Asikwambie mtu biashara ni usimamizi ata umweke ndugu yako kama hauna mda Wa kusimamia ni bora hiyo hela uiweke vinginevyo itateketea yooote.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli yule msimamzi sidhani kama ataumia na pesa ya msingi
Wala pango! Dada angepata likizo akae kwenye biashara aangalie upepo unapoelekea ndipo amkabidhi mtu
Unless otherwise ampe hesabu atakayofuata jioni kama kwenye chips.
Dada samahani,
Ulishawahi kufanya biashara huko nyuma?
Waliokuelekeza hapo wapo sahihi!
You are the owner of your ideas.
Hongera kwa kufikiria kuanzidha biashara ya chakula ambayo ndio biashara inayolipa kwa wakatu huu kwani lazima ule kwa njia yoyote. ili uipatie hii biashara ziangatia ushauri ufuatao.
1. Mpishi. Lazima uwe na mpishi ambaye atapika vyakula vikuu kutoka na na sehemu husika na vyenye ladha ambayo hata mtu akiwa tegeta asijisikie vibaya kuja bunju kula plate ya ubwabwa kwa dada naniliu.
2.Viungo. Matumizi sahihi ya viungo na kwa mapishi gani? nilishaona sehemu wametia binzari ya mchuzi kwenye chai wakidhani tea masala. usipike chai ya rangi ukatia maji na majani hamna hata karafuu, maganda ya iliki, mdalasini wala mchaichai.
3.Usafi. Usafi wa mpishi, sehemu unayofanyia biashara, vyombo vya kupikia na vyombo vya kulia vyakula chakula. sio vyombo vichafu vinasuuzwa baada ya kuoshwa na kufanya rangi ya sahani imebadilika na unaweza ukajiongeza kwa kuvizuuza na maji ya uvuguvugu kuuwa bakteria.
4. Bei. kwa kuwa unaanza hakikisha bei zako ni rafiki pamoja na kuwa ladha ya chakula chako ni tofauti na banda la mama lishe.
5.Vitendea kazi. Lazima uwe na vitende akazi tofauti kama blenda, microwave, jiko la gesi dogo na mtungi wake, sio mteja anataka chakula anapata chakula cha baridi japo kuwa amekujamida ambayo sio ya kibiashara kivile.
6. Mahitaji. Hakikisha unakwenda kwenye masoko makuu kwa mahitaji na epukakununua mahitaji mengi sana kwa wakati mmoja kama samaki na kuku unawaweka kwnye friza mwezi mzima kwani huwa wana tabia ya kuwa na kaharufu ambacho hakikati hata umuunge vp. usinunue mchicha jumapili uje kupika ijumaa hapana, Jitahidi japo mara mbili kwa week sio mbaya uwe unakwenda mwenyewe marikiti.
6. Jiongeze. Usiuze chakula kikuu tu kama wali pilau, la ongeza najuice za viwandani na za kutengeneza mwenyewe matunda mengi ni kupata ujuzi tu, tengeneza salad baada ya kachumbari kwa kulia chakula, tengeneza pilipili za kupikana sio mteja atake pilipili umpe nzima akate mwenyewe, kwani kuna vitu vidogo vinavutia wateja sana na kama sio mjuzo sana ingia hata you tube utaona mapishi ya tofauti.
Kama kuna la ziada njoo pm nitakupa maujuzi zaidi.
KwanI na huo pia c ni ushauri
Sijaona kama kuna yeyote aliyeshauri uache kazi.
Kuna kitu wanasema learning on the fly, fungua hiyo biashara, mwache huyo unayemwamini asimamie, utajifunzia hapo.
Mimi naungana na wewe, kama una mtu una mwamini mpe asimamie, biashara itaenda vizuri sana na baada ya muda atakuachia biashara yako ataanzisha yake pale pembeni achukue na wateja wake. Muhimu ni yeye kupata mtaji tu.
