Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Ila pia nina imani kwa mbali sana na kauli kuwa black people hawapati corona kwasababu, ugonjwa umelipuka maeneo ya wuhan ambapo kuna population ya watu mil 10 na ndipo ambapo kuna vyuo vingi sana china na inasemekana mpk mwaka 2018 inchi za africa zote kwa pamoja zina idadi ya wanafunz elfu 6 waliokuwa wanasoma katika vyuo mbali mbali pale china especially mji wa wuhani, lakini pia wuhan ndipo ambapo pia kuna masoko so interaction kati ya wa china na waafrica ni kubwa sana ila mpk kufikia leo ambapo pale china tu kuna maambukizi takriban 780000 na vifo zaidi ya 2800 hakuna black people hata mmoja aliyestukiwa na ugonjwa wala kufariki kwa sababu ya huo ugonjwa, kwa hayo tu basi inatosha kusema kwamba corona ni km mafua na hayana impact kwa black people,
Unless otherwise mwenyezi MUNGU aendelee kutunusuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila pia nina imani kwa mbali sana na kauli kuwa black people hawapati corona kwasababu, ugonjwa umelipuka maeneo ya wuhan ambapo kuna population ya watu mil 10 na ndipo ambapo kuna vyuo vingi sana china na inasemekana mpk mwaka 2018 inchi za africa zote kwa pamoja zina idadi ya wanafunz elfu 6 waliokuwa wanasoma katika vyuo mbali mbali pale china especially mji wa wuhani, lakini pia wuhan ndipo ambapo pia kuna masoko so interaction kati ya wa china na waafrica ni kubwa sana ila mpk kufikia leo ambapo pale china tu kuna maambukizi takriban 780000 na vifo zaidi ya 2800 hakuna black people hata mmoja aliyestukiwa na ugonjwa wala kufariki kwa sababu ya huo ugonjwa, kwa hayo tu basi inatosha kusema kwamba corona ni km mafua na hayana impact kwa black people,
Unless otherwise mwenyezi MUNGU aendelee kutunusuru

Sent using Jamii Forums mobile app
This time hilo ni janga lao white people na watajuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majinga sana yani
Hii inaonesha jinsi gani alivyo na akili za ajabu
Kulingana taarifa ya jana ya waziri wa afya ummy mwalimu, nina kila sababu ya kuisi kwamba ugonjwa umefika tz ila labda wanaficha tu kwasababu tayar walishafanya makosa ya kuwakaribisha wachina ambao kimsingi ndio super-spreader,
Kauli inayonipa shaka mpk ss
1. Kutoa agiza kwa kila mkuu wa mkoa kuandaa sehemu ambayo watahifadhiwa watakaostukiwa kuwa nao
2. Ujaji wa wageni elfu 11 na wote kuwa salama hali ya kuwa huu ugonjwa huwa unavumbuka mpk siku 14 mara baada ya mgonjwa kupata maambukizi.



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Ufaransa imeripoti visa vipya 30 na kufikisha jumla ya visa 130 hadi sasa huku wagonjwa wawili (2) wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na virusi vya Corona nchini humo hadi hivi sasa.

Wagonjwa wapatao tisa (9) wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi na wagonjwa wapatao 12 wakipata nafuu huku kukiwa na uwezekano wa visa vipya kuripotiwa zaidi.
 
Sasa kwa hawa walioingia majuzi hapa huwezi jua kama wameibeba

Sent using Jamii Forums mobile app
Ili kujua kama wana maambukizi ama wako salama wanapaswa kufanyiwa screening kama utaratibu ulivyo katika mataifa mengine mara tu waingiapo nchini.

Lakini, thermal screening ni hatua ya mwanzo tu na si hitimisho la kuthibitisha kuwa mtu hana kabisa maambukizi kulingana na tafiti zilizofanyika.

Mara nyingi screening huonesha maambukizi pale ambapo mgonjwa tayari ameanza kuonesha dalili maana kinachopimwa ni joto la mwili na inaweza kuchukuwa muda wa siku kadhaa tokea mtu kuambukizwa na joto ama dalili za homa kuonekana.

Hatua inayopaswa kufanyika baada ya hapo ni kuweka utaratibu wa karantini kwa muda wa siku 14 na kuendelea hususani kwa wale wanaotokea katika mataifa yaliyoathirika zaidi huku vipimo vya mara kwa mara vikiendelea.
 
