Mbona kama unaonekana kuna vitu unavifanya visivyo vya halali ktk hii biashara? Naona unazunguka zunguka tu reply zako zote. Sikiliza mtoa mada, hii biashara ni mzuri ukipata eneo lenye movement kubwa. Kwasasa kama walivyosema baadhi ya watu kwamba commission zimeshuka sana ukilinganisha na awali. Pia siku hizi unakatwa kodi ya asilimia kumi ya commission yako, zamani haikuwepo. Kwa mikoa ya pwani yani dar na wenzie, tigo ndo anaongoza kwa commission, kwa mikoa ya kusini, airtel ndo anaongoza. Kanda ya ziwa vodacom anaongoza. Ukipata sehemu mzuri kwa dar tigo unaweza kupata hadi laki 7 vodacom laki 4 na airtel laki 3. Zamani tigo ilikuwa hadi 1m vodacom laki 8. Changamoto ktk biashara hii, ukiachilia mbali matapeli na vibaka kukumezea mate, lkn pia inatabia ya kukata pesa bila kujua sababu. Yani unawza balance vizuri hasubui, lkn jioni ukakuta hata tsh 70,000 haipo. Hiyo ndo changamoto kubwa ambayo haijapatiwa ufumbuzi hadi leo. Namna ya ziada kujiongezea kipato ni kuwachaji watu wanaotaka kutuma hela direct, unaweza kuchaji hata buku, unaangalia na mtu mwenyewe. Ukipata watu wa 5 kwa siku unakuwa ushapata nauli.