Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Korea Kusini

Visa vipya 114 pamoja na vifo vipya sita (6) vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 7,869 huku wagonjwa wapatao 36 wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 333 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia 66 hadi hivi sasa.
 
Is China downplaying its numbers?
inawezekana china kweli imeudhibiti na inajitahidi huu ugonjwa kwa mujibu wa mitandao yao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti kasi ya maambukizi hata km unakumbuka kuna memba humu mchina bakary jinsi alivyoeleza naweza kubari kabisa wamejitahidi kuudhibiti kimbembe kipo ulaya huko walijiachia km tunavyojiachia sisi hadi ulivyowafika ndo wakazinduka wkt ushasambaaa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Iran

Visa vipya 1,075 sanjari na vifo vipya 75 vimeripotiwa nchini humo.

Hadi sasa, idadi ya visa vyote nchini humo imefikia 10,075 huku idadi ya waliokufa ikifikia 429.

Wagonjwa walioripotiwa kupata ahueni wamefikia 2,959.

Makamu wa kwanza wa rais wa nchi hiyo, Eshaq Jahangiri, pamoja na mawaziri wawili wamebainika kuwa na maambukizi ya COVID-19, shirika la habari la Fars (FNA) limeripoti.
 
NEWS ALERT: Iran's senior vice president and two other cabinet members have the new coronavirus, the semiofficial Fars news agency reported.

The news report on Wednesday comes amid days of speculation about the health of Vice President Eshaq Jahangiri, who has not been seen in images of recent top-level meetings.

Fars said other sick officials are Ali Asghar Mounesan, minister of cultural heritage, handicrafts and tourism, and Reza Rahmani, minister of industry, mines and business. [Al Jazeera]
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 546 pamoja na vifo vipya viwili (2) vimeripotiwa nchini humo.

Mpaka kufikia sasa, jumla ya visa 2,512 vimeripotiwa nchi nzima ambapo wagonjwa wapatao 25 wameripotiwa kupata ahueni huku wengine wawili (2) wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Ujerumani imekwisha ripoti vifo vitano (5) hadi sasa vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Italia

Visa vipya 2,651 pamoja na vifo vipya 189 vimeripotiwa nchini humo.

Mpaka hivi sasa, Italia imekwisha ripoti jumla ya visa 15,113 pamoja na vifo 1016 vilivyosababishwa na COVID-19.

Kati ya visa vyote, wagonjwa wapatao 1,153 wako katika hali mbaya zaidi huku wengine 1,258 wakiripotiwa kupata nafuu.

Serikali imeamuru maduka, baa na migahawa yote nchi nzima kufungwa.
 
Wataalamu wanatuambia virusi hivii havistawi katika sehemu zenye joto Kama huku Africa na nchi za kitropiki
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya 782 pamoja na vifo vipya 31 vimeripotiwa nchini Uhispania.

Mpaka kufikia sasa, jumla ya visa 3,059 vimeripotiwa nchi nzima pamoja na vifo vipatavyo 86.

Idadi ya waliopata ahueni imefikia 189 huku wagonjwa wapatao 190 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Mechi ya soka ya ligi ya Europa kati ya klabu ya Sevilla ya nchini humo na Roma ya Italia iliyopangwa kuchezwa mnamo Alhamisi imeghairishwa kutokana na virusi vya Corona.
 
Trump atangaza kwa mbwembwe na kukosea kilichokusudiwa kuhusu Safari za Ulaya
Habari sio nzuri huku watu wanahaha na kukusanya chakula
Lakini yatapita


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
UPDATE: Barani Afrika

1. Algeria imeripoti visa vipya vitano (5). Miongoni mwa visa hivyo kimeripotiwa kifo cha kwanza nchini humo. Mpaka sasa nchi hiyo imekwisha ripoti visa vipatavyo 24.

2. Afrika Kusini imeripoti visa vipya vinne (4) na kufikisha jumla ya visa 17 hadi sasa.
 
Kiuhalisia uchumi wa dunia utapungua na hasara haitasahaulika

Sent using Jamii Forums mobile app
mpk sasa me binafs nishaanza onja joto ya kiuchumi kuna baadhi ya mari zishaanza kuadimuka kiwandani kuna bidhaa za kiwandani zinatoka korea kwakweli bei wamepandisha maradufu
mm nalalamika bei imepanda ghafla wanipunguzie
wezangu wanagombea kutahamaki mari hakuna dah !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa huu mwandiko inaonyesha unamiliki kiwanda cha wanzuki au kiwanda cha gongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…