Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Uhispania

Idadi ya visa vyote ni 1,695 hadi sasa nchi nzima.

Wagonjwa wapatao 101 wako katika hali mbaya zaidi huku idadi ya vifo ikifikia 36 hadi sasa.

Idadi ya waliopata nafuu imefikia 135 mpaka sasa nchini humo.

Nchi hiyo imesitisha safari zote za ndege kutokea nchini Italia.
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vyote nchini humo vimefikia 1,565 nchi nzima hadi sasa.

Wagonjwa wawili (2) wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku idadi ya waliopata ahueni ikifikia 18.

Hadi sasa, Ujerumani imekwisha ripoti vifo viwili (2) vinavyohusishwa na virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Japan

Idadi ya visa vyote ni 581 nchi nzima hadi sasa huku idadi ya vifo ikifikia 10.

Wagonjwa wapatao 31 wako katika hali mbaya zaidi. Waliopata nafuu wafikia 59 hadi sasa nchi nzima.

Nchi hiyo imezindua mpango mkakati wa dola za Kimarekani bilioni 4 ili kukabiliana na janga la virusi vya Corona nchini humo.
 
UPDATE: Norway

Idadi ya visa vyote nchini humo ni 400 hadi hivi sasa.

Hakuna ripoti ya vifo vilivyotokana na virusi vya Corona nchini humo mpaka sasa.

Shirika la ndege la Norwegian limesitisha safari zake takribani 3000 kuanzia katikati ya mwezi Machi hadi katikati ya mwezi Juni kutokana na kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
 
UPDATE: Marekani

Idadi ya visa vyote imefikia 1000 hadi sasa.

Idadi ya vifo imefikia 30 huku wagonjwa nane (8) wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 9 wakipata nafuu.
 
UPDATE: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeripoti kisa cha kwanza (1) nchini humo na kuwa nchi ya 11 ya Afrika kuthibitisha visa vya COVID-19.

Mgonjwa huyo ni Mkongo wa miaka 52 anayeishi Ufaransa, ambaye aliingia nchini humo siku ya Jumapili na alikuwa amewekwa karantini baada ya uchunguzi aliofanywa katika uwanja wa ndege wa Kinshasa kubaini kuwa ana ishara za mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona.

Mgonjwa huyo kwa sasa ametengwa huku akipatiwa matibabu mashariki mwa mji wa Kinshasa.

Waziri wa afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eteni Longondo ametoa wito kwa watu kuwa watulivu na kuzingatia usafi kwa kuosha mikono yao mara kwa mara.
 
NEWS ALERT: EU pledges $28bn to tackle coronavirus crisis

The European Commission will set up an EU fund worth 25 billion euros ($28bn) to tackle the economic crisis caused by the coronavirus outbreak, the head of the EU executive branch said. [Al Jazeera]
 
Kuhusu DRC; Taarifa za awali zilidai kuwa kisa ambacho ni cha kwanza nchini humo ni raia wa Ubelgiji ambaye amekuwepo nchini humo (DRC) kwa muda wa siku kadhaa.

Lakini taarifa ya baadaye kutoka Wizara ya afya imedai kuwa, kisa hicho ni raia wa Kongo, ambaye amewekwa karantini nchini humo.
 
UPDATE: Kifo cha kwanza kimeripotiwa nchini Morocco.

Kifo hicho kinahusisha mwanamke ambaye ni raia wa Morocco, 89, aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na moyo, Wizara ya afya ya nchi hiyo imeeleza.
 
NEWS ALERT: Italy is the first European country to put more than 60 million people on lockdown to stem the spread of coronavirus. [Al Jazeera]

All sporting events, schools and universities have been cancelled. Places of public gathering such as cinemas, theatres and nightclubs remain closed.

Religious ceremonies including funerals and weddings will also be postponed.

1583902642357.png
 
NEWS ALERT: Safari za ndege zasitishwa

Uingereza:
Shirika la ndege la Uingereza, British Airways, limesitisha safari zake za Italia baada ya nchi hiyo kuwekwa kizuizini hadi mwezi Aprili ili kukabiliana na virusi vya Corona.

Israel: Shirika la ndege la Wizz Air limesitisha safari zake kati ya Israel na Italia ikiwa ni hatua ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ili kukabiliana na virusi vya Corona

Denmark: Waziri mkuu wa nchi hiyo Mette Frederiksen ametangaza kusitishwa kwa safari za ndege kuingia nchini humo kutoka katika mataifa yaliyoathirika zaidi kama vile Italia, Iran na Korea Kusini.

Uhispania: Serikali imetangaza kusitishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja kutokea nchini Italia kwa muda wa wiki mbili ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Ureno: Serikali imetangaza kusitishwa kwa safari za ndege za abiria za kwenda na kutokea Italia kwa muda wa siku 14 kuanzia Jumatano ikiwa ni hatua mojawapo ya kuzuia kuenea zaidi kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Canada: Shirika la ndege la nchi hiyo, Air Canada, limesitisha safari zote za kwenda na kutokea Italia hadi mwezi Mei kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.
 
Ukichukua total cofirmed cases toa recoveries na death unapata (80778-(61475+3158)= 16145)

Kwa maneno mengine mpaka sasa wagonjwa walioko china ni kwenye elf16 [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] wakati mahospitali yamefurika
Hesabu haidanganyi Mkuu..

Tupe majibu sahihi uliyopata baada ya kuhesabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukichukua total cofirmed cases toa recoveries na death unapata (80778-(61475+3158)= 16145)

Kwa maneno mengine mpaka sasa wagonjwa walioko china ni kwenye elf16 [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] wakati mahospitali yamefurika


Sent using Jamii Forums mobile app
😆😆😆😆 nimecheka utadhani mazuri
 
Back
Top Bottom