Fahamu kuhusu bakteria wa H.Pylori; Athari na tiba yake

Fahamu kuhusu bakteria wa H.Pylori; Athari na tiba yake

Agakhan dar walinipa heligokit na amoxicillin pia na rabeprazole nikatumia zote kwa pamoja nilipata nafuu sana ni kama nilipona maaana nilivyopima huyo bakteria hakuonekana ni miaka 5 iliyopita ila mwaka huu mwezi wa tatu nilianza kuumwa tena nikaenda regency nikapima choo akaonekana tena hapa nipo kwenye kit tena lakini niliongezewa na rabeprazole natumia kwa pamoja,

Ndugu nikujibu hiyo dawa ni metronidazole siyo kama unavyoandika lakini ipo ndani hiyo kit imetumia jina la tinidazole, pia dr's wanaweza kujua ugonjwa kwa kujua dalili hivyo kukuuliza na kukuandikia dawa ni sahihi kabisa pia kupima endoscopy ni kujua ukubwa wa vidonda na utumbo unahali gani kuna vidonda ambavyo chanjo siyo huyo helicobacteria ili ujue chanzo ni huyo unapima damu na choo kikubwa.

akiwepo ndio kutumia hizo kit kama hayupo unatumia hizo omeprazole au rabeprazole au esomeprazole lansoprazole lakini zilizo za karibuni ni hiyo rabe na eso kuna rafiki yangu alienda kutibiwa hilo tatizo South Africa ameniambia hana huyo bacteria kapewa esomeprazole na Domperidone hii walimwambia vidonda husababisha kichefuchefu au hata kusikia kutapika hali hiyo hufanya acid kuzalishwa kwa wingi zaidi hiyo dawa inazuia kichefuchefu na kutapika
 
Ivi boss kuna ugonjwa ambao wewe huna dawa yake
Hakuna Maradhi ambayo yasiyo kuwa na dawa yake. Kila Maradhi yana dawa yake. Ninatibu karibu maradhi yote unayo yajuwa wewe.

ALKALINE FOODS.jpg
 
Wakuu heshima zenu,

Mara ya kwanza nilipima choo nikaambiwa nina hpylori ila sina vidonda vya tumbo, mara ya pili nikapima choo na pia endoscopy ya kuingiziwa mpira wenye kamera tumboni. Nikakutwa tena na hpylori, ila picha zikatoka nikaambiwa sina vidonda vya tumbo.

Tatizo kubwa nililo nalo ni tumbo na kifua kuwaka moto, je hii inasababishwa na nini iwapo sina vidonda vya tumbo

Msaada wenu niweze kufahamu vizuri

Nawasilisha
 
Pole sana ndugu,

Inawezekana kabisa kuwa na h pylori bila kuwa na vidonda vya tumbo. Hawa ni bacteria walio common sana kwenye mazingira yetu. Inakadiriwa asilimia 60 ya watu wana hawa bacteria kwenye matumbo yao, lakini si lazima upate vidonda unapokuwa nao japo ni moja ya factor muhimu zinazopelekea vidonda vya tumbo (ulcers).

Kupata kiungulia maana yake unatengeneza acid nyingi tumboni ambayo inarudi nyumba (reflux) na kuunguza sehemu ya juu ya njia ya chakula yaani umio (oesophagus) na kukusababishia maumivu unayoyasikia (heartburn). Uzalishwaji wa acid nyingi waweza kusababishwa na vyakula vyenye viungo vingi (spicy foods), citric, mkazo (stress), kuvuta sigara, baadhi ya dawa - hasa zilizo katika kundi la NSAIDs kama aspirin na ibuprofen - nk.

Kupunguza au kuepuka vitu hivi itakukinga na kiungulia lakini pia kuna dawa (antiaacids) ambazo zinaweza kupunguza utengenezaji wa acid uliopitiliza na hivyo kukuponya na kiungulia.

Acid kuweza hurudi nyuma kama una tatizo linaitwa hiatal hernia, ambayo husababisha tumbo kupanda juu na kupelekea acid kuingia katika umio (oesophagus) na kusababisha maumivu. Au ile sphincter inayotenganisha tumbo na umio ikiwa imelegea, acid yaweza ingia pia kwenye umio.

Unaweza kuwa na inflammation (kama mikwaruzo fulani) na sio vidonda (ulcers) na ukapata maumivu ya chembe ya moyo pia.

Si vibaya pia ukatibu hao H pylori kwani kwa hali yako wanaweza kukuletea vidonda baadae.
 
kapotolo,
Mkuu hpylori nimepima, ila sijarudi tena kucheki baada ya matibabu, pia huo ugonjwa wa hiatal hernia unapimwaje,.Kingine sina stress, wala situmii hivyo vyakula. Na kama ni mikwaruzo tu tumboni nitumie dawa gani kuponya ikiwa kiungulia hakiishi, ila sina vidonda vya tumbo. Au hpylori wanasababisha kiungulia. Naomba mawazo yako
 
Mwaka jana kifua kilinisumbua sana hasa kuwaka moto, baada ya kupima nilikuwa na Typhoid. Baada ya kutumia dozi hali ilikuwa shwari hadi leo hii
Dozi gani kama unaikumbuka ili nijaribu na doctari wangu
 
Angalia aina ya vyakula unavyokula... Huenda unakula maharage yaliyoungua na vitu kama hivyo.
DAWA.
Chukua majivu ya jiko la mkaa vijiko viwili, koroga kwenye maji safi kisha kunywa. Fanya hivi kila mara usikiapo kiungulia.
 
Angalia aina ya vyakula unavyokula... Huenda unakula maharage yaliyoungua na vitu kama hivyo.
DAWA.
Chukua majivu ya jiko la mkaa vijiko viwili, koroga kwenye maji safi kisha kunywa. Fanya hivi kila mara usikiapo kiungulia.
Asante sana, nitajaribu na hii pale nipatapomuda nikiwa karibu na majivu
 
Sasa umeomba ushauri unashauriwa unasema uyaomba ushauri kwa daktari wako , dawa naijua vizuri sana tena haizidi sh mia 2, mimi nimeteseka sana na nimepona kwa mia 2
 
Sasa umeomba ushauri unashauriwa unasema uyaomba ushauri kwa daktari wako , dawa naijua vizuri sana tena haizidi sh mia 2, mimi nimeteseka sana na nimepona kwa mia 2
Hapana, nimetumia madawa mengi ya heligo kit kutibu hpylori, kumbuka nima antbiotics ambayo mtu hushauriwi kutumia mara kwa mara, ndio maana nikasema hivyo
 
Back
Top Bottom