Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Korea Kusini imeripoti visa vipya 145 hivyo kufikisha jumla ya visa 5,766 nchini humo hadi hivi sasa ambapo wagonjwa wapatao 52 wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 88 wakipata ahueni.

Korea Kusini imekwisha ripoti vifo vipatavyo 35 hadi hivi sasa vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Japan

Visa vipya 12 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 331 nchi nzima hadi hivi sasa ambapo wagonjwa wapatao 29 wako katika hali mbaya zaidi (mahututi) huku wengine 10 wakiripotiwa kupata ahueni.

Mpaka sasa, Japan imekwisha ripoti vifo vipatavyo sita (6) vitokanavyo na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Iran

Visa vipya 591 vimeripotiwa nchini humo sambamba na vifo vipya 15 na kufikisha jumla ya visa 3,513 huku wagonjwa wapatao 552 wakiripotiwa kupata nafuu.

Vifo vipatavyo 107 vimekwisha ripotiwa nchini humo hadi hivi sasa vilivyotokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19).
 
UPDATE: Urusi imeripoti kisa kipya (1) nchini humo na kufikisha jumla ya visa vipatavyo vinne (4) hadi hivi sasa huku wagonjwa wawili (2) wakiripotiwa kupata nafuu.
 
UPDATE: China

Hadi hivi sasa;

  • Visa 80,409 vimeripotiwa nchini humo
  • Vifo 3,012 vimeripotiwa nchini humo
  • Wagonjwa 5,952 wako katika hali mbaya zaidi
  • Wagonjwa 52,045 wamepata ahueni
 
UPDATE: Ubelgiji imeripoti visa vipya 27 nchini humo na kufikisha jumla ya visa 50 hadi sasa huku mgonjwa mmoja (1) akiripotiwa kupata nafuu.
 
UPDATE: Malaysia imeripoti visa vipya vitano (5) nchini humo nakufikisha visa 55 nchi nzima huku wagonjwa wapatao 22 wakiripotiwa kupata nafuu.

Mpaka hivi sasa, Malaysia haijaripoti kifo chochote kinachohusishwa na COVID-19 nchini humo.
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya sita (6) vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 248 nchi nzima ambapo wagonjwa wapatao saba (7) wameripotiwa kuwa mahututi huku wengine wawili (2) wakipata ahueni.

Uhispania imekwisha ripoti vifo vipatavyo vitatu (3) vinavyohusishwa na COVID-19 nchini humo.
 
UPDATE: China

Hadi hivi sasa;

  • Visa 80,409 vimeripotiwa nchini humo
  • Vifo 3,012 vimeripotiwa nchini humo
  • Wagonjwa 5,952 wako katika hali mbaya zaidi
  • Wagonjwa 52,045 wamepata ahueni
Kwa hiyo mkuu kwa tathmini za haraka haraka huu ugonjwa hauonekani japo kupungua hata mara moja hasa hapo kwenye main point yake China zaidi unazidi kuenea?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…