Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Katika replies zote hakuna aliyeweza msaidia alichouliza ilihali kuna watu wamesema wanaifanya hii biashara, mmoja2 kasema wanalipa kwa kamisheni mwisho wa mwezi, najua hajaelewa kamisheni inakuwaje, mfano labda ukifanya miamala kiasi flani, tegemea kupata kamisheni ya sh kadhaa kwa mwezi

Niulize chkulia mfano umefanya miamala ya ya200k kwa mwezi, watakulipa sh ngapi kwa mwezi?? (Wengi tunajifunza, na kujifunza kwetu hakuzibi riziki ya wew uliyeko kwenye system!

Nawasilisha

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app

7KQ84ES Imethibitishwa
tarehe 26/11/20 3:28 PM
Toa Tsh175,000.00 kwa
255 - C M.
Salio lako ni Tsh503,569.00, Kamisheni Tsh460.00 pamoja na kodi.

Hivyo basi hapa ili upate faida unahitaji kuwa na mzunguko mkubwa faiada kwa muamala ni hizo 50 mpaka 1000 na mapoint hivyo ili upate faida kubwa unapaswa kufanya miamala mingi kwa siku na si vinginevyo uzuri ni kwamba kila ukifanya muamala unapata mavuno yako hapo hapo sema kamisheni ndo wanatoa kidogo ukilinganisha na ghalama anazo tozwa mteja wakati wa kutoa hela ilipaswa mtoa huduma na kampuni wagawane ile tozo aliotozwa mteja wakati anatoa pesa nisi wao kuchukua asilimia 98% na wewe kuchukua asilimia 2%
 
U
View attachment 1486746


Wana jukwaa,

Naomba maelezo ya namna ya kuwa wakala wa M-PESA pamoja na uuzaji wa luku.

Ikiwezekana kama kuna mtu anayehusika moja kwa moja naomba kumuona. Nipo Dar es Salaam



wapalepale post
Heshima kwenu,
1. M PESA
2. Tigo pesa
3. Airtel money
4. CRDB fahari huduma
5. Kifaa cha max malipo kwa ajili ya luku etc

Jamani ndugu yenu nafikiria kuanzisha hii biashara ya u-wakala wa m-pesa. Mwenye details kidogo kuhusu hii biashara anijuza hasa nataka kufahamu kuhusu:

1. Kiwango cha chini cha mtaji unao hitajika
2. Jinsi faida inavyopatikana
3. Jinsi ya kujisajiri (hili nadhani sio issue sana naweza kwenda kwa voda wenyewe) itanirahisishia zaidi

Nawasilisha

================​

Mimi ni wakala wa M-Pesa kitambo sana sijawahi tapeliwa,inalipa sana kama tu goli lako lipo sehemu yenye mchanyiko wa watu wengi na kama unaielewa vizuri biashara hiyo.Unahitaji kuwa na laini,TIN na eneo la kufanyia biashara
kumsajili mteja ni Tsh 500/- kamishen

mteja aliyesajiliwa akiweka pesa kwa mara ya kwanza unapata tsh 2000 kamisheni akituma pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh 300/- hadi tsh 5000/- inategemeana ametuma kiasi gani
akitoa pesa kwako unapata kamisheni kuanzia tsh500/- hadi tsh 5000/- inategemeana katoa shilingi ngapi

akinunua airtime kwako unapata karibia 10% kamisheni ya airtime aliyonunua
akinunua Luku unapata kamisheni kadhaa
Biashara hii ili ufanikiwe zaidi unaweza kuichanganya na biashara nyingine kama kuuza luku, na vinywaji baridi kama soda na juisi ambavyo havihitaji mtaji mkubwa au kama una biashara yako tayari halafu ukaongezea hii biashara kama ziada

Yaani kwa kijana wa kitanzania wa kawaida akiwa serious inaweza akatolewa na biashara hii kwa ufupi ZAP,M-pesa na Tigo Pesa kama una magoli matatu au maanne kipato cha mwezi ni net 2m, yanini kuajiliwa sasa?

