Pre GE2025 Ezekiel Kamwaga: Tundu Lissu anaweza kuwa Dikteta mtarajiwa

Pre GE2025 Ezekiel Kamwaga: Tundu Lissu anaweza kuwa Dikteta mtarajiwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwandishi wa habari Ezekiel Kamwaga, akizungumza na Jambo TV, ameeleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa kisiasa wa Tundu Lissu, akimtaja kuwa na tabia zinazoweza kumfanya “dikteta mtarajiwa” iwapo atapewa nafasi ya kuongoza.

Kamwaga amedai kuwa Lissu hutumia lugha ya kudhalilisha wapinzani wake, akiwaita majina kama “msaliti” au “mbogamboga,” akilinganisha hili na tabia za madikteta kama Adolf Hitler. Pia, amesema Lissu hana woga wa kutoa madai mazito bila ushahidi wa kutosha, akirejelea tuhuma za hivi karibuni kuhusu watu wanaodaiwa kumpatia fedha.

Ameonya kuwa, licha ya siasa zake kukubalika kwa sasa, Lissu anahitaji muundo wa uongozi thabiti kutoka kwa Freeman Mbowe ili kuongoza kwa mafanikio ndani ya CHADEMA. Kamwaga amependekeza chama hicho kumpa nafasi Lissu bila kuharibu taswira ya Mbowe.

Amesisitiza kuwa siasa za Tanzania zinahitaji aina ya uongozi wa Lissu, lakini akataka tahadhari zichukuliwe ili kuepuka changamoto za baadaye.
 
Back
Top Bottom