Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Visa vipya vitatu (3) vimeripotiwa nchini Bahrain. Watu watatu waliorejea nchini humo wakitokea nchini Iran.
 
UPDATE: Ufaransa imeripoti visa vipya 43 nchini humo na kufikisha jumla ya visa 100 huku wagonjwa wapatao nane (8) wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Wagonjwa 12 wamepata ahueni huku wagonjwa wapatao wawili (2) wakipoteza maisha kutokana na virusi vya Corona nchini humo hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya nane (8) vimeripotiwa nchini humo. Visa hivyo vinajumuisha;
  • Visa vitatu (3) kutoka mjini Madrid
  • Visa viwili (2) kutoka katika jimbo la Catalonia
  • Kisa kimoja (1) kutoka mjini Valencia
  • Kisa kimoja (1) kutoka katika visiwa vya Baleari
 
UPDATE: Uholanzi

Visa vipya vinne (4) vimeripotiwa nchini humo.

Visa viwili (2) kati ya hivyo ni mwenzi pamoja na mtoto wa mwisho wa mgonjwa wa pili kuripotiwa nchini humo

Visa vingine viwili (2) ni mke pamoja na binti wa mgonjwa wa kwanza kuripotiwa huko Loon op Zand mjini Tilburg.
 
UPDATE: Uingereza imeripoti visa vipya vitatu (3) nchini humo.

Wawili (2) kati ya wagonjwa hao walikuwa wamerejea nchini humo hivi karibuni wakitokea nchini Italia huku mwingine mmoja (1) akirejea nchini humo kutokea barani Asia.
 
UPDATE: Singapore imeripoti visa vipya vinne (4) na kufikisha jumla ya visa 102 vilivyothibitika nchini humo hadi hivi sasa huku ikiwa ni nchi ya sita kwa kuripoti visa vingi zaidi duniani.

Wagonjwa wapatao saba (7) kati yao wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 72 wakipata nafuu.
 
UPDATE: Visa vipya vitano (5) vimeripotiwa nchini Iraq huku vinne (4) kati ya hivyo ni kutokea mjini Baghdad na kisa kingine kimoja (1) kikitokea katika mkoa wa Babil.
 
UPDATE: China

Wizara ya afya nchini humo imeripoti visa vipya 573 pamoja na vifo vipya 35 nchini humo huku visa 570 na vifo 34 vikiripotiwa katika mkoa wa Hubei pekee.

Hadi hivi sasa, China imekwisharipoti visa vipatavyo 79,824 pamoja na vifo 2,870 nchini humo tokea mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) ulipoanza huku wagonjwa wapatao 41,825 wakiripotiwa kupata nafuu na wengine 7, 365 wakiwa katika hali mbaya zaidi.
 
UPDATE: Korea Kusini

Visa vipya 376 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 3,526 vilivyothibitika hadi sasa nchi nzima huku idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona nchini Korea Kusini ni 17 hadi sasa.
 
UPDATE: Australia imeripoti kifo cha kwanza (1) kinachohusishwa na virusi vya Corona nchini humo. Ni miongoni mwa abiria waliokuwemo katika meli ya Diamond Princess.
 
UPDATE: Australia imeripoti kifo cha kwanza (1) kinachohusishwa na virusi vya Corona nchini humo. Ni miongoni mwa abiria waliokuwemo katika meli ya Diamond Princess.
Vp mkuu kwa nchi za Algeria, na Nigeria kuliporipotiwa visa vya kwanza hakuna update yoyote ya either patients zaidi au recovery ya mgonjwa husika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Korea Kusini

Visa vipya 376 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 3,526 vilivyothibitika hadi sasa nchi nzima huku idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona nchini Korea Kusini ni 17 hadi sasa.
Mkuu inamana Korea kaskazini bado hawana mgonjwa hata mmoja ama kunakitu kisicho eleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri kasema wageni hawana corona na ukumbuke Waziri wetu wa afya ni mjuzi sana ,tena kuliko mawaziri na wataalam wengine wa afya dunian

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…