Fahamu kuhusu bakteria wa H.Pylori; Athari na tiba yake

Fahamu kuhusu bakteria wa H.Pylori; Athari na tiba yake

Hapa JF kila mtu ni mtaalamu makushauri uende hospital
 
Kuna dawa inaitwa kit for hyperol, nadhani hapo ndio suruhisho lilipo japo ni gharama kidogo
 
osama BLD said:
Mkuu meza saws Heligo for seven days alafu inauzwa kuqnzia alf40 hadi 50 kisha siku ya 8 kuna nyingine unaendela nay kwa cku 23 jina sikumbuki vizur ila nadhan inaitwa tendazole sina uhakika nilivyo itajq
Mkuu nshafanya hivyo, nasubr mda kidogo nikapime tena
 
Mkuu meza saws Heligo for seven days alafu inauzwa kuqnzia alf40 hadi 50 kisha siku ya 8 kuna nyingine unaendela nay kwa cku 23 jina sikumbuki vizur ila nadhan inaitwa tendazole sina uhakika nilivyo itajq
Una nia nzuri uko sahihi ni dose nzuri, hiyo ya siku 23 unameza kidongo kimoja ndani ya 24hrs mimi pia nimeisahau ila inakuwa packed together kwenye Heligo kit!
 
Una nia nzuri uko sahihi ni dose nzuri, hiyo ya siku 23 unameza kidongo kimoja ndani ya 24hrs mimi pia nimeisahau ila inakuwa packed together kwenye Heligo kit!
umepona
 
jitahidi mkuu usije ukaingia kwenye friji nenda kapime kama huamini hayo matibabu niliyokupa
 
Wakuu habari za muda,

Nimeanza kuumwa hili tatizo tangu mwaka jana mwezi wa nane. Nimetumia heligo kit mara mbili, na dawa moja moja mara moja ambazo sio kit. Nikaenda tena kupima na endoscopy ile unaingizwa mpira tumboni, nikakutwa sina vidonda ila bacteria bado wapo. Kikubwa kinachonisumbua ni kuwa na kiungulia kikali, kifua kinawaka moto. Naombeni msaada wa mawazo.

Pia kuna dawa nasikia anauza yule dada Natasha wa bongo movie, mwenye info zake anaweza kunisaidia, nimesikia ni dawa nzuri.

Naombeni msaada wa mawazo na kimatibabu
 
Nilikuwa natatizo hilo kwa mwaka miaka miwili lakini nimekuja kupona kabisa. Nipo job now nikifika home nitakutumia dawa nilizo tumia. Naamini utapona.
 
Nilikuwa natatizo hilo kwa mwaka miaka miwili lakini nimekuja kupona kabisa. Nipo job now nikifika home nitakutumia dawa nilizo tumia. Naamini utapona.
Mkuu asante sana. Nakupm namba yangu. Ntashukuru sana.
 
Sasa wakuu mngeweka hapa hizo info ili na wengine pia wapate msaada ndo maana nzima ya jamiiforum.. Mkipeana taarifa kimya kimya sio poa.. Nawasihi na kuwaomba kiungwana tu muweke ufumbuzi wa hilo tatizo hapa ili na wengine wapone...
Usijali, hapa tunaelimishana, kila kitu kitawekwa wazi
 
Kwanza kabisa nianze kwa kuwafahamisha vile nilivyokuwa nasumbuliwa, lakini pia nikili kuwa Mimi si mtaalamu wa masuala hayo. Kwanza tatizo lilianza nikiwa chuo kikuu mwaka wa pili, dalili nilizokuwa nazo ni kiungulia kikali katikati ya tumbo na kifua(kwenye chembe ya moyo) hasa nikiwa na njaa na baada ya kula baadhi ya vyakula kama dagaa, maharage, nikinywa soda, nikila mboga ya majani iliyoungwa nyanya nyingi, nikila matunda yenye kamba kamba kama chungwa na embe ila nilikuwa nahisi maumivu kupungua nikila parachichi. Lakini pia maumivu makali nilikuwa nikiyapata na kupata choo cheusi endapo tu nitakila pilau. Shida nyingine ilikuwa nikiwa na stress kidogo tu, maumivu niliyokuwa nikiyapata ni makali sana.

Hatua nilizochukua ilikuwa ni kwenda kupima hospital na madaktari wakaniambia ninavidonda vya tumbo wakanipa dawa ambazo sizikumbuki kwa sasa ila hazikunisaidia chochote ila baadae nikamshirikisha ndugu yangu ndipo akaniambia nijaribu dawa inayoitwa Omeprazole. Nikainunua lakini kiukweli dawa hii ikawa inatuliza tu maumivu lakini baadae yakawa yanarudia.

Nimeendelea kutumia dawa hiyo toka nikiwa chuo mwaka wa tatu hadi 2015 ni takribani miaka miwili. Sikumoja ambayo sitaisahau niliingia pharmacy kununua dawa zangu kama nilivyozoea ndipo nikamkuta muhudumu(mtu wa makamo) na ninadhani atakuwa mstaafu katika idara ya afya, nikamwambia nahitaji omeprazole, akaniuliza unavidonda vya tumbo? bila kupoteza muda nikamjibu ndio! akaniambia kwa hiyo dawa utakuwa unatuliza maumivu tu, nikamuuliza kwahiyo unanishaurije? Akaniambia nitakupa dozi ifuatayo ukaitumie, usipoona mabadiliko rudi nikupe dozi nyingine ila gharama yake ni 35 elfu. Ndipo akaniandikia dozi ifuatayo:
- Amoxillin caps 2×3,
- Metroprozole Rx 2×3, na
- Omeprazole 1×2.

Nakumbuka nilikunywa kuanzia tarehe 13 hadi 17/6/ 2015. Toka siku hiyo nilipo maliza kunywa hiyo dozi hadi leo hii. Nipo vizuri na vyakula vyote nilivyokuwa nikitumia napatwa na maumivu navitumia vizuri tu na sihisi maumivu tena na hata dozi ya pili aliyoniambia nikachukue nisipoona mabadiliko sikurudi. Kwahiyo nilipona kwa 8500Tsh. Hivyo ndivyo nilivyopona. Nimejaribu kueleza kwa kirefu ili mnielewe kwasababu yawezekana dalili zinatofautiana.

Ahsanteni na samahani kama maelezo yangu hayatakusaidia.
 
Back
Top Bottom