Kwanza kabisa nianze kwa kuwafahamisha vile nilivyokuwa nasumbuliwa, lakini pia nikili kuwa Mimi si mtaalamu wa masuala hayo. Kwanza tatizo lilianza nikiwa chuo kikuu mwaka wa pili, dalili nilizokuwa nazo ni kiungulia kikali katikati ya tumbo na kifua(kwenye chembe ya moyo) hasa nikiwa na njaa na baada ya kula baadhi ya vyakula kama dagaa, maharage, nikinywa soda, nikila mboga ya majani iliyoungwa nyanya nyingi, nikila matunda yenye kamba kamba kama chungwa na embe ila nilikuwa nahisi maumivu kupungua nikila parachichi. Lakini pia maumivu makali nilikuwa nikiyapata na kupata choo cheusi endapo tu nitakila pilau. Shida nyingine ilikuwa nikiwa na stress kidogo tu, maumivu niliyokuwa nikiyapata ni makali sana.
Hatua nilizochukua ilikuwa ni kwenda kupima hospital na madaktari wakaniambia ninavidonda vya tumbo wakanipa dawa ambazo sizikumbuki kwa sasa ila hazikunisaidia chochote ila baadae nikamshirikisha ndugu yangu ndipo akaniambia nijaribu dawa inayoitwa Omeprazole. Nikainunua lakini kiukweli dawa hii ikawa inatuliza tu maumivu lakini baadae yakawa yanarudia.
Nimeendelea kutumia dawa hiyo toka nikiwa chuo mwaka wa tatu hadi 2015 ni takribani miaka miwili. Sikumoja ambayo sitaisahau niliingia pharmacy kununua dawa zangu kama nilivyozoea ndipo nikamkuta muhudumu(mtu wa makamo) na ninadhani atakuwa mstaafu katika idara ya afya, nikamwambia nahitaji omeprazole, akaniuliza unavidonda vya tumbo? bila kupoteza muda nikamjibu ndio! akaniambia kwa hiyo dawa utakuwa unatuliza maumivu tu, nikamuuliza kwahiyo unanishaurije? Akaniambia nitakupa dozi ifuatayo ukaitumie, usipoona mabadiliko rudi nikupe dozi nyingine ila gharama yake ni 35 elfu. Ndipo akaniandikia dozi ifuatayo:
- Amoxillin caps 2×3,
- Metroprozole Rx 2×3, na
- Omeprazole 1×2.
Nakumbuka nilikunywa kuanzia tarehe 13 hadi 17/6/ 2015. Toka siku hiyo nilipo maliza kunywa hiyo dozi hadi leo hii. Nipo vizuri na vyakula vyote nilivyokuwa nikitumia napatwa na maumivu navitumia vizuri tu na sihisi maumivu tena na hata dozi ya pili aliyoniambia nikachukue nisipoona mabadiliko sikurudi. Kwahiyo nilipona kwa 8500Tsh. Hivyo ndivyo nilivyopona. Nimejaribu kueleza kwa kirefu ili mnielewe kwasababu yawezekana dalili zinatofautiana.
Ahsanteni na samahani kama maelezo yangu hayatakusaidia.