Habari zenu WAKUU poleni na janga la covid 19.
Aisee niende moja kwa moja kwenye mada. Nilikuwa na shida ya kupumua,viungo kuuma na kufa ganzi,moyo kwenda mbio na kuuma kwenye chemba ya kifua ,kichwa kuuma, tumbo kuuma, kuharisha, mara mgongo, pia masikio kutosikia vizuri na macho kutoona vizuri, kuhisi kizunguzungu na mwili hauna nguvu, kupata kiunguulia Mara kwa mara, Koo kuhisi Kama umebeba kitu hivi Ila ukimeza unameza vizuri, kuhisi baridi na homa,pia kipanda uso. Kupungua uzito kwa Kasi nilikuwa na uzito 77 saivi Nina 73.
Nikaenda hospitali aisee nilijua tayari corona,kwenda kupima nikakutwa na huyo bakteria aisee imesoma +.nikapewa dozi karibia zote antibiotics sijui heligo kit kila aina yaani nimetumia lakini wapi maumivu yanapungua halafu anarudi tena.
Sasa WAKUU hivi huyu mdudu ANAONDOKAJE aisee.maana nimekata tamaa kabisa kuna dawa niliambiwa ya tiba asili inaitwa netragen Ina uwezo wa kumuondoa huyu bado sijajua Kama Ni kweli inafanya kazi.
Ambao mlipatwa na hii kitu mliponaje aisee mtujuze maana hili gonjwa nooma unaweza kujihisi una ukimwi au corona.
Tusaidiane WAKUU tafadhali naamini madokta mpo humu.asanteni
NB: Sio kila dalili Ni korona, hili la bakteria Ni janga lingine,tena kubwa tu.
Sent using
Jamii Forums mobile app