Wandugu wa jf habarini za midaa hii.
ama baada ya salaam mi nipende kuja na mada hii kama inavyosomeka hapo juu. kwa sisi ambao tupo kijasiliamali zaidi huwa tunapenda kujihusisha na vitu mbalimbali vya kutupatia ugali ili siku iende; kwa maaana hiyo huwa hata tunafanya kazi za uwakala.
Changamoto iliyonikuta mpaka nakuja humu ni kwamba ni upi hasa utaratibu wa kupata laini ya uwakala wa mpesa unaotambulika?
Mwaka 2016 niikuwa pande za SUA pale Mji kasoro bahari, pale niliomba lain mashariti niliyoambiwa ni kupeleka nakala ya TIN, Leseni na kitambulisho zikiwa zimethibitishwa na mwanasheria na mimi nilifanya hivyo nikapata laini yangu ndani ya mwezi mmoja.
hapa TARIME nimekuja ni tofauti kabisa, mbali na kupeleka hizo nakala unaambiwa na wale wahudumu wa vodashop ya mzungu mmoja eti ulipie 50,000/= swali langu kwa VODACOM ni kwamba upi utaratibu hasa wa kupata laini? kwa nini mkoa mwingine iwe ni bure wakati sehemu zingine tunalipia? tena cha ajabu ukilipia halafu ukadai risiti unapewa risiti imeandikwa .....Chacha....... hii ina maana gani?
achilia hilo, unaweza peleka nakala zako ukamaliza mwaka hujapata laini yako, mfano: maka jana (2017 may nilienda vodashop Tarime kuomba hiyo laini nikaacha nakala zilizodhibitishwa za baba, nikaambiwa nitajulishwa kwa sms, siku zilipita nyingi bila kupata sms hivyo nikaenda kuulizia majibu niliyoyapata ni kwamba document zilichomwa moto kimakosa na hivyo napaswa kupeleka tena upya hizo document. sikukuzipeleka tena maana nilikata tamaa cha ajabu mwaka huu mwezi wa april baba kapigiwa simu ikimtaka atumie laini vinginevyo itafungwa ili hali mimi niliambiwa laini haipo na haikutengenezwa. niliamua kwenda kuulizia wakasema hata wao hawajui hii ina maana kwamba waliuza laini yangu ama kwa makusudi ama kwa kutojua...nilipeleka document tena kuomba swap mwezi wa june mpaka leo laini haijatoka na hakuna majibua ya kueleweka.
OMBI: 1. naomba kama kuna afisa yeyote wa voda anipatie hayo majibu ni kwanini inakuwa hivyo kama nilivyoeleza hapo juu.
2. naomba msaada wa kisheria humu namna ya kufanya ili nipate laini maana nahisi kama ni makosa kutumia visvyo vyako bila rdhaa ya mmiliki na kama ndo hivyo nifanyeje ili nimwajibishe meneja wa vodashopTarime kwa kunipotezea mda kiasi hicho?