Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Ni kweli yule msimamzi sidhani kama ataumia na pesa ya msingi
Wala pango! Dada angepata likizo akae kwenye biashara aangalie upepo unapoelekea ndipo amkabidhi mtu
Unless otherwise ampe hesabu atakayofuata jioni kama kwenye chips.

Kuangalia mapato ya awali ni muhimu si ntayaona wakiwa wanauza cha msingi hutakiwi kukata tamaa.
 
Dada samahani,
Ulishawahi kufanya biashara huko nyuma?
Waliokuelekeza hapo wapo sahihi!
You are the owner of your ideas.

Sijawahi ila nna idea nayo najua vitu muhimu vya kuzingatia but huyo dada ana utaalamu. Mimi sioni ndani, kama sio yeye hamna biashara hapo.
 
Hongera kwa kufikiria kuanzidha biashara ya chakula ambayo ndio biashara inayolipa kwa wakatu huu kwani lazima ule kwa njia yoyote. ili uipatie hii biashara ziangatia ushauri ufuatao.

1. Mpishi. Lazima uwe na mpishi ambaye atapika vyakula vikuu kutoka na na sehemu husika na vyenye ladha ambayo hata mtu akiwa tegeta asijisikie vibaya kuja bunju kula plate ya ubwabwa kwa dada naniliu.

2.Viungo. Matumizi sahihi ya viungo na kwa mapishi gani? nilishaona sehemu wametia binzari ya mchuzi kwenye chai wakidhani tea masala. usipike chai ya rangi ukatia maji na majani hamna hata karafuu, maganda ya iliki, mdalasini wala mchaichai.

3.Usafi. Usafi wa mpishi, sehemu unayofanyia biashara, vyombo vya kupikia na vyombo vya kulia vyakula chakula. sio vyombo vichafu vinasuuzwa baada ya kuoshwa na kufanya rangi ya sahani imebadilika na unaweza ukajiongeza kwa kuvizuuza na maji ya uvuguvugu kuuwa bakteria.

4. Bei. kwa kuwa unaanza hakikisha bei zako ni rafiki pamoja na kuwa ladha ya chakula chako ni tofauti na banda la mama lishe.

5.Vitendea kazi. Lazima uwe na vitende akazi tofauti kama blenda, microwave, jiko la gesi dogo na mtungi wake, sio mteja anataka chakula anapata chakula cha baridi japo kuwa amekujamida ambayo sio ya kibiashara kivile.

6. Mahitaji. Hakikisha unakwenda kwenye masoko makuu kwa mahitaji na epukakununua mahitaji mengi sana kwa wakati mmoja kama samaki na kuku unawaweka kwnye friza mwezi mzima kwani huwa wana tabia ya kuwa na kaharufu ambacho hakikati hata umuunge vp. usinunue mchicha jumapili uje kupika ijumaa hapana, Jitahidi japo mara mbili kwa week sio mbaya uwe unakwenda mwenyewe marikiti.

6. Jiongeze. Usiuze chakula kikuu tu kama wali pilau, la ongeza najuice za viwandani na za kutengeneza mwenyewe matunda mengi ni kupata ujuzi tu, tengeneza salad baada ya kachumbari kwa kulia chakula, tengeneza pilipili za kupikana sio mteja atake pilipili umpe nzima akate mwenyewe, kwani kuna vitu vidogo vinavutia wateja sana na kama sio mjuzo sana ingia hata you tube utaona mapishi ya tofauti.

Kama kuna la ziada njoo pm nitakupa maujuzi zaidi.

Asante dada yangu huo ndio ushauri
 
KwanI na huo pia c ni ushauri

Wacheni roho ya kwanini humu ndani, mbona wengi mmeganda hapo? Hamna ushauri mwingine wa kuboresha? "KAA MWENYEWE" dada wa watu amejiaminisha na ni mwaminifu wacha afanye kazi aniingizie pesa namjua ameshafanya kazi before na kuingiza pesa so hilo niachieni mimi. Kwa kifupi kuhusu usimamizi niachieni mimi.
 
Sijaona kama kuna yeyote aliyeshauri uache kazi.

Kuna kitu wanasema learning on the fly, fungua hiyo biashara, mwache huyo unayemwamini asimamie, utajifunzia hapo.

Mimi naungana na wewe, kama una mtu una mwamini mpe asimamie, biashara itaenda vizuri sana na baada ya muda atakuachia biashara yako ataanzisha yake pale pembeni achukue na wateja wake. Muhimu ni yeye kupata mtaji tu.

Afungue mara ngapi? unafikiri ni wa njaa huyo? alishakuaga na biashara yake
 
Mwanzo mzuri mkuu...

Angalia tu binafsi kero zangu tu nikupe huenda ukazifanyia kazi.

Napenda chakuka kitamu, hasa wali hakikisha unatafta mchele mzuri na wenye ladha.

Uharaka wa huduma huwa sipendi nimefika then sisikilizwi, wahudumu wawe shapu,

Mambo ya mtu umeagiza supu then chapati za kusubili hiyo wengi hatupendi aisee.

