Fahamu kuhusu Kampuni za Mfukoni-Briefcase Corporations

Uamuzi unategemea na Malengo ya Hiyo Kampuni Mpya na Shughuli zinazaofanywa na hiyo kampuni ya Zamani.Kwa Tanzania hatuna mfumo wa LLP.Ulijadiliwa ila haukufikia Muafaka.Ili kukupa ushauri mzuri ningependa kufahamu zaidi kuhusu malengo ya kampuni ya sasa na Malengo ya kampuni Mpya.
Sawa mkuu, nimekupata
 
Mtoa Mada nakuuna mkono na Mimi Binafsi tulifungu Partnership mwaka juzi ikiwa kwenye makaratas tunamshukuru Mungu Sasa Tumeingia kwnye VRN last week na Ofisi ipo MAGOMENI
Tumeajiri vijana wa 5 permanently na 3 temp-Vibarua

Kampuni inadeal na Ufungaji CCTV camera,Electrical Fence ,GPS Tracking, n.k (insta @cimax_tech_solutions au www.climaxtechsolutions.co.tz)

Nilivyoingia kwenye VAT for the first time nikajipiga kifua nikaajiita "Managing Director " nikamalizia kwa kicheko Kikubwa Sana

Jamani kila kitu is possible nakaribisha wawekezaji Sasa tuinvest kwenye GPS tracker na tracking nna proposal Idea kubwa Sana na nzuri changamoto no CAPITAL TU
Hongereni Sana,Kila Jambo ni hatua kwa Hatua....
 
Kuna maswali nilitaka kumuuliza mtoa mada ila nimeona hapa umegusia.
Kama kampuni haina ofisi mkataba wa pango unauchukulia wapi?
Pia umesema angalau umeanza kupata kazi ndogo ndogo zinazokuwezesha kulipa kodi za TRA na kulipa wafanyakazi/vibarua,sasa kwa mtu ambaye hajapata tenda maalumu na inatakiwa aendelee kulipa kodi TRA si inakuwa hasara au hii imekaaje
Mkataba wa pango sio option pekee ya kupatia leseni kwasababu sio biashara zote hukodishiwa sehemu ya kazi, wengine hupewa na ndugu wengine ni nyumbani kwake so unaweza kupeleka mkataba kama unashare na mtu ofisi yako ukachukua mkataba wake ukapeleka, au kama umeweka ofisi sehemu ambayo haulipii ila una mahusiano na mwenye jengo then akupatie au kama ni kwako chukua hati ya hilo eneo ndio unakwenda nayo kama ushahidi wa address ya ofisi yako ilipo.
 
Hii kitu haipo nimewauliza BRELA wamesema lazima uwe na ofisi hata kama ni nyumbani kwako sio mbaya
Sio lazima hata wao wanajua. Physical address inalazimishiwa ili waweze jua pa kukupata ikitokea wanachangamoto yoyote.

So kama umepanga nyumba unayoishi ila biashara zako unaifanyia mtandaoni meaning hauna frame ambayo kila asubuhi unaenda kufungua na kufunga jioni ,then huo huo mkataba wa nyumba uliyopanga ndio mkataba wako wa kupeleka huko TRA na halimashauri wakati wa tathimini.
 
Ningeomba usaidizi nahitaji kufungua jina la biashara na nimefuata hatua zote ktk usajili kupitia mtandao ila kuna baadhi ya taarifa naona mfumo unazikataa, so mwenye uzoefu nalo ningehitaji tuwasiliane tafadhari.
Haujawa specific ni taarifa gani zinakataa.
 
Hapo ndio pana utata, sitaki wajue kama mimi ni owner kwa sababu zangu binafasi na kuhusu mgogoro wa kimaslahi material naunua ofisini ila sitaki tu wajue nina kampuni yangu
Weka hata mkeo au mchumba wako au mama yako au baba yako kama owner na wewe kama muwajiriwa mbona simple tu.
 
Habari za wakati huu;

Je unajua kuwa biashara zote kubwa zilianza kama wazo? Je, unajua kwama biashara nyingi kubwa zilianza kama briefcase companies? Je, unajua kuwa biashara nyingi kubwa zilianza chini?Leo nataka nizungumze kuhusu Briefcase Companies na umuhimu wa kuwa na Kabiashara kako ka Briefcase

Briefcase Company ni kampuni ambazo zina exist ama on paper only (Registered) au zina operate nyuma ya Kampuni nyingine kama Cover. Ni aina ya kampuni ambayo inaweza kuwa inaundwa na watu wa chache, haina bidhaa maalum wala huduma, haina anuani maalum ya biashara lakini ina vibali vyote vya msingi vya kuweza kufanya biashara. Briefcase Company inaweza kuwa ni Limited Company au Sole Proprietorship. Kmapuni inaweza kuanza kama Briefcase Company na baadaye ikakua na kuwa biashara kamili yenye TIJA.

Nini faida ya Briefcase Company? Faida za Briefcase Company ni nyingi sana.

Kwanza inakuwezesha kutumia fursa za kibiashara pindi zinapojitokeza bila kupata ugumu. Mfano kama wewe ni mwajiriwa na ikatokea ofisini kuna kakazi ambako kanahitajika kufanywa kwa kutumia mtu wa nje unaweza kutumia briefcase Company yako kufanya hio kazi bila kuleta mgogoro wa maslahi.

