Fahamu kuhusu bakteria wa H.Pylori; Athari na tiba yake

Fahamu kuhusu bakteria wa H.Pylori; Athari na tiba yake

Pole sana ndugu,

Inawezekana kabisa kuwa na h pylori bila kuwa na vidonda vya tumbo. Hawa ni bacteria walio common sana kwenye mazingira yetu. Inakadiriwa asilimia 60 ya watu wana hawa bacteria kwenye matumbo yao, lakini si lazima upate vidonda unapokuwa nao japo ni moja ya factor muhimu zinazopelekea vidonda vya tumbo (ulcers).

Kupata kiungulia maana yake unatengeneza acid nyingi tumboni ambayo inarudi nyumba (reflux) na kuunguza sehemu ya juu ya njia ya chakula yaani umio (oesophagus) na kukusababishia maumivu unayoyasikia (heartburn). Uzalishwaji wa acid nyingi waweza kusababishwa na vyakula vyenye viungo vingi (spicy foods), citric, mkazo (stress), kuvuta sigara, baadhi ya dawa - hasa zilizo katika kundi la NSAIDs kama aspirin na ibuprofen - nk...
Hii acid reflux ndo GERD? je inatibika?? Isipotibiwa na kupona madhara yake huwa ni nini?
 
Dah mimi nina hili tatzo, lilianza mda nimeshapima hiyo OGD, nikaambiwa nina GERD nikapewa mavidonge baada ya kumaliza dozi tatizo likarudi upya, nikapimwa mwez wa 6 nikaambiwa nina hao bacteria H.P nikatumia dawa lakn had wakati huu naandika moto unawaka tumbon had kifuani nikikaa sana joto linajitokeza hadi nje ya mwil ingawa nikipima na kipima joto, nakuta joto liko nomo, sasa sijui hata nifanyeje ila nateseka si mchezo
Tatizo bado unalo?
 
Hapa kuna kitu kinaitwa kansa ya tumbo ndo kinafananishwa na vidonda vya tumbo
 
Jamani maumivu ninayo yapata nimakali sana,miguu,kifua,mgongo,na miguu kuwaka moto na viungo vyote vinauma ,tar 3/11/2018 nlienda regency nkaonekana vidonda vya tumbo na bacteria H pylori,
 
Kuna jamaa nilimpa tiba asili alikuwa na vidonda tumbo yaani akienda Choo ni damu vilikula sana utumbo , amepona na anagonga kila kitu ni miaka inapita yupo namwona
Jamani maumivu ninayo yapata nimakali sana,miguu,kifua,mgongo,na miguu kuwaka moto na viungo vyote vinauma ,tar 3/11/2018 nlienda regency nkaonekana vidonda vya tumbo na bacteria H pylori,
 
Mama yangu aliugua H pyori ameshatumia clarithromycin, tinidazole, na omeprazole lakini tatizo halikwisha akapewa heligo kit lakini bado anaumwa.

Naombeni msaada wenu kwa anayefahamu matibabu mengine.
 
Habari zenu WAKUU poleni na janga la covid 19.

Aisee niende moja kwa moja kwenye mada. Nilikuwa na shida ya kupumua,viungo kuuma na kufa ganzi,moyo kwenda mbio na kuuma kwenye chemba ya kifua ,kichwa kuuma, tumbo kuuma, kuharisha, mara mgongo, pia masikio kutosikia vizuri na macho kutoona vizuri, kuhisi kizunguzungu na mwili hauna nguvu, kupata kiunguulia Mara kwa mara, Koo kuhisi Kama umebeba kitu hivi Ila ukimeza unameza vizuri, kuhisi baridi na homa,pia kipanda uso. Kupungua uzito kwa Kasi nilikuwa na uzito 77 saivi Nina 73.

Nikaenda hospitali aisee nilijua tayari corona,kwenda kupima nikakutwa na huyo bakteria aisee imesoma +.nikapewa dozi karibia zote antibiotics sijui heligo kit kila aina yaani nimetumia lakini wapi maumivu yanapungua halafu anarudi tena.

Sasa WAKUU hivi huyu mdudu ANAONDOKAJE aisee.maana nimekata tamaa kabisa kuna dawa niliambiwa ya tiba asili inaitwa netragen Ina uwezo wa kumuondoa huyu bado sijajua Kama Ni kweli inafanya kazi.

Ambao mlipatwa na hii kitu mliponaje aisee mtujuze maana hili gonjwa nooma unaweza kujihisi una ukimwi au corona.

Tusaidiane WAKUU tafadhali naamini madokta mpo humu.asanteni

NB: Sio kila dalili Ni korona, hili la bakteria Ni janga lingine,tena kubwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom