Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: COVID-19 Duniani

Hadi hivi sasa, idadi ya visa vilivyothibitishwa ulimwenguni kote imefikia 173,955. Kati ya hivyo, vifo ni 6,686.

Wagonjwa wapatao 77,520 wametibiwa na kupata ahueni huku visa vipatavyo 89,749 duniani, bado havijapatiwa ufumbuzi.

Hiyo ni kulingana na takwimu rasmi.
Fatality rate mbona kama ipo chini sana tofauti na panic ya watu mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli mkuu. Tumekumbwa kama na hofu tu flani kubwa sana kuliko uhalisia.
Yaani malaria licha ya kuwepo na tiba pamoja na njia za kujikinga lakini kwa mwaka inaua watu mpaka laki 5 ila tunaiona ya kawaida na hata hatukumbuki kulala na vyandarua,

Huu ugonjwa bado haujapatiwa dawa lakini ndani ya miezi 4+ fatality ni 7000 kasoro ila tunauogopa sana.

Sijui kwa sababu mkubwa kasema?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali ni mbaya sana kwa mashirika ya ndege duniani
Virgin Airlines wamewaomba wafanyakazi wachukue likizo ya miezi miwili bila malipo
BA wamepunguza sana usafiri
Norwagin nao hawako nyuma
Flight zote kwenda Italy wamesitisha
Watu wengi watakosa kazi kuanzia April na kuendelea
Hali ni mbaya Ulaya

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hali ni mbaya sana kwa mashirika ya ndege duniani
Virgin Airlines wamewaomba wafanyakazi wachukue likizo ya miezi minne bila malipo
BA wamepunguza sana usafiri
Norwagin nao hawako nyuma
Flight zote kwenda Italy wamesitisha
Watu wengi watakosa kazi kuanzia April na kuendelea
Hali ni mbaya Ulaya

Sent from my iPhone using Tapatalk
Kifuatacho ni economic depression.
 
UPDATE: Barani Afrika

Hadi sasa, visa vipatavyo 376 vimethibitishwa barani Afrika kwa ujumla.

Mataifa ya Afrika yapatayo 29 yameripoti visa vya COVID-19 katika nchi zao huku Misri ikiwa kinara kwa kuripoti visa vingi zaidi barani Afrika mpaka kufikia sasa.

Idadi ya visa vyote hadi sasa;
  1. Misri: Visa 126 vikiwemo vifo viwili (2). Wagonjwa 26 wamepata ahueni
  2. Afrika Kusini: Visa 62 hadi sasa
  3. Algeria: Visa 54 vikiwemo vifo viwili (2). Wagonjwa nane (8) wamepata ahueni
  4. Morocco: Visa 28 vikiwemo vifo viwili (2). Mgonjwa mmoja (1) pekee amepata ahueni
  5. Senegal: Visa 26. Mpaka sasa, wawili (2) wamepata ahueni
  6. Tunisia: Visa 16. Mgonjwa mmoja (1) amepata nafuu
  7. Burkina Faso: Visa 15 hadi sasa
  8. Ghana: Visa sita (6) hadi sasa
  9. Rwanda: Visa vitano (5) hadi sasa
  10. Ethiopia: Visa vitano (5) hadi sasa
  11. Cameroon: Visa vinne (4) hadi sasa
  12. Ivory Coast: Visa vinne (4) hadi sasa
  13. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC): Visa vitatu (3) hadi sasa
  14. Shelisheli: Visa vitatu (3) hadi sasa
  15. Kenya: Visa vitatu (3) hadi sasa
  16. Nigeria: Visa viwili (2). Mgonjwa mmoja (1) amepata ahueni
  17. Namibia: Visa viwili (2) hadi sasa
  18. Togo: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  19. Gabon: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  20. Guinea: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  21. Mauritania: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  22. Sudan: Kisa kimoja (1) hadi sasa ambacho pia ni kifo cha kwanza (1) nchini humo
  23. Eswatini/Swaziland: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  24. Guinea ya Ikweta: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  25. Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR): Kisa kimoja (1) hadi sasa
  26. Kongo: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  27. Liberia: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  28. Tanzania: Kisa kimoja (1) hadi sasa
  29. Somalia: Kisa kimoja (1) hadi sasa

Taarifa zaidi zitafuata!
 
Mkuu hawa wanaokata moto Africa je ni wazungu tu au mpk blacks?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Avoid anti-inflammatory drugs
France's Health Minister Olivier Veran said on Twitter on Saturday for pain relief it was better to take paracetamol because over-the-counter anti-inflammatory drugs may worsen the coronavirus.

"The taking of anti-inflammatories [ibuprofen, cortisone] could be a factor in aggravating the infection. In case of fever, take paracetamol. If you are already taking anti-inflammatory drugs, ask your doctor's advice," said Veran.

Patients should choose paracetamol, also known known in the United States by the generic name acetaminophen and commonly by the brand name Tylenol, because "it will reduce the fever without counter-attacking the inflammation", the health ministry added.

Anti-inflammatory drugs are known to be a risk for those with infectious illnesses because they tend to diminish the response of the body's immune system.

Source: Aljazeera
 
Kifuatacho ni economic depression.

Hii haina mjadala kabisa huku tumeanza kuiona zamani Mkuu kila kitu kinapanda, makampuni wanasema chukueni likizo ya dharura bila malipo
Yaani hali ni mbaya sana ila kwa Africa hali ni tofauti kabisa kwani wanajali siasa zaidi kuliko uhalisia
Angalia na uchaguzi utatafuna mabillion na miradi inaendelea kumaliza hela badala ya kuweka kwa ajili ya matukio Haya yanayoendelea duniani
Africa vitu vingi vinatoka nje na bei zitapanda mara 2 je wamejiandaaje zero

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Yaani malaria licha ya kuwepo na tiba pamoja na njia za kujikinga lakini kwa mwaka inaua watu mpaka laki 5 ila tunaiona ya kawaida na hata hatukumbuki kulala na vyandarua,

Huu ugonjwa bado haujapatiwa dawa lakini ndani ya miezi 4+ fatality ni 7000 kasoro ila tunauogopa sana.

Sijui kwa sababu mkubwa kasema?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ni kuwa spreading yake ni very fast
 
Hakika Akili ni nywele kila mtu ana zake!
Wakati dunia inahangaika na kutapatapa kujinasua na Corona!

Zipo tuhuma kwamba virusi hivi vilitengenezwa na watu ili kukidhi haja zao!
Wakati dunia inahangaika kutafuta tiba kumbe kuna kamati ya roho mbaya inatapanya ugonjwa usambae dunia nzima!
Watu wanalipwa madola kuuvusha ugonjwa huu mataifa ya mbali, watu wanapakaza na kuambukiza wenzao kwa makusudi kutimiza lengo n.k

Kiufupi Adui wa mtu ni mtu

Hapo ndipo zao la Donor fund project linapoibua FAIDA kwa mataifa!

Pamoja na kilio cha mataifa changa kutokuwa na pesa kupambana na ugonjwa huu wa Corona!

Lakini tukumbuke kwamba Mvua njoo katarina njoo!

Watu kupitia ugonjwa huu watapiga pesa ndefu!

Hadi Corona itakapoisha kuna watu watakuwa wametajirika ajabu!

Inauma sana kwa upande mwingine!

Nimetafta mtoto wa kiume kwa miaka kumi na tano paspo mafanikio!; hatimae nimebahatika mwaka huu inauma sana kusikia kuna CORONA !

......BINADAM WABAYA SANA....
Doto mkali umerudi makambako sasa!?
 
Back
Top Bottom