Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli mi pia ninatatizo hilo aseeSasa wakuu mngeweka hapa hizo info ili na wengine pia wapate msaada ndo maana nzima ya jamiiforum.. Mkipeana taarifa kimya kimya sio poa.. Nawasihi na kuwaomba kiungwana tu muweke ufumbuzi wa hilo tatizo hapa ili na wengine wapone...
Mkuu umeshawahi kutumia, na ikabaki historiaNenda duka la dawa tafuta dawa inaitwa heligo kit tumia then ikiisha endelea na omeprrazole kwa siku 21...tatzo lako litabak kua historia ndugu
Hiyo ni full dose kwa helicobacter pylori...usiwe na waswas rumia kama nilivyokuelekeza ..Mkuu umeshawahi kutumia, na ikabaki historia
Nishawahi kutumia, ndio maana nakuuliza hivyo. Je kuna masharti wakati unatumia, unaweza kunielezaHiyo ni full dose kwa helicobacter pylori...usiwe na waswas rumia kama nilivyokuelekeza ..
Kweli kabisa!Na si kuumwa tu chembe ya moyo na tumbo unaweza hata kujifikiria una ukimwi maana dalili zake ni nyingi vidonda mdomoni maumivu ya mwili hata unaweza kufikiri ni typhoid au malaria mgongo na kiuno kuuma miguu uchomvu mwilini kichwa kuuma miguu kuwanga nk
Je kifua kilikuwa kinawaka moto au ni dalili tofauti na hizoNilienda hospital ya Regency wakanipa heligo kit na dawa nyingine mbili mwaka jana nikazitumia ipasavyo mpaka tembe ya mwisho. Mpaka sasa sijaumwa tena na nilienda kupima tena sikukuta huo ugonjwa.
Dalili ninazo, na nimefanya endoscopy sina vidonda ila bacteria ninao, je hapo suluhisho ni lipiH. Pylori ndio ansababisha vidonda mpaka upate dalili hizo ni tayari una vidonda hivyo basi nenda wakufanyie endoscopy kubaini hivyo vidonda, huyo bakteria mara nyingi ana tabia ya kurudi ukitumia dawa anaisha baada ya muda anarudi, prof mmoja aliniambia kati ya watu 10, nane wanao huyo kitu na hadi daliki zijitokeze umeshaishi nae si chini ya miaka 10 huwa anamwaga acid kwenye utumbo ambayo husababisha vidonda na kukausha yale majimaji yayofanya choo kiwe laini matokeo yake kupata choo kigumu
amoxillin kutwa mara ngapi, na kila kipindi ngapiTumia kwanza helicokit kwa wk 2 hadi 3 wakati unatumia hiyo tumia na amoxicillin 2 bd kwa siku 14 utanipa majibu
Heligo kit ina dawa tatu, mbili zikiwa ni antibiotics yaani Clarithromycin na Tinidazole na ya tatu ni ile yakupunguza tindikali(proton pump inhibitor) Lansoprazole. Dose ni vidonge 3 kila baada ya masaa 12 (mara mbili kwa siku) kwa siku 7, jumla ni vidonge 42. Baada ya hapo utaendelea na Lansoprazole pekee kwa wiki 4.Kuna dawa aina tatu katika kutibu vidonda vya Tumbo
Antibiotic hii ni ya kuua bakteria hpylori
Dawa ya pili ni ile ya kupunguza tindikali
Na dawa ya tatu ni ile ya kutengeneza ute ndani ya kuta za tumbo
Wakati unatumia heligo kit unashauriwa usitumie tena dawa nyingine ya antibiotic zaidi ya kutumia dawa za kupunguza tindikali Omeprazole au jamii ya dawa za kupunguza tindikali
Kwa wale wanaotaka kujalibu kutumia dozi ya heligo kit tafadhari someni kwanza maelezo yake..