Janga la corona, limedhihirisha kwamba wazungu ni waoga, sijui kwa sababu wote wamesoma.. unajua kuto kusoma nako ni faida kwa kuchukulia mambo poa.
Wazungu saizi wanaogopa corona kuliko hata simba wakati africa bando matangazo ya disco na sherehe yanaendelea kubandikwa.
Tumeona wazungu wakikimbia africa, wana amini watakufa na corona, lakini cha kushangaza hakuna corona africa kama ilivyo kwa wazungu.
WHO ilitabiri kuona maiti zikizagaa wakasahahu kwamba bara la africa ndilo lenye binadamu fit wenye afya kuliko mabara mengine. Africa hakuna huduma za afya ukiona mtu anatembea ujue yupo fit.
Naomba nikusahihishe, ni culture yao kuchukulia mambo very seriously, mfano
1. Huwezi kukuta kwao mzungu anaendesha baiskeli bila kuvaa helmet let alone pikipiki.
2. Ukipiga simu polisi utawaona mlangoni kwako ndani ya sekunde chache.
3. Gari inayotembea barabarani ni lazima iwe imechekiwa na imepewa certificate kwamba ni roadworthy.
4. Mitaa karibu yote ina street cameras kwa ajili ya usalama.
5. Uingereza club zinafungwa saa nane za usiku, muda ukikaribia polisi wanasogea. Lakini uongozi wa club unaobserve muda wa kufunga bila kulazimishwa.
6. Ukiwa under 16 huwezi kuendesha gari barabarani, na wote wanatii.
7. Under 16 huruhusiwi kuingia club, hata ukipenya wahudumu hawatakuuzia kileo
8. Kuna muda ukifika huruhusiwi kupiga honi ya gari
9. Misikini na makanisa lazima yawe na sound proof.
10. Kukitokea jambo kama mauaji wanafanya thorough investigation na inaundwa kamati kuangalia chanzo cha tatizo na wanatoa recommendations nini kifanyike ili tatizo hilo lisijirudie tena.
Mfano tu kulikuwa na mauaji ambayo hawakuwahi kuyashuhudia UK, mtu mwenye asili ya Afrika aliuawa kwa kukatwa vipande, akafungwa kwenye kiroba na kutupwa mto Thames.
Polisi walifanya uchunguzi na wakawapata wahalifu. Kilichowashangaza ni aina ya mauaji, ikabidi waanze kuchunguza why, wakagundua kuwa ilikuwa ni rituals za wanaijeria. Polisi walikwenda Nigeria vijijini kuwaona waganga na wazee wa jadi ili kupata taarifa za kwanini mauaji yanafanyika kwa staili hizo.
Ndio maana unawaona ni waoga, hiyo ni style yao ya maisha. Hawafanyi mambo kiholela kama huku kwetu, ndio maana kuna tofauti kubwa ya maendeleo kati yetu na wao.
Sent using
Jamii Forums mobile app