Kwa mtazamo huu, inaelekea Lissu akipata kura za ushindi toka kwa Watanzania, basi itahesabika ni kukamilika kwa “malengo ya wenye nia zilizojificha”! Bila shaka wasiwasi Huu unatokana na uwezekano mkubwa wa Lissu kupata kura nyingi sana. Isingekuwa hivyo, naamini Lissu angepuuzwa kama kina Lipumba, Rungwe, Membe, nk.
Miaka yangu yote nimekuwa nikisikia kauli za aina hii katika nchi za kikomunisti. Nafikiri mtazamo wa serikali ya awamu hii ni kurejea kwenye enzi hizo na kuwa na “vanguard party” kabisa yenye kikundi cha makada wanaoamua nani wawe viongozi wa taifa. Kwa nini tusifanye hivyo rasmi ili kuwazibia kabisa mabeberu na vibaraka wao?