Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Australia hali si hali!

Coronavirus imefanya bidhaa madukani kugombaniwa mpaka watu kupigana ngumi. Imebidi jeshi la polisi liingilie kati.
 
NEWS ALERT: People in many parts of the world are being asked to avoid crowds, limit travel and even work from home to help limit the spread of novel coronavirus, and satellite images suggest they're heeding that advice. [CNN]
 
NEWS ALERT: The World Health Organization has called the spread of the virus "deeply concerning" as 94 nations and territories have now reported cases of the disease. [AFP]
 
UPDATE: Barani Afrika

Kisa cha pili cha COVID-19 kimeripotiwa nchini Afrika Kusini.

Pia, nchi nyingine ya Togo iliripoti kisa cha kwanza (1) nchini humo hapo jana.

Mpaka sasa, nchi tano (5) zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zimeripoti visa vya COVID-19.

Taarifa zaidi zitafuata.
 
ha ha ha mkuu umenichekesha eti naiwe hivyo usipatikane
dah ! sema tuombe hilo janga iwe kweli halimuathili black people mana km ni kusema joto nchi zenye joto zisharepotiwa tayari kuwa na maambukizi
hvyo tuombe uwe ugonjwa wa wanaojiweza hao weupe
we fikilia hongkong tu imegawa zaidi ya mln 1 na ushehe kwa kila mwananchi wake zakujikimu
wkt ITARY yeye katenga zaidi ya trilion 17 kupambana kuhakikisha wananchi wake wanabaki salama
wkt hapa bongodasilamu likitokea tetemeko tu yeye hajaleta tetemeko na pesa za rambirambi zinaliwa
sasa ikija hiyo COVID-19 maiti si zitagaa mtaani tu mana tutakimbiana

Sent using Jamii Forums mobile app

haha kwakweli hata WHO walisema heri corona iisgie huko kwao na si Afrika!!!
 
UPDATE: Ulimwenguni

Mpaka sasa, jumla ya visa 102,084 vimeripotiwa duniani huku idadi ya vifo ikifikia 3,491 ulimwenguni kote hadi hivi sasa kulingana na takwimu rasmi.

Wagonjwa wapatao 57,331 wameripotiwa kupata ahueni huku visa vya COVID-19 vikizidi kuongezeka zaidi.
 
Adjustments.JPG


United Kingdom



Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Iran

Visa vipya 1,076 sanjari na vifo vipya 21 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 5,823 huku wagonjwa wapatao 1,669 wakitajwa kupata ahueni.

Hadi sasa, watu wapatao 145 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Ubelgiji imeripoti visa vipya 60 na kufikisha jumla ya visa 169 nchi nzima huku wagonjwa wawili (2); mmoja akiwa mahututi na mwingine akiripotiwa kupata nafuu.
 
UPDATE: Uswisi imeripoti visa vipya 54 nchini humo na kufikisha jumla ya visa 264 nchi nzima ambapo wagonjwa wapatao watatu (3) wameripotiwa kupata ahueni huku mgonjwa mmoja (1) akiwa mahututi.
 
UPDATE: Uhispania

Visa vipya 98 pamoja na vifo vipya vitano (5) vimeripotiwa nchini Uhispania na kufikisha jumla ya visa 500 huku wagonjwa wapatao 11 wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 30 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia 10 hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 130 vimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 800 ambapo wagonjwa wapatao 17 wametajwa kupata ahueni huku wengine wawili (2) wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Hadi sasa, Ujerumani haijaripoti kifo chochote kile kinachohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini humo.
 
UPDATE: Ufaransa

Visa vipya 336 pamoja na vifo vipya saba (7) vimeripotiwa nchini Ufaransa na kufikisha jumla ya visa 949 huku wagonjwa wapatao 21 wakiwa katika hali mbaya zaidi na wengine 12 wakiripotiwa kupata nafuu.

Idadi ya vifo nchini humo vinavyohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) imefikia 16 hadi hivi sasa.
 
Back
Top Bottom