizi, ukaguzi nk).
Note: kazi kubwa ya architect sio kukuchorea ramani tu, sbb kama ni ramani ziko nyingi tu internet unaweza download.. au kununua. kazi yake ni kukushauri mchakato mzima wa ujenzi ikiwemo ramani kama sehemu ndogo tu. kutumia mil 50 kwenye ujenzi ni jambo la kawaida na inaweza isitoshe kwa 3-4 bedroom house, ukiweza kupata mtu sahihi wa kukushauri katika huo mchakato basi naamini utakua katika mazingira mazuri ya project yako.
in the spirit ya kujenga taifa, naweza kujitolea kukusaidia kukushauri kama third party ukapata mtu unaemhitaji.