Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Thats a good business and am also interested.,am a busy guy,so i want to put some one incharge..so how can i monitor her/him to make sure i ge (he profits, and not her/he parting away with it ?
 
thats a good business and am also interested.,am a busy guy,so i want to put some one incharge..so how can i monitor her/him to make sure i ge (he profits, and not her/he parting away with it ?
I think you should find a reasonable person mtu unayemuamini biashara ndivyo zinavyokwenda pamoja na umakini lazima pia umuweke mtu unayemuamini
 
Heshima kwenu,

1. M PESA
2. Tigo pesa
3. Airtel money
4. CRDB fahari huduma
5. Kifaa cha max malipo kwa ajili ya luku etc

Jamani ndugu yenu nafikiria kuanzisha hii biashara ya u-wakala wa m-pesa. Mwenye details kidogo kuhusu hii biashara anijuza hasa nataka kufahamu kuhusu;

1. Kiwango cha chini cha mtaji unao hitajika
2. Jinsi faida inavyopatikana
3. Jinsi ya kujisajiri (hili nadhani sio issue sana naweza kwenda kwa voda wenyewe) itanirahisishia zaidi

Nawasilisha
===========

Mimi ni wakala wa M-Pesa kitambo sana sijawahi tapeliwa, inalipa sana kama tu goli lako lipo sehemu yenye mchanyiko wa watu wengi na kama unaielewa vizuri biashara hiyo.Unahitaji kuwa na laini, TIN na eneo la kufanyia biashara kumsajili mteja ni Tsh 500/- kamisheni.

Mteja aliyesajiliwa akiweka pesa kwa mara ya kwanza unapata tsh 2000 kamisheni akituma pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh 300/- hadi tsh 5000/- inategemeana ametuma kiasi gani akitoa pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh500/- hadi tsh 5000/- inategemeana katoa shilingi ngapi.

Akinunua airtime kwako unapata karibia 10% kamisheni ya airtime aliyonunua
akinunua Luku unapata kamisheni kadhaa.

Biashara hii ili ufanikiwe zaidi unaweza kuichanganya na biashara nyingine kama kuuza luku, na vinywaji baridi kama soda na juisi ambavyo havihitaji mtaji mkubwa au kama una biashara yako tayari halafu ukaongezea hii biashara kama ziada.

Yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi ZAP, M-pesa na Tigo Pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, ya nini kuajiriwa sasa?
================

Faida yake inategemea yafuatayo:

1. Ufanisi wako (via Operator) wa kazi;

Kama service ni nzuri hasa in unavyowasikiliza na kuwashughulikia wateja, hii inahusisha mhudumu wako kua haraka na kujua huduma zote.

Mfano: Mteja anaweza asijue jinsi ya kutumia akaunti yaM-pesa, hapo ina maana Mhudumu awe mpole amsaidie.

2. Mtaji

Uwe na mtaji wa kutosha ili kuhakikisha mteja akija kutoa au kutuma pesa anapata.
Hii itasaidia kutopoteza miamala kwa kukosa pesa na pia itamfanya mteja awe anaiamini sehemu yako hata siku nyingine kuja kwenye banda lako.

3. Mahesabu

Hakikisha jioni unafunga mahesabu pesa yako mkononi na kwenye laini. Kama jumla ilikuwa milioni mbili asubuhi jioni inatakiwa iwe hio hio milioni mbili.

Unapata pesa ya commission mwisho wa mwezi.

Kama mtaji wako ni Million 5 kwa siku na inazunguka ipasavo na hio sehemu ina shughuli nyingi, kamisheni inaweza fikia hata milioni moja au zaidi.

Changamoto
  • Kama sehemu haina mzunguko wa pesa wa kutosha unaweza kupoteza muda wako, wateja wapo wa kutosha ni nadra kupata hasara. More inakua out of mistakes kama kutuma pesa mahala ambako sio husika kwa bahati mbaya.
  • Unaweza ukatuma pesa kwa mtu mwingine ambaye sio mteja kwa bahati mbaya, japo pesa hii unaweza kupiga simu kwa vodacom halafu wakarudisha muhamala huo mara nyingine unaweza usiupate kama uliyemtumia atakuwa haraka kwenda kutoa.
  • Noti feki kama kuna wateja wanaweza wakakuletea mabunda ya pesa huku wakiwa wamechanganya na mabunda ya noti feki, kabalaya kuweka pesa kwenye droo yako hakikisha unaziangalia, kama unafanya hadi usiku nunua tube light ili kuwe na mwanga wa kutosha kugundua noti feki.
  • Kuna vikwazo pia katika biashara hii, na kubwa likiwa ni suala zima la usalama kuna vibaka au majambazi wanaweza wakakutegea ukiwa unatoka wakakukaba, ni bora kuwa na sefu lako imara, kwenye fremu yako pia kunatakiwa kuwe na grili imara kuzunguka dirisha na mlango.
 
Mimi ni wakala wa M-Pesa kitambo sana sijawahi tapeliwa,inalipa sana kama tu goli lako lipo sehemu yenye mchanyiko wa watu wengi na kama unaielewa vizuri biashara hiyo.

Kichwa kukisajili ni Tsh 500/- kamishen
Kichwa kilichosajiliwa kwa mara ya kwanza kikiweka pesa unapata tsh 2000 kamisheni.
Kichwa kikituma pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh 300/- hadi tsh 5000/- inategemeana katuma shilingi ngapi.
Kichwa kikitoa pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh500/- hadi tsh 5000/- inategemeana katoa shilingi ngapi
Kichwa kikinunua airtime kwako unapata karibia 10% kamisheni ya airtime aliyonunua
Kichwa kikinununa Luku unapata kamisheni kadhaa.

Yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi ZAP, M-pesa na Tigo Pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, yanini kuajiliwa sasa?
 
Mimi ni wakala wa M-Pesa kitambo sana sijawahi tapeliwa,inalipa sana kama tu goli lako lipo sehemu yenye mchanyiko wa watu wengi na kama unaielewa vizuri biashara hiyo.
@kichwa kukisajili ni Tsh 500/- kamishen
@kichwa kilichosajiliwa kwa mara ya kwanza kikiweka pesa unapata tsh 2000 kamisheni.
@kichwa kikituma pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh 300/- hadi tsh 5000/- inategemeana katuma shilingi ngapi.
@kichwa kikitoa pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh500/- hadi tsh 5000/- inategemeana katoa shilingi ngapi
@kichwa kikinunua airtime kwako unapata karibia 10% kamisheni ya airtime aliyonunua
@kichwa kikinununa Luku unapata kamisheni kadhaa
Yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi ZAP,M-pesa na Tigo Pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, yanini kuajiliwa sasa?

Salute Mkuu
 
Yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi ZAP,M-pesa na Tigo Pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, ya nini kuajiliwa sasa?
Sidhani kama hapo ni kujiajiri. Nionavyo mimi ni kwamba umeajiriwa na Zain (ZAP), Vodafone (M-PESA) na Tigo (TIGO-PESA)
 
mimi ni wakala wa m-pesa kitambo sana sijawahi tapeliwa,inalipa sana kama tu goli lako lipo sehemu yenye mchanyiko wa watu wengi na kama unaielewa vizuri biashara hiyo.
@kichwa kukisajili ni tsh 500/- kamishen
@kichwa kilichosajiliwa kwa mara ya kwanza kikiweka pesa unapata tsh 2000 kamisheni.
@kichwa kikituma pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh 300/- hadi tsh 5000/- inategemeana katuma shilingi ngapi.
@kichwa kikitoa pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh500/- hadi tsh 5000/- inategemeana katoa shilingi ngapi
@kichwa kikinunua airtime kwako unapata karibia 10% kamisheni ya airtime aliyonunua
@kichwa kikinununa luku unapata kamisheni kadhaa
yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi zap,m-pesa na tigo pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, yanini kuajiliwa sasa?

shukran - kama ungenijuza pia masharti ya kuwa wakala plz
 
Nasikia kupata uwwakala wa MPESA ni issue hebu utujuze jamani
mimi nataka hata kesho lakini kupata hiyo number nasikia sasa hivi ni issue nikuone wapi themankind ili ikiwezekana nianze kabla ya tarehe 15 nimedhamiria
 
