Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Miji mingi wamesha rudi makazini na ukiwauliza wana kuambia kila kitu kipo under control na serekali ya watu wa china !
Hawasemi sijuwi mhemiwa nani au mtu kufu nani dah wao ni serekali ya watu wa china!
Tuna kwama wapi kila neno jiwe!
Screenshot_20200213_214456.jpg
 
Wakuu mazingira ya utoaji taarifa China ni sahihi? Wadau wengine kama WHO na mataifa washirika wanapata fursa kuratibu taarifa sahihi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Japan imeripoti kifo cha kwanza kabisa nchini humo kutokana na virusi vya Corona.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Kazi na Ustawi ya nchini humo.
 
UPDATE: Singapore imeripoti visa vipya nane (8) vya COVID-19 nchini humo hii leo.

As of 13 February 2020, the Ministry of Health (MOH) has confirmed and verified eight additional cases of COVID-19 infection in Singapore, all of which are linked to previous cases. [Singapore's Ministry of Health]
 
UPDATE: Taarifa kuhusiana na meli ya Diamond Princess iliyopo karantini nchini Japan:

Watu wengine takribani 44 waliokuwa katika meli hiyo wamebainika kuwa na maambukizi ya COVID-19 hii leo na mpaka sasa jumla ya watu takribani 218 waliokuwa katika meli hiyo wamebainika kuwa na maambukizi.

1581625591531.png
 
UPDATE: Hong Kong imeripoti visa vipya vitatu (3) hii leo. Jumla ya visa vyote vilivyobainika Hong Kong mpaka sasa ni 53.

Report from Hong Kong:
The Centre for Health Protection (CHP) of the Department of Health (DH) announced that as of 8pm today (February 13), the CHP is investigating three additional case of novel coronavirus infection, taking to 53 the number of confirmed cases so far in Hong Kong.
 
Korea Kaskazini: Kuna taarifa za uwepo wa visa vitano (5) mpaka saba (7) nchini humo lakini bado hakuna taarifa rasmi.

Tuendelee kusubiri.
 
CORONAVIRUS: Vifo 1370 pamoja na Visa 60,390 hadi sasa | 1370 Dead and 60,390 Cases

Nchini China, miji kadhaa imefungwa hivi sasa na watu wametakiwa kubaki ndani ya nyumba zao huku huduma muhimu zikitolewa na serikali za mitaa katika baadhi ya maeneo huku pia mamlaka za baadhi ya maeneo nchini humo zikitoa tangazo la kukamata wale watakaokiuka agizo hilo na kutoka bila kibali maalumu.

Biashara zimesimamishwa kwa muda huku wafanyakazi wakibaki katika makazi yao wakati ambao serikali pamoja na wadau mbalimbali wakiendelea kukabiliana na mlipuko wa janga hilo.
 
BREAKING: Kutoka Hubei nchini China, vifo vipya 116 pamoja na visa vipya 4,823 vimeripotiwa.
 
UPDATE: Idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya Corona (COVID-19) mpaka sasa yafikia 1,483.

Idadi hiyo ni kwa mujibu wa taarifa rasmi.
 
CORONAVIRUS: TOTAL

Total Cases: 65,210
Total Deaths: 1,486
Total Recoveries: 5,954


1581642684958.png
 
IMPORTANT: Should you wear a medical mask to avoid Coronavirus?

If you're coughing or sneezing, it is advised that you wear one.

But there is no need if you don't have any symptoms.

A mask alone won't stop infections so be sure to wash your hands and cover sneezes and coughs.

[UNICEF]
 
Ulaya: Mawaziri wa EU waimarisha maandalizi ya kupambana na virusi vipya

Mawaziri wa Afya wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana Jumatano (13.02.2020) kuimarisha maandalizi na kuweka mpango wa pamoja wa kuvizuia virusi vya corona ambavyo vimezuka nchini China dhidi ya kusambaa zaidi kote Ulaya.

Katika mkutano wa dharura mjini Brussels, maafisa kutoka mataifa 27 wanachama wa umoja huo wamesema wanahitaji kupanga zaidi ili kuepuka uhaba wowote wa madawa au vifaa ya kujikinga wakati wa mripuko huo, ambao Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema ni tishio kwa afya ulimwenguni.

Kwa mujibu wa maafisa wa afya wa China, mripuko huo umewaambikiza watu 53,000 kote duniani na kuwauwa zaidi ya 1,300 ambapo asilimia 99 vimetokea China. Watalaamu wanaamini idadi halisi ya visa vya mripuko huo huenda vikawa juu zaidi. [DW]
 
Back
Top Bottom