Tafta na friji weka juisi, soda na maziwa mtindi kama kuna wapenzi nayo kama mimi.
Staha epuka maneno yanatayokushushia heshima, but tarajia maneno ya kukera kutoka kwa wateja.

Sent from my Nokia 6 using Jamii Forums mobile app
Ushauri mzuri huu. Hope atazingatia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipata watu sahihi kabisa, wapishi wazuri na sikukurupuka, hata huyo shangazi yangu ndie mpishi mkuu, na alikuwa na mghahawa wake mdogo akapata matatizo na kufilisika hivyo hii biashara anaijua vizuri sana, nilitengeneza mfumo mzuri sana wa kuiendesha biashara yangu, na bado ninaifanya huku ninaendelea na shughuli zangu japo eneo nimehama baada ya chuo kuacha kupokea wanafunzi

Nakukumbusha tuu, binadamu kiasili ni wabinafsi - unalowaza wewe na yeye yanaweza kuwa sawa au tofauti who knows.

Weka mkakati makini wa kuisimamia biashara yako, na kufanya baadhi ya shughuli mwenyewe, mimi nikiwa hapa mjini jumamosi asubuhi ninaingia mwenyewe sokoni na supplier wangu ni wale wale.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sawa shangazi yako alikua na biashara yake akafilisika but ulitakiwa uone shangazi yako kama akimfanyia mtu biashara anaifanyaje, sio ya kwake
 
Jamani kashauriwa saana kashasema anamwamini mwacheni Mimi binafsi nakuunga mkono asilimia elf kumi nilifanya biashara 3 zote niliangukia pua kisa kuachia watu yaani sasa hivi nakaba mpaka mia
huu ni ukweli mchungu ambao wengi hatuupendi kuambiwa.


Dunia nzima hakuna mtu anaependa kumfanyia mwenzake kazi ya kumtafutia hela..

Huyo dada atakuibia tu. hata awe muaminifu vipi

Biashara inayoweza kukulipa vizuri ni ile unayoifanya wewe mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani kashauriwa saana kashasema anamwamini mwacheni Mimi binafsi nakuunga mkono asilimia elf kumi nilifanya biashara 3 zote niliangukia pua kisa kuachia watu yaani sasa hivi nakaba mpaka mia

Sent using Jamii Forums mobile app

ULIANGUKIA PUA coz hukuwa makini, huyo dada ni mwaminifu ntamwachia kila kitu afanye yeye na bila yeye hamna biashara hapo, namfaham vizuri
 
Nashukuru kwa maoni yenu. Vitu ntanunua soko kuu ntadamka, ntajitahidi kuweka viungo mfano binzari,nazi, ntazingatia usafi, uchangamfu, customer care msijali dada yupo vizuri kwenye hilo anafaham vizuri haya mambo, ntafanya projection kujua sahani zinazotoka ktk kila kilo, mimi ntakuepo jumamosi kuwatembelea na kusikia baadhi ya comments na mengineyo
 
Look at u! hakuna anaekuvunja moyo hicho unachojua ni tine usichojua ni bahari ndo maana upo jukwaani kuomba msaada! Kujua sio bei ya sahani ni ratio ya maandalizi na utachouza!..Fanya moyo wako unavyokut7ma usisumbue watu
Sasa asiejua hesabu la sahani ni nani? A very light point. Usijali sivunjiki moyo kirahisi mpaka sasa sijaona point ya kunivunja moyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itakushinda kama utaanza hiv dada angu,nikwambie ukwel tuu...

Sabab management ndo kila kitu,huyo msichana si maono yake hyo biashara so yeye anafanya tuu alipwe..wew ndie mwenye maono kwamba unataka chakula kiwe hiv,quality i mean..usaf,hospitality,uwepo uvumiliv,acountability etc .so huyo dada hatowez,

Atauza wik 1 ataona hamna wateja atavunjika moyo ataanza lipua kaz na ndo mwanzo wa kuharibika..sabab trend ya biashara yoyote.enewea,graph huanza kidogo then hushuka kwa kas ya ajab,badaee ndo huanza kupanda,je huyo unaemwachia ataweza haya yote

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ndio ukweli mchungu. Nafanya hii biashara kupitia mke wangu ni ndoto yetu plus yeye ni fundi wa kupika ila kwenye ofisi ni msimamizi coz hauwezi simamia kitu usichojua.

Kwa kifupi huyu mtoa mada anatakiwa kujua hauwezi panda farasi wawil kwa wakati mmoja i.e hauwezi kuwa mwajiri alafu na wewe uajiriwe piga hesabu zako kwanza kama huo mgahawa baada ya miaka miwil utaweza kukulipa mshahara sawa na uliko ajiriwa sasa basi acha kazi na kama jibu n no basi funga mgahawa na komaa na kazi ya mwajiri wako hadi siku atakayosema hakuhitaji tena ukakomae na kikokotoo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom