Fahamu kuhusu " Deep State " ilivyo na inavyofanya kazi

Fahamu kuhusu " Deep State " ilivyo na inavyofanya kazi

Kama unaamini kwamba utajiri unaamuliwa na deep state endelea na conspiracy theory zako. Mataifa yenye deep state ni yale ya kitajiri. Kwa nchi yetu deep state ilitaka kujitokeza kupitia kundi la wanamtandao lakini ishavurugikaa
Mtandao huwa hauvurugiki.
 
Haujailezea kwa Mapana Yake...Mfano kwa nchi kama Tanzania Bado naona Urais ni open race mtu yeyote tu aweza kuwa Rais hilo ni hatari sana iko siku tutapata mtu mjinga asie na maana awe Rais.....

Viongozi wengi ni Wanafiki na wala hawaipendi hii nchi....Hao Deep sidhani walimtaka Magufuli Lakini akawa Rais ...Kule USA Hawakumtaka Trump lakini akawa Rais..Kenya Deep state ilimtaka Ruto kwanjni alishinda hii ni mada nyingine tofauti na ndefu...
 
Ndio maana kuna Mshkaji mmoja kila siku analalamika "Mniombee"

Kwahyo nae anaiogopa hyo Deep State? Ina maana yeye licha ya kuwa namba 1 hawajui hao members 50 wanaounda Deep State ili awashughulikie?

Kwa lugha nyingine mwandishi unatuambia kuwa Deep State pia ni watu wasiojulikana?

Naomba majibu...
Inafikirisha
 
Hawa dipu steti wao hawajishughulishi na wizi wa mali za umma, mikataba ya kinyonyaji kwenye rasilimali zetu, kurithishana uongozi vizazi kwa vizazi hata kwa watu wasio na uwezo n.k? Miaka 60 ya uhuru my ass!
 
Deep State kwa tafsiri isiyo rasmi ni “Waundaji na Waendeleza Taifa”. Tanzania neno “System” (Mfumo) huwa linatumiwa sana kumaanisha deep state lakini kiuhalisia deep state sio system. System ni mojawapo ya zao dogo tu la deep state na inaweza kusambaratishwa wakati wowote.

Deep State ni kundi lisilo rasmi la kiintelijensia ambalo hujumuisha makundi mbalimbali. Hujumuisha baadhi ya watu waliopo katika utumishi na wastaafu na hata marehemu (maandishi yao) katika intelijensia ya jeshi, usalama wa taifa na hawa huja pamoja si kwa kuambiwa au kuelekezwa bali kwa yale ambayo wao wanayaamini kimapokeo kuwa ni misingi ya uhai wa taifa.

Watu hawa huamua nani awe mgombea Urais kwa mfano, nani awe Makamu wake, nani awe Waziri Mkuu, nani awe tajiri mkubwa (kwa nchi nyingi za Afrika kwa mfano matajiri wengi wamefanikiwa kwa kupitia kazi za miradi ya umma) kadhalika. Maamuzi haya hayafanywi usiku mmoja, wakati mwingine huchukua miaka wakitumia njia zote zinazowezekana kuhakikisha nani anafikia nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi au sehemu fulani nyeti na nani hafiki.

Wakiamua wewe hutakaa uwe Rais wa nchi kwa mfano, huwezi kuwa. Huwa hawana upendeleo, wana roho ngumu, maamuzi magumu, hakuna anayemzidi mwingine kwa uzito na umuhimu wa maoni na hutazama mustakabali wa nchi kwa miaka mingi mbele, tofauti na wanasiasa ambao wao hutaka tu kushinda chaguzi. Ifahamike kuwa inawezekana hata Rais aliye madarakani asifahamu kwa hakika watu hao wote kwa ujumla wao. Hii hutokea hasa katika nchi zinazofanya chaguzi kila baada ya miaka michache.

Waasisi wengi wa mataifa huwa ni sehemu ya deep state mfano Mwalimu Nyerere ambaye maandiko yake ndicho chanzo cha Waziri Kiongozi wa zamani wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kufungwa gerezani na hadi leo kuendelea kuota ndoto za kuwa Rais wa Zanzibar ambazo huenda anakwenda nazo kaburini. Deep state huwa ni kama jini, wakati mwingine unaweza kusema halipo ni maneno tu.

Deep state huweza kutikisa nchi kwa kuhujumu uongozi ulio madarakani kama ikidhihirika walikosea katika kumpitisha kiongozi husika au wakipoteza nguzo inayowalinda ambayo ni uhai wa taifa. Nchini Tanzania kundi la “deep state” halizidi watu 50 katika wakati wowote.

Itaendelea...
Hawa deep state wa Tanzania wana uchungu kweli na hili taifa au wapo kwa maslahi yao binafsi na watu wao wa karibu?
 
Sina haja ya kurudia kusoma,Umeelewaka vizuri tu maana hukuandika kihindi hapo,..
"Umesema kuthibitisha uwepo wa deep state,Trump atakuwa rais wa awamu moja tu"
Nimekwambia iyo deep stateya kina Clinton na Obama haiwezi fanya chochote,sababu ni ya kimagumashi tu.The real deep state ndio iliyomuweka Trump pale,na atashinda tena 2020.
Next time tuliza bichwa,usije na mihemko yako kama umelewa chang'aa.
Hivi Trump alishinda Tena 2020
 
Kuna tetesi kutoka katka korido za makumbusho,

member mkuu wa deep state alitangulizwa mahala pema huko juu usiku fulani hivi wa mwezi julai...inasemekana tu... chanzo ni kuedit katiba ili jamaa mmoja awe wa mihula yote sasa yeye kama role model akawa anagoma...inasemkana tu me mwenyewe sina uhakika
Atakuwa yule wa kule SOPALU?
 
Back
Top Bottom