Pili iwapo hauna ajira ya kudumu unaweza kuweka Briefcase Company yako katika CV yako na ukajipa Cheo na majukumu kama yale unayotaka kufanya kulingana na uzoefu na utaalamu wako
Tatu unaweza kutumia Briefcase Company kutafuta mikataba ya kibiashara, dili za kibiashara na ukashirikiana na kampuni kubwa zenye ukwasi katika kuzitekeleza.

Katika karne hii ya ishirini na moja ni Rahisi zaidi kuanzisha Briefcase Companies ambazo kwa sasa zimekuwa zikiitwa Virtual Business/Digital Business. Hizi ni aina ya Biashara ambazo zinaendesha na kusimamiwa kwa njia ya mtandao, zinauza na kununua bidhaa na huduma kwa njia ya mtandao. Aina hii ya biashara ina maana kwama huhitaji Ofisi kwa ajili ya kuweka stock ya mzigo wala watu kuka kufanya kazi kwani kila kazi inaweza kufanywa kwa njia ya teknolojia.

Mfano Rahisi ni Jamii Forums Mmiliki wa JF anaweza weka Servers za JF Nyumbani kwake au akakodi toka kwa kampuni zinazotoa huduma hizo popote duniani. Kisha hawa moderators wakawa wanafanya kazi wakiwa sehemu tofauti kwa njia ya mtandao kulima watu ban na kufuta post za watu ili jukwaa liendelee kuwa safi na kazi ikaenda.

Ukitazama utaona kwamba hii kampuni haitahitaji kuwa na phyisical office, ndio maana hutasikia mod wa JF anakwambia ukiwa na malalamiko njoo ofisini tuyashughulikie mnamaliza kila kitu mtandaoni. Hii ina maana kwamba teknolojia inatumika vizuri.

Kinachosumbua watu wengi ni ama kutokuwa na ujuzi wa kutumia teknolojia au kutokujua waanzie wapi katika kuanzisha hio Kampuni ya Briefcase. Kuna namna nyingi za kuanzisha Briefcase Company na leo nitazungumzia moja ambayo ni rahisi. Fuata hatua zifuatazo ili kuanzisha Kampuni ya Briefcase.

  1. Hatua ya kwanza ni kutambua ujuzi au utaalamu wako. Hakikisha Angalau unakuwa na utaalamu fulani mfano unaweza kuwa na Genge la Nyanya, Muuza Karanga au Muuza mkaa. Sasa hakikisha kwamba unajenga mfumo wako wa biashara kwa kuzingatia hilo kwani biashara yako ndogo lazima uwe na maono makubwa nayo. Mfano Biashara ya mkaa inaweza husiana na sector ya Domestic energy au Forest Management, Biashara ya Karanga na genge la nyanya inaweza husiana na Kilimo biashara.
  2. Pili chagua Jina la Biashara ambalo litakua pamoja na Biashara yako.
  3. Kulingana na aina ya biashara unaweza kuanzisha kurasa za mitandao ya kijamii na hata tovuti ili uweze kurahisisha mawasiliano
  4. Sajili jina la biashara, tafuta leseni na Ufungue bank account kwa kutumia Jina la Biashara.
Ukishakuwa na hivyo tayari unayo Biashara yako ya Mfukoni ambayo sasa unaweza kuhangaika kuitafutia mtaji, wateja na bidhaa au huduma.

Ukishakuwa na Kampuni yako hakikisha unakuwa na Business cards na unakuwa active kuipeleka biashara yako sokoni. Kwa mfano unaweza anza kwa kuwatafuta wateja wa karibu na marafiki kisha ukaongeza na wengine. Zingatia Mfano niliotoa ni mfano mdogo.

Hata hivyo teknolojia inakuruhusu kuanzisha ecommerce shops za kuuza bidhaa mbalimbali kwa uwekezaji mdogo tu kwenye website na application za simu.

Anza leo na kuna siku utakuja kunishukuru.Uskubali CV yako iwe tupu kwamba huna kazi wakati unaweza kusajili jina la biashara na ukawa Mwajiriwa katika Biashara yako hata kama huna mshahara.Ukiona huwezi andika cheo kikubwa basi sema tu uko Field kwenye kampuni yako mwenyewe hakuna atakayekuuliza maswali.

Kama Unahitaji kanzisha kampuni yako ya mfukoni (Briefcase Company) Wasiliana nasi kwa email masokotz@yahoo.com ili tuone namna tunaweza kusaidiana.Tutshirikiana na wewe kufanya yafuatayo:

  1. Kusajili Biashara yako BRELA, TRA, LESENI, na VIBALI Vingine
  2. Kufungua Akaunti Bank
  3. Kuandaa Company Profile ikiwa ni pamoja na LOGO, WEBSITE, EMAILS etc
  4. Kutuma cold emails kwa potential Clients ikiwa ni pamoja na kufanya Appointments
  5. Kuandaa Job description kwa nafasi mbalimbali na kufanya shorlisting pamoja na interview.
  6. Kuwa na wewe katika hatua za mwanzo za biashara yako mpaka itakapoimarika na kukusaidia kupata ushauri wa kitaalam kwa gharama nafuu

Karibuni tujadili namna bora ya kuanzisha na kusimamia Briefcase Companies na Faida na Changamoto zake.
Mkuu masokotz umepotelea wapi?
 
KAMPUNI YA MFUKONI....

Hapa unamaanisha full company kabisa (LTD COMPANY)? au unamaanisha just a BUSINESS NAME?
 
Yeyote Ile inategemea na wewe tu mwenyewe umejipangaje
 
Back
Top Bottom