Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Inabidi nchi za kiafrica zifanye confirmation haraka kujua kama huu ugonjwa hautuathiri sisi ngozi nyeusi ili itumie hii fursa kuwapeleka vijana wetu wakapige kazi huko china na nchi zilizoathiriwa.
Inawezekana hii ndio fursa ya pekee iliyoletwa na Mungu ili kumkomboa mwafrica kutoka kwenye lindi la umaskini
tumefanana mawazo, kwamba ni muda sasa Afrika kuitawala dunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi saana... Corona kamua baba...usitumie hirizi population ya Dunia ipungue watu tumefika billions kadunia kenyewe kadogo.

We are overpopulated.... Please depopulates us friendly.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dunia ndogo Wakati flat Earthers wanasema baada ya ukuta wa barafu Antarctic kuna mabara 35 yanayo endelea kabla ya kufika kwenye kizuizi cha Dome ya kioo!
 
UPDATE: China

Mpaka sasa, China imekwisha ripoti visa vipatavyo 80,151 vya COVID-19 nchini humo huku wagonjwa wapatao 6,806 wakiripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi na wengine 47,204 wakiripotiwa kupata nafuu.

China imekwisha ripoti vifo vipatavyo 2,943 vilivyotokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo hadi hivi sasa.
Mbona update za china wanazotoa zimekaa kimapishi mapishi sana,,,,wachina wawe wakweli bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona update za china wanazotoa zimekaa kimapishi mapishi sana,,,,wachina wawe wakweli bhana

Sent using Jamii Forums mobile app

It seems wachina wameamua sasa kutaka watu wao warudi makazini, kwa hivyo data wanazotoa kila siku zinapungua ili baadae wawaaminishe watu wao kuwa hali shwari kumbe bado.

Nadhani wameshajiaminisha kuwa kila mtu keshajua namna ya kujikinga kwa hiyo hata wakirudi makazini infection rate itapungua.

Problem ya hii approach ni kwamba kuna watu wataanza kuwa reckless kwa kuamini hali iko shwari na hivyo kujiachia, matokeo yake maambukizi kutokoma anytime soon
 
Inabidi nchi za kiafrica zifanye confirmation haraka kujua kama huu ugonjwa hautuathiri sisi ngozi nyeusi ili itumie hii fursa kuwapeleka vijana wetu wakapige kazi huko china na nchi zilizoathiriwa.
Inawezekana hii ndio fursa ya pekee iliyoletwa na Mungu ili kumkomboa mwafrica kutoka kwenye lindi la umaskini
Nmecheka kama mazuri[emoji23] kufa kufaana
 
UPDATE: Uingereza

Visa vipya 10 vimeripotiwa nchini Uingereza na kufikisha jumla ya visa 51 huku wagonjwa wapatao nane (8) wakiripotiwa kupata nafuu.

Mpaka sasa, Uingereza haijaripoti kifo chochote kile kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
Kwakua ushafika kwamalkia nawaomba sana na nawashauri sana waakhirishe epl tulikua hatuombi ufike ila madam ushafika epl ife liva wakaetena bila kombe [emoji23][emoji16][emoji3][emoji12][emoji14]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia ndogo Wakati flat Earthers wanasema baada ya ukuta wa barafu Antarctic kuna mabara 35 yanayo endelea kabla ya kufika kwenye kizuizi cha Dome ya kioo!
Kwanza huko wala usifike huku huku tu kwakawaida kuna sehemu kubwa sana ambayo bina adam hajaigusa wala kuigusa katika makazi viwanda hata kilimo pia yaani nisehemu ipo tu imekaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Uswisi imeripoti visa vipya 22 nchini humo na kufikisha jumla ya visa 59 nchi nzima hadi hivi sasa.
 
UPDATE: India imeripoti visa vipya 22 nchini humo na kufikisha jumla ya visa 28 hadi sasa huku wagonjwa watatu (3) wakiripotiwa kupata nafuu.
 
UPDATE: Korea Kusini

Visa vipya 293 vimeripotiwa nchini humo hivyo kuongeza idadi ya visa vyote mpaka kufikia 5,621 nchi nzima hadi hivi sasa huku wagonjwa wapatao 34 wameripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo kutokana na COVID-19 nchini humo ni 33 hadi sasa.
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 37 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 240 nchi nzima ambapo wagonjwa wawili (2) wameripotiwa kuwa katika hali mbaya zaidi huku wengine 16 wakipata ahueni.

Hadi sasa, Ujerumani haijaripoti kifo chochote kitokanacho na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
NEWS ALERT: South Korea will use an app to monitor people who are quarantined over coronavirus and if they leave their designated location, the system will set off an alarm. [CNN]
 
UPDATE: Iraq imethibitisha kifo cha kwanza nchini humo kilichotokana na COVID-19 ambapo mpaka hivi sasa, visa vipatavyo 32 vimeripotiwa nchini humo.
 
UPDATE: Visa vipya vya COVID-19
  • Visa vipya viwili (2) vimeripotiwa nchini Australia na kufikisha jumla ya visa 41 nchini humo hadi sasa
  • Visa vipya viwili (2) vimeripotiwa Uskochi, Uingereza na kufikisha jumla ya visa 53 nchini humo hadi sasa
  • Visa vipya viwili (2) vimeripotiwa nchini Belarus na kufikisha jumla ya visa sita (6) nchini humo hadi sasa
  • Visa vipya viwili (2) vimeripotiwa nchini Iceland na kufikisha jumla ya visa 16 nchini humo hadi sasa
 
Back
Top Bottom