Siku hizi wanachakachua ile faida ya mawakala hawa watu...wasipojirekebisha akina Tigopesa na airtell pesa wanakuja....mgema akisifiwa tembo hulitia maji...jirekebisheni ninyi
 
Mimi nimeanza hii biashara siku za hivi karibuni kw amtaji wa shilingi milion 1....hard cash laki 3 na soft cash laki 7.....kupata laini ilikua kazi sana,na sijapata moja kwa moja toka voda ila wale waliosajiliwa na voda huwa wanapewa laini 4 hadi 5 mimi nina my friend kanipa lain 1 kwamalipo ya 25% of the comision every month
 
Habari zenu wana jf, nimekuwa nikijiandaa kwa muda na msingi lakini biashara ninayofikiria kufanya ni hii ya mambo ya m pesa, tigo pesa with stationary stuffs,

JE, HII VODACOM AND TIGO PESA ZIKO VIPI? I MEAN FAIDA ZAKE, JINSI YA KUJIUNGA?
NATANGULIZA SHUKRAN!!!


ZASASULE...............
 
Kwanza andaa duka mahala penye mzuko wa kifedha kata leseni ya biashara, toa nakala ya kitambulisho na ya tin namba yako na ya leseni yako tembelea vodashop au tigo centre iliyokaribu nawe uombe uwakala.

Ina faida kubwa sana kwa mawakala wa muda mrefu na walioko maeneo yenye mshike shike nyingi. Yaani utaipenda ukipata eneo nzuri.

Kwa maelezo na ushauri zaidi nipigie kwenye no. 0753819003, 0767819003, 0783819003, 0773819003, 0718014803, 0718014813.

Umechagua biashara poa.
 
habar zenju wana jf na wadau wote.
ndugu zanguni napenda kujuzwa juu ya biashara ya m pesa na tigo pesa
na mchakato mzima juu ya uanzishwaji wake. habari chache ni ziizokuwa
nazo na maitaji yake kama ifuatavyo
1) deposited money m pesa 1000000 tigo 500000
2) leseni ya biashara mfn stationery
3) front office and etc

ndugu wadau mwenye habari zaid naomba amwage data,then iyo depodited
money inaingia kny mtaji au mtaji unajitegemea?
na kama m pesa ni office zipi za vodacome unaweza kupata faster
naomba kuwasilisha.
 
mkuu una maswali kama yangu ngoja tusubili great thinker watuelimishe
 
Habari wadau, Nimekua nikitamani kufanya/kuwa wakala wa hizi huduma za m~pesa na tigo~pesa ila sijui taratibu za kupitia zikoje, kianzio kipoje, faida inapatikanaje,? tafadhali naombeni mwenye taarifa ama maarifa yoyote yanayohusia na hizi huduma naomba anijuze. best regards.
 
​kuna kiwango cha fedha kama mtaji unaotakiwa uwe nao nadhani ni kama shs milioni moja hivi....kisha unaenda kwenye ofisi zao wanakusajili , kumbuka kuwa na TIN namba unapoenda kwao
 
2. Jinsi faida inavyopatikana
Sio tu faida inavyopatikana. Ni vizuri pia utafiti faida inayopatikana.

Niliwahi kuwafuatilia hao kina Voda nikagonga mwamba makao makuu, wakanambia sijui nimwone fulani, leo katoka, jana yuko likizo, kesho kutwa kampeleka mkewe hospitali, nikaona ujinga, nikaachana nao.

Experience yangu kwa uwakala wa makampuni makubwa kwa ujumla ni mbaya. Nimekuwa supplier wa Cocacola, nimeuza mafuta ya GAPCO, nimeuza internet services za TTCL. Nikaapa sitafanya uwakala wa kampuni kamwe. Wao wanapanga bei bila kujua bei ya mtaani huku ni ngapi, hawajali unapata faida au hupati, very ignorant people, customer service mbovu, hawana kitengo cha mawakala, unakuta kuna ofisa mmoja wamemuweka kwenye cubicle ndio eti a deal na issue zote za suppliers! So ridiculous.
 
Back
Top Bottom