UPDATE: Misri imeripoti kisa kipya ambacho ni kisa cha pili cha virusi vya Corona kuripotiwa nchini humo hadi sasa.

Mtu huyo ni raia wa kigeni ambaye uraia wake haukutajwa, tayari amekwishawekwa katika uangalizi maalumu, Wizara ya afya ya nchi hiyo imethibitisha.

Hiki ni kisa cha nne kuripotiwa barani Afrika.

Taarifa zaidi zitafuata.
 
NEWS ALERT: Egypt detects second case of new coronavirus: health ministry. [Reuters]

Egypt’s health ministry announced on Sunday that one foreigner was tested positive for the new coronavirus strain inside Egypt, the ministry said in a statement on its Facebook page.

The ministry said that the person, whose nationality was not announced, was taken to an isolation hospital and is currently receiving the necessary medical care. It also added that it is currently taking strict preventive measures regarding those who were in contact with the person.

It is the second case of new coronavirus detected in Egypt. The first person has recovered, the statement said.
 
UPDATE: Ujerumani

Hadi hivi sasa, visa vipatavyo 130 vimeripotiwa nchini humo, wagonjwa wapatao wawili (2) wakiwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 16 wakiripotiwa kupata nafuu.

Hadi hivi sasa, Ujerumani haijaripoti kifo chochote kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Italia

Mpaka sasa, visa vipatavyo 1,694 vimeripotiwa nchini humo, wagonjwa wapatao 140 wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 83 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo ni 34 hadi sasa.
 
UPDATE: Japan

Hadi sasa, visa vipatavyo 256 vimeripotiwa nchini humo, wagonjwa wapatao 19 wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 32 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo ni sita (6) hadi sasa.
 
UPDATE: Uhispania

Mpaka hivi sasa, visa vipatavyo 84 vimeripotiwa nchini Uhispania, wagonjwa watano (5) wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine wawili (2) wakiripotiwa kupata nafuu.

Hadi sasa, Uhispania haijaripoti kifo chochote kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Thailand imeripoti kifo cha kwanza (1) nchini humo kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19).

Mpaka sasa, visa vipatavyo 42 vimeripotiwa nchini Thailand huku mgonjwa mmoja (1) akiripotiwa kuwa mahututi na wengine 30 wakiripotiwa kupata ahueni.
 
UPDATE: Iran

Mpaka hivi sasa, visa vipatavyo 978 vimeripotiwa nchini humo huku wagonjwa wapatao 140 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo ni 54 hadi sasa.
 
UPDATE: Meli ya Diamond Princess

Visa vipatavyo 705 vimeripotiwa katika meli hiyo huku wagonjwa wapatao 36 wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 10 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) kwa wagonjwa waliokuwemo katika meli hiyo ni sita (6) hadi sasa.

1583111197536.png
 
UPDATE: Singapore

Hadi sasa, visa vipatavyo 106 vimeripotiwa nchini humo huku wagonjwa wapatao saba (7) wakiripotiwa kuwa katika hali ya umahututi na wengine 74 wakiripotiwa kupata nafuu.

Mpaka sasa, Singapore haijaripoti kifo chochote kinachotokana na virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Nchi ya San Marino ambayo ni miongoni mwa nchi ndogo zaidi duniani imeripoti kifo cha kwanza (1) nchini humo kilichotokana na virusi vya Corona sambamba na visa vipya saba (7).
 
BREAKING: Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 202 pamoja na vifo vipya 42 nchini humo.

Visa 196 kati ya visa vipya vilivyoripotiwa pamoja na vifo vyote 42 ni kutoka katika mkoa wa Hubei pekee.
 
UPDATE: Visa vipya viwili barani Afrika nchini Algeria

Algeria imethibitisha visa vipya viwili (2) nchini humo Jumatatu. Visa hivyo vimetajwa kuwa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 53 pamoja na bintiye mwenye miaka 24, Wizara ya afya ya nchi hiyo imesema.

Watu hao wawili wametengewa sehemu maalumu katika jimbo la Blida kusini mwa mji mkuu Algiers, Wizara imeeleza.

Ongezeko hilo linapelekea idadi ya visa vyote kuripotiwa nchini humo kufikia tatu (3) hadi sasa.
 
Back
Top Bottom