================​


Faida yake inategemea yafuatayo:

Ufanisi wako (via Operator) wa kazi;
Kama service ni nzuri hasa in unavyowasikiliza na kuwashughulikia wateja, hii inahusisha mhudumu wako kua haraka na kujua huduma zote.

Mfano: mteja anaweza asijue jinsi ya kutumia akaunti yaM-pesa, hapo ina maana Mhudumu awe mpole amsaidie.

uwe na mtaji wa kutosha ili kuhakikisha mteja akija kutoa au kutuma pesa anapata
hii itasaidia kuptopoteza miamala kwa kukosa pesa na pia itamfanya mteja awe anaiamini sehemu yako hata siku nyingine kuja kwenye banda lako.
  1. Hakikisha jioni unafunga mahesabu pesa yako mkononi na kwenye laini. Kama jumla ilikuwa milioni mbili asubuhi jioni inatakiwa iwe hio hio milioni mbili
  2. Unapata pesa ya commission mwisho wa mwezi. Kama mtaji wako ni Million 5 kwa siku na inazunguka ipasavo na hio sehemu ina shughuli nyingi, kamisheni inaweza fikia hata milioni moja au zaidi
Changamoto
  1. Kama sehemu haina mzunguko wa pesa wa kutosha unaweza kupoteza muda wako, wateja wapo wa kutosha ni nadra kupata hasara. More inakua out of mistakes kama kutuma pesa mahala ambako sio husika kwa bahati mbaya.
  2. Unaweza ukatuma pesa kwa mtu mwingine ambaye sio mteja kwa bahati mbaya, japo pesa hii unaweza kupiga simu kwa vodacom halafu wakarudisha muhamala huo mara nyingine unaweza usiupate kama uliyemtumia atakuwa haraka kwenda kutoa
  3. Noti feki kama kuna wateja wanaweza wakakuletea mabunda ya pesa huku wakiwa wamechanganya na mabunda ya noti feki, kabalaya kuweka pesa kwenye droo yako hakikisha unaziangalia, kama unafanya hadi usiku nunua tube light ili kuwe na mwanga wa kutosha kugundua noti feki.
  4. Kuna vikwazo pia katika biashara hii, na kubwa likiwa ni suala zima la usalama kuna vibaka au majambazi wanaweza wakakutegea ukiwa unatoka wakakukaba, ni bora kuwa na sefu lako imara, kwenye fremu yako pia kunatakiwa kuwe na grili imara kuzunguka dirisha na mlango
Uzi mzuri nitarudi
 
Kuna Till ya M-PESA (lain ya M-PESA) inauzwa kwa aliyetayar nichek 0764928129 location Mbeya mjini
 
Man ukifanikiwa kupata Luku also weka M-Pesa, Zap, Tigo pesa. Nitakupa mbinu how to get more business by using M-Pesa, Zap, na Tigo pesa and Luku. Hapo Dar sijaona watoa huduma ya Luku wakiitumia hiyo mbinu. It is too profitable if you are based in Dar.

I think kupata M-Pesa, Zap na Tigo Pesa ni rahisi sana ugumu uko kwenye Luku, lazima uwe na muda wakutosha na uvumilivu pia unatakiwa.
Naomba unisaidie mawasiliano unisaidie kitu hapa mkuu.
 
Na huo ndio uhalisia muhimu mzunguko tu mtaji si mali kitu na mleta mada akiwa mvumilivu miezi mitatu tu biashara hii inampa mtaji mkubwa zaidi me nilianza na laki Na nusu tena nikiwa na line moja kila mwezi nilikua si chini ya 60 elfu commission saa Hizi mtaji umekua kama 400k line zipo mbili najipatia laki 80 safi kwa mwezi
Umenipa kitu aisee nilikuwa natafuta comment kama hii.
 
Sasa hivi ukienda kwenye maduka ya vodshop wanakuambia huduma ya kusajili mawakala wapya imesimamishwa mpaka mwezi wa nane. Ss cjui ni kwa Moshi na Arusha au nikote?
 
laini za uwakala

TIGO na Voda 150,000 ndani ya saa 24
Halotel - 30,000
TTCL - 20000
AIRTEL MONEY - 30000

Serious customers ni PM
 
Back
Top Bottom