Fahamu jinsi ya kuwasiliana na Viziwi kwa njia ya Alama

Fahamu jinsi ya kuwasiliana na Viziwi kwa njia ya Alama

Fingers spell au tahajia ya vidole ,hutumika kuelezea majina ya mtu au sehemu .au misamiati isiyo na alama. Kuhusu sentensi lugha ya alama ni tofauti na kiswahili . Kwenye LAT unafikishwa ujumbe muhimu tu . Na sio sentensi nzima
Upo sahihi
 
Fingers spell au tahajia ya vidole ,hutumika kuelezea majina ya mtu au sehemu .au misamiati isiyo na alama. Kuhusu sentensi lugha ya alama ni tofauti na kiswahili . Kwenye LAT unafikishwa ujumbe muhimu tu . Na sio sentensi nzima
Kumbe nawe nawe ni mdau wa elim maalum??
 
Ngoja nitawapa link ya kamusi ya lugha ya alama ambayo ndio pendekezwa.
 
Pia nikipata fursa nitawatumia na Vitabu vya kuanzia kujifunza lugha ya alama ni rahisi ka una nia ila ni ngumu kama huna nia.
 
Vitabu itabid mvumilie kdg maana mb ni shida kdg. Nikiwa vzr nitawatumia . Tuwe tuna kumbushana
 
Pia kuna group la chuo kikuu huria tawi la Tabora wanafundisha lugha ya alama kuanzia mwanzo kabisaaaa hasa kwa wanaoanza linawafaa kabisaaa maana awamu ya kwanza walianza na alphabets,numbers na kuunganisha herufi na kuunda sentensi..
Kwa awamu ya kwanza walimaliza ila mwisho wa mwezi huu tena wataanza kufundisha. Wakikaribia kuanza nitawajuza ili mkajiunge mfaidike. Pia muwe mnanikumbusha wakuu.
Asanteni
 
Naomba niwatumie kwanza hii yenye mb ndg SIKU ZA WIKI.
 

Attachments

  • VID-20241006-WA0000.mp4
    9 MB
Mkuu PM yangu inashida nashindwa kusoma jumbe zilizotumwa wala mm kutuma . I remember tulipanga kuwasiliana jana
Yah ni kweli mkuu. Maana nimeku PM but msg haijasomwa.
Naomba unipe njia ya kuwasiliana nawe.
 
Habari za saizi wakuu,

Twende moja kwa moja kwenye mada yetu ya Leo.

Lugha ya alama nini?

Lugha ya alama Tanzania ni chombo cha mawasiliano ambacho humuwezesha mzungumzaji kufikisha ujumbe kwa jamii kwa hadhira iliyokusudiwa na jamii husika.

Lugha ya alama imegawanyika katika makundi mawili;

1. Alama kwa njia ya herufi (alphabet)
2. Alama kwa njia ya ishara.

Katika mada hii ntaongelea zaidi kipengele cha kwanza ambacho ni ALAMA KWA NJIA YA HERUFI..

Kwanini?

Kwa sababu kipengele hiki ni rahisi kumfundisha mtu aliye mbali na akaelewa mfano hapa JAMII FORUMS.

Kipengele cha pili hufundishwa MUBASHARA .

Tulisongeshe,

ALAMA KWA NJIA YA HERUFI (ALPHABET)

Herufi A, B, C,D,E,F,G, H,I,J, K, L, M,N,O mpaka Z huweza kuandikika kwa kutumia vidole vyetu.

Mbinu gani hutumika?

Mbinu zitumikazo hapa ni kukunja vidole kwa kufuata umbo la herufi husika.

Mfano herufi "C" ukitizama katika picha hapo chini utaona KIDOLE GUMBA na vidole vingine vimekunjwa kuunda shape ya herufi C. Utaratibu huu pia hutumika katika kuandika herufi zinazo fuata.

NB: Herufi "I" na "J" katika picha utaona kama zinafanana, utaratibu wa kuzitofautisha upo hivi, UKITAKA KUANDIKA HERUFI J ANZA KWA KUANDIKA HERUFI ,"I" THEN KUWA KAMA UNACHORA HERUFI J HEWANI.

72453ddd3ee3cd7b225040237ac64135.jpg

55ac6f54a4f4accaf3df94ff08e5cb9d.jpg


Wakuu TUMIENI umakini kuchunguza MIKUNJO YA VIDOLE pamoja na alama husika mtagundua mikunjo ya vidole na imekunjwa kwa kufuata UMBO LA HERUFI HUSIKA. Mfano mzuri tizameni herufi Y.

HERUFI HIZI HUTUMIKA JE?

Herufi hizi hutumika kwa kuandika neno au maneno uliyokusudia kwa mhusika (kiziwi) kwa kufuata herufi tajwa hapo juu katika picha.

Jaribu sasa kwa kuanza na maneno kama DADA, KAKA, MAMA, BIBI n.k,
Ni rahisi sana na utaweza kuwasiliana au kuongea na kiziwi yeyote.

Karibuni kwa nyongeza , maoni, hoja na maswali.

Ahsanteni.
Dole la kati kumbe haipo
 
Namba
 

Attachments

  • ni_sehemu_ya_kuweza_kujua_lugha_ya_alama_karibu_Jifunze_namba_kwa_lugha_ya_alama(360p).mp4
    3.3 MB
Back
Top Bottom