Fahamu kuhusu Fao la Kukosa Ajira Tanzania (Unemployment Benefit)

Attachments

Kwa Sasa nahisi foa la kujitoa lililofutwa ni Bora zaidi kuliko hili la kutokuwa na ajira kutokana na nature ya upatikanaji wa ajira
 
Mkuu hii inawahusu waajiriwa wa mkataba ambao wanachukua gratuity kila baada ya mkataba kuisha na ku-renew mkataba mwingine...?
Mkuu mkataba ukiisha na ukarenew mwingine maana yake si-unaendelea na kazi....!?
 
Mkuu mkataba ukiisha na ukarenew mwingine maana yake si-unaendelea na kazi....!?
Yes kazi inaendelea ila mnapewa gratuity ya michango mliyokuwa mkichangia then mnaendelea na mkataba mpya imekaaje hiyo kiongozi...?
 
Nina kuelewa kwanini umesema hivyo lakini, Fao la kujitoa lililetwa kisiasa tu na ndio maana likafutwa, maana lilikuwa ni janga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii,
Fao halikuwa na shida na wala halikuwa tishio kama mifuko ingekuwa inawekeza kwenye miradi yenye tija, mifuko Haina ubunifu wa kuvutia hata watu kujiunga, ukiondoa Sheria wengi wasinge jiunga
 
Yes kazi inaendelea ila mnapewa gratuity ya michango mliyokuwa mkichangia then mnaendelea na mkataba mpya imekaaje hiyo kiongozi...?
Hiyo haipo mkuu, Fomu unazo pewa kwaajiri ya mafao ya kukosa ajira inasehemu ya mwajiri kusaini kama huna kazi tena, na utatakiwa kuweka kiapo cha kuto kuwa na ajira, na uchunguzi unaweza fanyika na PSSSF/NSSF Kujilizisha kama kweli huna kazi tena...
 
Fao halikuwa na shida na wala halikuwa tishio kama mifuko ingekuwa inawekeza kwenye miradi yenye tija, mifuko Haina ubunifu wa kuvutia hata watu kujiunga, ukiondoa Sheria wengi wasinge jiunga
55% Naungana na wewe.
 
Na baada ya kulipwa asilimia 33.3 je ni kweli kuwa unaendelea kulipwa kila mwezi kiwango hicho hicho mpaka upate ajira?
 
Na baada ya kulipwa asilimia 33.3 je ni kweli kuwa unaendelea kulipwa kila mwezi kiwango hicho hicho mpaka upate ajira?
Hapana, baada ya kulipwa 33.3% ya mshahara wako wa mwisho, utasubiri miezi 18+ ukitafuta ajira, ukikosa ndio utaruhusiwa kuchukua kiasi kilichobaki
 
Elimu nzuri ila hapo tu kwenye "msaada" ndo mgogoro, zile hela ni za mwanachama na si msaada na ikipita miezi 18 unalipwa kiasi ulichochangia na wanatoa hiyo 33% ya mshahara wako waliokulipa miezi 6.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…