FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
- Thread starter
- #241
Coronavirus: Je nchi za Afrika ziko tayari kukabiliana na janga hili?
Afrika ni moja ya mabara mawili ambayo bado hayajathibitisha kisa chochote cha virusi vya corona ingawa wataalamu wameonya kuwa hilo huenda lisiendelee kwa kipindi kirefu kwasababu ya uhusiano wa bara hilo na China.
Wiki iliyopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kwamba mlipuko wa virusi vya corona ni ugonjwa wa dharura kwa dunia nzima kwasababu ya hofu kwamba nchi maskini huenda zikashindwa kukabiliana na mlipuko huo.
"Sababu kuu ya kutambua virusi hivi kama hali ya hatari duniani sio Uchina, lakini kile kinachotokea katika nchi zingine. Wasiwasi wetu mkubwa ni uwezo wa kusambaa kwa virusi hivyo, katika nchi zenye mfumo dhaifu wa afya," amesema mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, kutoka Ethiopia.
Mifumo ya afya katika nchi nyingi za Afrika tayari inakabiliwa na ugumu wa kazi zilizolimbikizana, na hapo ndipo tunapojiuliza, je nchi hizi zinaweza kukabiliana na mlipuko kama huu ambao unasambaa kwa haraka mno?
Michael Yao, Mkuu wa huduma za dharura eneo la Afrika, amesema "baadhi ya nchi za Afika sio kwamba hazina pa kuanzia lakini uwezo ni mdogo sana".
"Tunajua vile mfumo wa afya ulivyo dhaifu katika bara la Afrika na mifumo hii tayari inazidiwa na milipuko ambayo inaendelea kujitokeza, kwa hiyo kwetu sisi ni muhimu kuutambua mapema kama janga ili tuweze kudhibiti usambaaji wake."
[BBC]