Kuwa na makundi tofauti ya wateja na kupanga bei za vyakula kulingana na uwezo wa makundi hayo ya wateja ni kitu muhimu sana, wateja kwa mfano wale wa kipato cha kati na kipato cha chini ni wengi sana lakini unaweza usiwapate kwa sababu tu umeamua wewe mgahawa wako kuuza chakula kwa bei moja tu ya juu ukilenga upate faida kubwa.
Sikatai unaweza ukaweka chakula cha bei ya kuu kwa wateja wale wenye uwezo mkubwa lakini weka hata ugali na maharage, wali/ugali kwa mbogamboga za majani, mihogo ya kuchemsha, hivi ni kwa ajili tu ya wale wateja wadogowadogo ambao hawamudu vyakula vya bei kubwa. Kwa mtindo huo unaweza kukuta unapata wateja wengi sana na hivyo faida kuwa kubwa pia.