Fahamu jinsi ya kuwasiliana na Viziwi kwa njia ya Alama

Fahamu jinsi ya kuwasiliana na Viziwi kwa njia ya Alama

Hongera MKUU umejitahidi xana. Poa ni muhim sana kwa watu wote wenye uwezo wa kusikia sauti kujifunza lugha hii ili kuwasaidia hawa wenzetu viziwi. Namshkur mungu nimejifunza lugha hii Na kwa sasa naweza kuwasiliana nao vizur n pia nawafundisha masomo yote. Ni lugha nzuri sana ila ni lugha ambayk haina siri kwa maana kuwa ukiongea kwa ishara mwingine anaweza kuona Na kujua unachoongea.
Samahn kiongozi ulijifunzia wap
 
Omoyogwane Asante kwa mada hii. Nami ni. Mdau wa lugha hii. Kamusi ya lugha ya alama Tanzania ya ki digital ipo tayari. Wanaweza kuipata online free
 
Habari za saizi wakuu,

Twende moja kwa moja kwenye mada yetu ya Leo.

Lugha ya alama nini?

Lugha ya alama Tanzania ni chombo cha mawasiliano ambacho humuwezesha mzungumzaji kufikisha ujumbe kwa jamii kwa hadhira iliyokusudiwa na jamii husika.

Lugha ya alama imegawanyika katika makundi mawili;

1. Alama kwa njia ya herufi (alphabet)
2. Alama kwa njia ya ishara.

Katika mada hii ntaongelea zaidi kipengele cha kwanza ambacho ni ALAMA KWA NJIA YA HERUFI..

Kwanini?

Kwa sababu kipengele hiki ni rahisi kumfundisha mtu aliye mbali na akaelewa mfano hapa JAMII FORUMS.

Kipengele cha pili hufundishwa MUBASHARA .

Tulisongeshe,

ALAMA KWA NJIA YA HERUFI (ALPHABET)

Herufi A, B, C,D,E,F,G, H,I,J, K, L, M,N,O mpaka Z huweza kuandikika kwa kutumia vidole vyetu.

Mbinu gani hutumika?

Mbinu zitumikazo hapa ni kukunja vidole kwa kufuata umbo la herufi husika.

Mfano herufi "C" ukitizama katika picha hapo chini utaona KIDOLE GUMBA na vidole vingine vimekunjwa kuunda shape ya herufi C. Utaratibu huu pia hutumika katika kuandika herufi zinazo fuata.

NB: Herufi "I" na "J" katika picha utaona kama zinafanana, utaratibu wa kuzitofautisha upo hivi, UKITAKA KUANDIKA HERUFI J ANZA KWA KUANDIKA HERUFI ,"I" THEN KUWA KAMA UNACHORA HERUFI J HEWANI.

72453ddd3ee3cd7b225040237ac64135.jpg

55ac6f54a4f4accaf3df94ff08e5cb9d.jpg


Wakuu TUMIENI umakini kuchunguza MIKUNJO YA VIDOLE pamoja na alama husika mtagundua mikunjo ya vidole na imekunjwa kwa kufuata UMBO LA HERUFI HUSIKA. Mfano mzuri tizameni herufi Y.

HERUFI HIZI HUTUMIKA JE?

Herufi hizi hutumika kwa kuandika neno au maneno uliyokusudia kwa mhusika (kiziwi) kwa kufuata herufi tajwa hapo juu katika picha.

Jaribu sasa kwa kuanza na maneno kama DADA, KAKA, MAMA, BIBI n.k,
Ni rahisi sana na utaweza kuwasiliana au kuongea na kiziwi yeyote.

Karibuni kwa nyongeza , maoni, hoja na maswali.

Ahsanteni.
Nilimsikia mtaalam mmoja akizungumza na BBC kutoka Arusha akisema hakuna standard language ya kuwasiliana na hao watu
 
Nilimsikia mtaalam mmoja akizungumza na BBC kutoka Arusha akisema hakuna standard language ya kuwasiliana na hao watu
Ipo mkuu. Kuna hii inaitwa international sign language. Hapa Kama Kuna viziwi kutoka sehemu mbali mbali inatamika hii
 
Unaweza kuwasiliana na Kiziwi anayeongea Kiingereza Kwa alama hizo ?
 
Omoyogwane Asante kwa mada hii. Nami ni. Mdau wa lugha hii. Kamusi ya lugha ya alama Tanzania ya ki digital ipo tayari. Wanaweza kuipata online free
Uzi uendelee kuna wadau watakuja kutoa elimu.

Siku hizi UDOM kuna digrii ya ualimu kwa watu wa makundi maakumu na wenye uhitaji


Wanafundisha alama
 
Nilimsikia mtaalam mmoja akizungumza na BBC kutoka Arusha akisema hakuna standard language ya kuwasiliana na hao watu
Ni kweli

Alama za KOREA na Tanzania .ni tofauti

Alama sio constant ni kama lugha zingine
 
Samahn kiongozi ulijifunzia wap
Mm nilijifunza chuoni japo vyuoni hua huwafundisha vitu vingi. Ila mm kiukweli nimejifunza sana mtaani kwa viziwi wenyewe, pia kamusi za lugha ya alama na videos mbali mbali
 
Omoyogwane Asante kwa mada hii. Nami ni. Mdau wa lugha hii. Kamusi ya lugha ya alama Tanzania ya ki digital ipo tayari. Wanaweza kuipata online free
Yah sasa ipo japo bado hawajaitangaza na hasa kwa ajili ya ufundishaji shuleni
 
kwahiyo sentence nzima unakuwa unafanya spelling!?
Hapana spelling ni kwa kuandika kwa mfano neno lisilokuwa na alama au alama huiji hapo utapeli. Ila kila neno lina alama yake kwa hio utatumia alama hizo kuunda sentence
 
Fingers spell au tahajia ya vidole ,hutumika kuelezea majina ya mtu au sehemu .au misamiati isiyo na alama. Kuhusu sentensi lugha ya alama ni tofauti na kiswahili . Kwenye LAT unafikishwa ujumbe muhimu tu . Na sio sentensi nzima
 
Back
Top Bottom