Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Italia

Visa vipya 466 vimeripotiwa nchini Italia pamoja na vifo vipya 27 na kufikisha jumla ya visa 2,502 ambapo wagonjwa wapatao 140 wakiwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 160 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia 79 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Ufaransa

Visa vipya 21 vimeripotiwa nchini humo sanjari na kifo kipya kimoja (1) na kufikisha jumla ya visa 212 ambapo wagonjwa wapatao nane (8) wakiwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 12 wakiripotiwa kupata ahueni.

Idadi ya vifo nchini Ufaransa vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia nne (4) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Japan

Visa vipya 19 vimeripotiwa nchini Japan na kufikisha jumla ya visa 293 ambapo wagonjwa wapatao 23 wakiwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 43 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo imefikia sita (6) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya 31 vimeripotiwa nchini humo sambamba na kifo cha kwanza kabisa (1) nchini Uhispania kilichosababishwa na COVID-19.

Kifo cha mgonjwa huyo kilitokea mnamo Februari 13 lakini hapo awali chanzo cha kifo hicho kilitajwa kuwa Nimonia {Pneumonia).

Idadi ya visa vyote nchini humo imefikia 151 hadi sasa ambapo wagonjwa wapatao saba (7) wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi.
 
UPDATE: Visa vipya vitano (5) vimeripotiwa nchini Iraq na kufikisha jumla ya visa 31 nchini humo hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Visa vipya vya COVID-19
  • Visa vipya sita (6) vimeripotiwa nchini Uholanzi na kufikisha jumla ya visa 23 nchini humo huku mgonjwa mmoja (1) akiwa katika hali mbaya zaidi
  • Visa vipya sita (6) vimeripotiwa nchini Austria na kufikisha jumla ya visa 24 nchini humo
 
UPDATE: Uswisi imeripoti visa vipya saba (7) na kufikisha jumla ya visa 37 nchini humo hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Marekani

Visa vipya tisa (9) vimeripotiwa nchini Marekani sambamba na vifo vipya vitatu (3) na kufikisha jumla ya visa 112 huku wagonjwa wapatao saba (7) wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine tisa (9) wakiripotiwa kupata nafuu.

Visa vipya vilivyoripotiwa ni pamoja na kisa cha kwanza katika jimbo la Carolina Kaskazini.

Idadi ya vifo nchini Marekani vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia tisa (9) hadi hivi sasa.
 
UPDATE: China

Mpaka sasa, China imekwisha ripoti visa vipatavyo 80,151 vya COVID-19 nchini humo huku wagonjwa wapatao 6,806 wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi na wengine 47,204 wakiripotiwa kupata nafuu.

China imekwisha ripoti vifo vipatavyo 2,943 vilivyotokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo hadi hivi sasa.
 
MPYA: Korea Kusini imeripoti visa vipya 142 pamoja na kifo kipya kimoja (1) na kufikisha jumla ya visa 5,328 pamoja na vifo 33 nchi nzima.
 
MPYA: Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 119 pamoja na vifo vipya 38 nchini humo.

Visa 115 kati ya hivyo pamoja na vifo 37 miongoni mwa vilivyoripotiwa ni kutokea Hubei pekee.
 
Usikute huu ndo ule ugonjwa ambao yule mke wa kocha wa zamani wa Yanga alisema upo na akataka serikali ifanye uchunguzi.
Alizungumzia kuhusu mafua makali
 
Duuh
Huu ugonjwa huko China haujaanza jana wala juzi, hadi China inautangazia ulimwengu kuwa kuna tatizo la Corona, ni dhahiri kabisa ni baada ya kulemewa na kuanza kusambaa kwa taarifa mitandaoni ndio wakaamua sasa kusema,muda wanaongea huenda tatizo limeshazunguka dunia nzima.

Ni kwamba nilikuwa China mwezi Septemba jimbo moja la Kunming, wakati naondoka Airport ya Bejing Kwenda jimbo la Kunming ndani ya ndege nilishuhudia hali mbaya sana ya afya za abiria wa kichina,walikuwa wakikohoa na makohozi hadi najisikia vibaya,nikishindwa hata kupata breakfast humo,hali hy niliikuta pia kwenye flight to Kunming kwenda Gasa...nikajua ni homa ya mapafu na koo labda kwa vile wachina wanavuta sigara sana.

Niliporudi hapa bongo niliugua sana madonda ya kooni na homa kali baada ya wiki moja mke wangu akaugua na wanangu wawili kwa pamoja,japo wote walipona homa ileile....sasa baada ya ugonjwa ule kutajwa nilipoangalia dalili,ni zilezile.....CORONA...

Ugonjwa humu nchini upo,sema tu huenda kweli waafrika tupo tolerant na ugonjwa huo,ugonjwa huu utakuwa umesambaa dunia nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi kumbe huu ugonjwa upo sana tu.
sahihi mkuu nakumbuka mwezi wa 11 kwenda 12 nilipigwa na mafua makali mpk viungo vikawa havikunji nikawekwa mapumziko mida saa 5 usiku kidspensary cha mtaani pima marelia hakuna lkn homa haishuki jasho linanitililika pua zimebana mbavu zinauma pumzi tabu kupumua haitoki nikahisi nakufa mana sikuwahi kukutana na mafua aina hiyo sasa sikutaka kulazwa mana ningekuwa lelemama ningetiwa drip nikarud home nikameza dawa za marelia zinaitwa ORODAR nikapiga dawa tatu tembe 2 na vidonge fulani vya pumu km ikibanaa sana
then nikavuta shuka nikalala kiubishi toka jasho sana baada masaa km manne homa ikadhuka viungo vikaachia
kesho yake ikawa ahuweni lkn jioni yake wife nae yeye akalazwa na drip akatiwa baada siku 2 ikampata mwanangu sema yeye haikumsumbua sana ila homa ndo ilikuwa shida
baada ya hapo ugonjwa ukahamia job ofisini nzima ikawpata kuna waliolaza na wengne ilikuwa kawaida
na kwakweli miezi hiyo mafua ya hivi yalisambaa sana mpk nakumbuka serikali ikatoa tamko kuhusu haya mafua mana hali ilikuwa tete

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom