Baada ya kusoma uzi mzima ndo nimeishia kuchanganyikiwa sasa hasa kuhusu matumizi yake. Kwahiyo ninapokuwa ktk mizunguko ya kawaida hapa mjini hiyo taa ya O/D kwenye dashboard niache inawaka au isiwake? Katika somo lililonikanganya hapa JF basi hili namba moja.
Taa zote zilizopo ktk dash board ni Alerts <angalizo> kwa dereva, hazipaswi kuwaka. Kuna taa ya mafuta, oil, betri, milango, hand break, ABS nk, yoyote ikiwaka ni ishara kwa dereva arekebishe jambo au kitu fulani. Hivyo taa ya O/D OFF haipaswi kuwaka muda wote wa kuendesha gari.. Comments za baadhi ya wana JF humu zinapotosha. Nakubaliana na comment ya ndg CTU, yupo sahihi na ameelimisha.