Ushauri mzuri huu. Hope atazingatiaMwanzo mzuri mkuu...
Angalia tu binafsi kero zangu tu nikupe huenda ukazifanyia kazi.
Napenda chakuka kitamu, hasa wali hakikisha unatafta mchele mzuri na wenye ladha.
Uharaka wa huduma huwa sipendi nimefika then sisikilizwi, wahudumu wawe shapu,
Mambo ya mtu umeagiza supu then chapati za kusubili hiyo wengi hatupendi aisee.
Tafta na friji weka juisi, soda na maziwa mtindi kama kuna wapenzi nayo kama mimi.
Staha epuka maneno yanatayokushushia heshima, but tarajia maneno ya kukera kutoka kwa wateja.
Sent from my Nokia 6 using Jamii Forums mobile app
Nilipata watu sahihi kabisa, wapishi wazuri na sikukurupuka, hata huyo shangazi yangu ndie mpishi mkuu, na alikuwa na mghahawa wake mdogo akapata matatizo na kufilisika hivyo hii biashara anaijua vizuri sana, nilitengeneza mfumo mzuri sana wa kuiendesha biashara yangu, na bado ninaifanya huku ninaendelea na shughuli zangu japo eneo nimehama baada ya chuo kuacha kupokea wanafunzi
Nakukumbusha tuu, binadamu kiasili ni wabinafsi - unalowaza wewe na yeye yanaweza kuwa sawa au tofauti who knows.
Weka mkakati makini wa kuisimamia biashara yako, na kufanya baadhi ya shughuli mwenyewe, mimi nikiwa hapa mjini jumamosi asubuhi ninaingia mwenyewe sokoni na supplier wangu ni wale wale.
Sent using Jamii Forums mobile app
huu ni ukweli mchungu ambao wengi hatuupendi kuambiwa.
Dunia nzima hakuna mtu anaependa kumfanyia mwenzake kazi ya kumtafutia hela..
Huyo dada atakuibia tu. hata awe muaminifu vipi
Biashara inayoweza kukulipa vizuri ni ile unayoifanya wewe mwenyewe.
Jamani kashauriwa saana kashasema anamwamini mwacheni Mimi binafsi nakuunga mkono asilimia elf kumi nilifanya biashara 3 zote niliangukia pua kisa kuachia watu yaani sasa hivi nakaba mpaka mia
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa asiejua hesabu la sahani ni nani? A very light point. Usijali sivunjiki moyo kirahisi mpaka sasa sijaona point ya kunivunja moyo
Mbona mwenye point katulia? Nkiomba ushauri ndo nikae kimya nisijibu?
Njoo uniombee dadaangu
Ukimwachia tu ushafeliNtamwachia ntapitia hesabu coz mda mwingi ntakua kibaruani
Ukifika mbali sana utafunga baada ya mwaka ila sana sana ni miezi sita tu.Ntamwachia ntapitia hesabu coz mda mwingi ntakua kibaruani
Huu ndio ukweli mchungu. Nafanya hii biashara kupitia mke wangu ni ndoto yetu plus yeye ni fundi wa kupika ila kwenye ofisi ni msimamizi coz hauwezi simamia kitu usichojua.Itakushinda kama utaanza hiv dada angu,nikwambie ukwel tuu...
Sabab management ndo kila kitu,huyo msichana si maono yake hyo biashara so yeye anafanya tuu alipwe..wew ndie mwenye maono kwamba unataka chakula kiwe hiv,quality i mean..usaf,hospitality,uwepo uvumiliv,acountability etc .so huyo dada hatowez,
Atauza wik 1 ataona hamna wateja atavunjika moyo ataanza lipua kaz na ndo mwanzo wa kuharibika..sabab trend ya biashara yoyote.enewea,graph huanza kidogo then hushuka kwa kas ya ajab,badaee ndo huanza kupanda,je huyo unaemwachia ataweza haya yote
Sent using Jamii Forums mobile app