Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Nijuavyo mimi O/D Inatumika kuongeza mkandamizo wa pistoni hivyo kuipa engine nguvu.
Inakua On pale unapominya kitufe cha O/D na kwenye dashboard taa ya O/D itawaka na kuonyesha maandishi ya O/D OFF.
Na kitaalamu inatakiwa uminye O/D gari ikiwa kunzia spee 40 na kuendelea.

Du maelezo humu yanasigana sana. Nilikuwa nimeelewa lkn sasa nazidi kuconfuse kabisa.
 
Du maelezo humu yanasigana sana. Nilikuwa nimeelewa lkn sasa nazidi kuconfuse kabisa.

mkuu hujaelewa nn?
Nikwamba ukiminya button, taa ya O/D Itawaka,na kwenye dashboard pata onekana maandishi ya taa nyekundu au blue ya O/D OFF= Hii inamana gari inatembea overdrive ikiwa on.
Ukiminya tena,taa ya O/D kwenye dashboard itazima = Hii inamaana gari inatembea overdrive ikiwa off.
 
Imagine gari yako ni manual transmission. Sasa hiyo ni button inayozuia gear no 4 isiende no 5 pindi ukikanyaga mafuta zaidi , kwa maana ya iongeze spidi kwa muda mfupi uwezekanavyo kwa ajili ya kulipita gari kwa haraka na kwa muda mfupi, yaani kufanya take off ya haraka sana..ukishampita unai off OD button ili isinywe mafuta zaidi na kuichokesha engine.
 
mkuu hujaelewa nn?
Nikwamba ukiminya button, taa ya O/D Itawaka,na kwenye dashboard pata onekana maandishi ya taa nyekundu au blue ya O/D OFF= Hii inamana gari inatembea overdrive ikiwa on.
Ukiminya tena,taa ya O/D kwenye dashboard itazima = Hii inamaana gari inatembea overdrive ikiwa off.

Asante kwa kuiweka kwa usahihi; natumai hivyo ndivyo inavyotakikana kutumika. Jf idumu milele"
 
Asanteni wadau wote kwa michango yenu makini mloitoa hapa jamvini kwa kunipa darasa mimi na wale wenzangu tulokuwa hatulijui jambo hili kwa usahihi wake.
 
Mkuu asante sana kwa elimu na ninaomba nichote hii post yako hapa. Nimekuwa nikiendesha na OD/OFF on muda mrefu sana bila kujua na nitakuwa nimechosha sana engine. Matokeo yake OD/OFF imeanza ku blink. Sasa kitaalam over use of it nipe ujuzi. Du nimesikitika sana.
Kweli mkuu wengi wanaendesha hizi automatic bila kujua matumizi sahihi ya OD/ON au OFF. Endapo unaendesha kasi na ukiwa hujaweka ON kwa maana ya kwamba hujaminya hako kabatani gari itakuwa inatumia mafuta mengi sana bila sababu na wakati huo huo utakuwa unai-overwork injini hivyo kuichosha haraka. Ile ukiiweka ON ukiwa katika mwendo wa kasi ya kuanzia spid ya km40 au 50 na kuendelea unaifanya gari kuwa nyepesi na hivyo hata mafuta kutumika kidogo. Watu wengi wameyalaumu magari yao kuwa yanatumia mafuta sana kumbe ni wao wanaokosea katika uendeshaji. Wengine huyapeleka kwa mafundi wakidai gari inabugia kiwese sana. Bahati mbaya mafundi wengi wa jua kali nao hawajui maana na matumizi ya Over drive hivyo kuishia kuichokonoa gari bila sababu. Na unapokuwa katika mwendo mdogo halafu umeweka Over drive ON unakuwa pia unaichosha gari kwa maana ya kuwa inakuwa Uncomfortable. Inakuwa ni kama vile umeweka gia namba 4 au 5 kwenye mwendo mdogo ambao ungehitaji gia namba 2 au 3. Ukiwa unaendesha mannual(ya kupanga gia) uatagundua haraka kwani gari inaweza kuzima unapolazimisha kutumia gia ndogo mahali inapohitaji kubwa. Hizi automatic ni zenyewe ni pole sana kwa maana ya kuwa huwa hazizimi unapokosea lakini madhara yake ni kuwa unakuwa unapunguza life span yake. Sasa wasiojua ndio utawsikia wakisema "automatic ni gari mbovu au hazidumu" kumbe wao ndio wabovu wa matumizi
 
Asanteni kwa Majibu mazuri; lakini samahani bado naona kuna shida kidogo hapo kwenye wakati gani O/D inakuwa On maana naona majibu yanasigana kidogo na baadhi ya waelimishaji; sasa napata shida hapa nishike lipi?
Lakini vinginevyo nimepata darasa zuri kabisa nashukuru sana.
Ukiminya kale kabatani na maandishi OD/OFF kufutika kwenye dsh board, maana yake unakuwa umeweka ON. Unapokwa hujakaminya kale kabatani na taa ya OD/FF ikiwa inawaka kwenye dash board maana yake ni kuwa Over drive iko OFF kama inavyosomeka kwenye dash board. Kwa ufupi ni kuwa inapokuwa ON hakuna maandishi yanayoonekana kwenye dash board yako yaani taa huwa inazima!
 
mkuu hujaelewa nn?
Nikwamba ukiminya button, taa ya O/D Itawaka,na kwenye dashboard pata onekana maandishi ya taa nyekundu au blue ya O/D OFF= Hii inamana gari inatembea overdrive ikiwa on.
Ukiminya tena,taa ya O/D kwenye dashboard itazima = Hii inamaana gari inatembea overdrive ikiwa off.
Sijui gari yako ni aina gani. Lakini ukweli ni kuwa Ukiminya button, taa ya OD/OFF inazima na kwa maana hiyo unakuwa umeweka Over drive ON. Usipominya ile button taa nyekundu au kijani (rangi hutegeana na watengenezaji walivyochagua) inayoonesha maandishi OD/OFF itakuwa inawaka na kwa maana hiyo Over drive iko OFF kama inavyosimeka.
 
Ahante kwa elimu hii, sikuwa hata najua maana yake hii, nimetembea O/D ikiwa off kwa maana ya taa kuwa kwenye dash board kwa muda kidogo, leo ndio nimejua nini ni nini
JF na idumu

mkuu hujaelewa nn?
Nikwamba ukiminya button, taa ya O/D Itawaka,na kwenye dashboard pata onekana maandishi ya taa nyekundu au blue ya O/D OFF= Hii inamana gari inatembea overdrive ikiwa on.
Ukiminya tena,taa ya O/D kwenye dashboard itazima = Hii inamaana gari inatembea overdrive ikiwa off.
 
Mbalamwezi;561997]Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita motakaa nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe motakaa yako inakuwa umepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka uklisha maliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
Hii ON na OFF inachanganya...
[/QUOTE]
 
Nimependa maelezo haya
quote_icon.png
By Mbalamwezi

Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kuna uzi kama huu na link imewekwa na Msalani ukurasa wa kwanza hapa bandiko Na. 4.
Taa ikiwaka kwenye dash board (O/D OFF) maana yake umezuia matumizi ya hiyo gia ya mwisho (say 5 au 6). Kiuhalisia O/D ipo off. Hairuhusu gia ya mwisho kufanya kazi. Siku zote, mjini au vinginevyo, weka tu on (maana yake usione taa kwenye dash board) ndo maana halisi ya automatic-itaamua yenyewe itumie gia gani na wakati/mazingira gani.

Katika hali ya kawaida, dash board haipaswi kuwaka taa yoyote ile. Iwakapo, O/D ama nyinginezo (ABS, (O), etc) fanya kitu kinachopaswa ziondoke/zizime.
 
Kwahiyo ukiwa unaendesha gari siku zote O/D ikiwa On Kwa maana ya kuifanya gari ichague yenyewe gia sahihi kwa wakati husika;je kuna madhara yoyote kwa chombo husika?
 
Ahante kwa elimu hii, sikuwa hata najua maana yake hii, nimetembea O/D ikiwa off kwa maana ya taa kuwa kwenye dash board kwa muda kidogo, leo ndio nimejua nini ni nini
JF na idumu
Karibu mkuu,hii ndio tofauti ya JF na mitandao mingine ya kijamii.
 
Hii ON na OFF inachanganya...
[/QUOTE]

Ikiwa kwenye dash board maandishi mekundu yanasomeka "O/D OFF" basi ujue gia namba 5 unakuwa umeizima. Haitakuja wakati itakapohitajika. Ili iwepo, inabidi ubonyeze kitufe ili maandshi hayo mekundu yatoweke. Umeelewa mkuu?
 
kitu ya kusaidia sana hii maana wengine ni kuangalia maji,mafuta,oil baada ya hapo twende kazi,thanks in advance wakuu mliotupa maujanja haya
 
Baada ya kusoma uzi mzima ndo nimeishia kuchanganyikiwa sasa hasa kuhusu matumizi yake. Kwahiyo ninapokuwa ktk mizunguko ya kawaida hapa mjini hiyo taa ya O/D kwenye dashboard niache inawaka au isiwake? Katika somo lililonikanganya hapa JF basi hili namba moja.
 
Back
Top Bottom