Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Visa vipya vya COVID-19
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Thailand na kufikia jumla ya visa 43 nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Australia na kufikia jumla ya visa 30 nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Croatia na kufikia jumla ya visa nane (8) nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Austria na kufikia jumla ya visa 15 nchini humo
  • Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa nchini Russia na kufikia jumla ya visa vitatu (3) nchini humo
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 20 vimeripotiwa na kufikisha jumla ya visa 150 nchini humo hadi sasa huku wagonjwa 16 wakiripotiwa kupata ahueni na wengine wawili (2) wakiwa mahututi.

Mpaka sasa, Ujerumani haijaripoti kifo chochote kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
Mkuu naona voice note inatembea mitandaoni kuwa Kenya , hii habari hii kweli?
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 20 vimeripotiwa na kufikisha jumla ya visa 150 nchini humo hadi sasa huku wagonjwa 16 wakiripotiwa kupata ahueni na wengine wawili (2) wakiwa mahututi.

Mpaka sasa, Ujerumani haijaripoti kifo chochote kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa barani Afrika nchini Senegal

Raia wa Ufaransa ambaye amekuwa akiishi nchini Senegal kwa zaidi ya miaka miwili amethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mtu huyo alisafiri kuelekea nchini Ufaransa katikati mwa mwezi Februari na kisha kurejea Senegal mnamo Februari 26 ambapo alikwenda katika kituo cha afya baada ya kuanza kuhisi homa na kichwa kuuma, Wizara ya afya ya Senegal imethibitisha.

Mgonjwa huyo tayari amewekwa katika uangalizi maalumu mjini Dakar nchini humo ambapo kisa hiki ni cha kwanza kuripotiwa nchini Senegal.

Taarifa zaidi zitafuata.
 
UPDATE: Kisa kipya kimoja (1) kimeripotiwa barani Africa nchini Senegal

Raia wa Ufaransa ambaye amekuwa akiishi nchini Senegal kwa zaidi ya miaka miwili amethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mtu huyo alisafiri kuelekea nchini Ufaransa katikati mwa mwezi Februari na kisha kurejea Senegal mnamo Februari 26 ambapo alikwenda katika kituo cha afya baada ya kuanza kuhisi homa na kichwa kuuma, Wizara ya afya ya Senegal imethibitisha.

Mgonjwa huyo tayari amewekwa katika uangalizi maalumu mjini Dakar nchini humo ambapo kisa hiki ni cha kwanza kuripotiwa nchini Senegal.

Taarifa zaidi zitafuata.
Hongera mkuu kwa kuendelea kutuletea taarifa za papo kwa hapo ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Kisa kingine kimoja (1) kimeripotiwa barani Afrika ambacho ni cha kwanza nchini Tunisia.

Tunisia imeripoti kisa cha kwanza cha virusi vya Corona nchini humo. Kisa hiko ni raia wa nchini hiyo (Tunisia) ambaye alirejea nchini humo hivi karibuni akitokea Italia, Wizara ya afya ya nchi hiyo imethibitisha.

Taarifa zaidi zitafuata.
 
UPDATE: Italia

Visa vipya 340 vimeripotiwa nchini humo sanjari na vifo vipya 18 huku kukiwa na uwezekano wa visa vipya kuongezeka zaidi.

Ongezeko hilo linapelekea idadi ya visa vyote nchini humo kufikia 2,036 huku idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona nchini humo ikifikia 52 hadi sasa.
 
UPDATE: Ufaransa

Visa vipya 61 vimeripotiwa nchini humo pamoja na kifo kipya kimoja (1) na kufikisha jumla ya visa 191 pamoja na vifo vitatu (3) nchi nzima hadi sasa.

Wagonjwa wapatao nane (8) nchini humo wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 12 wakiripotiwa kupata nafuu.
 
Back
Top Bottom