Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic


Du maelezo humu yanasigana sana. Nilikuwa nimeelewa lkn sasa nazidi kuconfuse kabisa.
 
Du maelezo humu yanasigana sana. Nilikuwa nimeelewa lkn sasa nazidi kuconfuse kabisa.

mkuu hujaelewa nn?
Nikwamba ukiminya button, taa ya O/D Itawaka,na kwenye dashboard pata onekana maandishi ya taa nyekundu au blue ya O/D OFF= Hii inamana gari inatembea overdrive ikiwa on.
Ukiminya tena,taa ya O/D kwenye dashboard itazima = Hii inamaana gari inatembea overdrive ikiwa off.
 
Imagine gari yako ni manual transmission. Sasa hiyo ni button inayozuia gear no 4 isiende no 5 pindi ukikanyaga mafuta zaidi , kwa maana ya iongeze spidi kwa muda mfupi uwezekanavyo kwa ajili ya kulipita gari kwa haraka na kwa muda mfupi, yaani kufanya take off ya haraka sana..ukishampita unai off OD button ili isinywe mafuta zaidi na kuichokesha engine.
 

Asante kwa kuiweka kwa usahihi; natumai hivyo ndivyo inavyotakikana kutumika. Jf idumu milele"
 
Asanteni wadau wote kwa michango yenu makini mloitoa hapa jamvini kwa kunipa darasa mimi na wale wenzangu tulokuwa hatulijui jambo hili kwa usahihi wake.
 
Kweli mkuu wengi wanaendesha hizi automatic bila kujua matumizi sahihi ya OD/ON au OFF. Endapo unaendesha kasi na ukiwa hujaweka ON kwa maana ya kwamba hujaminya hako kabatani gari itakuwa inatumia mafuta mengi sana bila sababu na wakati huo huo utakuwa unai-overwork injini hivyo kuichosha haraka. Ile ukiiweka ON ukiwa katika mwendo wa kasi ya kuanzia spid ya km40 au 50 na kuendelea unaifanya gari kuwa nyepesi na hivyo hata mafuta kutumika kidogo. Watu wengi wameyalaumu magari yao kuwa yanatumia mafuta sana kumbe ni wao wanaokosea katika uendeshaji. Wengine huyapeleka kwa mafundi wakidai gari inabugia kiwese sana. Bahati mbaya mafundi wengi wa jua kali nao hawajui maana na matumizi ya Over drive hivyo kuishia kuichokonoa gari bila sababu. Na unapokuwa katika mwendo mdogo halafu umeweka Over drive ON unakuwa pia unaichosha gari kwa maana ya kuwa inakuwa Uncomfortable. Inakuwa ni kama vile umeweka gia namba 4 au 5 kwenye mwendo mdogo ambao ungehitaji gia namba 2 au 3. Ukiwa unaendesha mannual(ya kupanga gia) uatagundua haraka kwani gari inaweza kuzima unapolazimisha kutumia gia ndogo mahali inapohitaji kubwa. Hizi automatic ni zenyewe ni pole sana kwa maana ya kuwa huwa hazizimi unapokosea lakini madhara yake ni kuwa unakuwa unapunguza life span yake. Sasa wasiojua ndio utawsikia wakisema "automatic ni gari mbovu au hazidumu" kumbe wao ndio wabovu wa matumizi
 
Ukiminya kale kabatani na maandishi OD/OFF kufutika kwenye dsh board, maana yake unakuwa umeweka ON. Unapokwa hujakaminya kale kabatani na taa ya OD/FF ikiwa inawaka kwenye dash board maana yake ni kuwa Over drive iko OFF kama inavyosomeka kwenye dash board. Kwa ufupi ni kuwa inapokuwa ON hakuna maandishi yanayoonekana kwenye dash board yako yaani taa huwa inazima!
 
Sijui gari yako ni aina gani. Lakini ukweli ni kuwa Ukiminya button, taa ya OD/OFF inazima na kwa maana hiyo unakuwa umeweka Over drive ON. Usipominya ile button taa nyekundu au kijani (rangi hutegeana na watengenezaji walivyochagua) inayoonesha maandishi OD/OFF itakuwa inawaka na kwa maana hiyo Over drive iko OFF kama inavyosimeka.
 
Ahante kwa elimu hii, sikuwa hata najua maana yake hii, nimetembea O/D ikiwa off kwa maana ya taa kuwa kwenye dash board kwa muda kidogo, leo ndio nimejua nini ni nini
JF na idumu

 
Hii ON na OFF inachanganya...
[/QUOTE]
 
Nimependa maelezo haya
 
Kuna uzi kama huu na link imewekwa na Msalani ukurasa wa kwanza hapa bandiko Na. 4.
Taa ikiwaka kwenye dash board (O/D OFF) maana yake umezuia matumizi ya hiyo gia ya mwisho (say 5 au 6). Kiuhalisia O/D ipo off. Hairuhusu gia ya mwisho kufanya kazi. Siku zote, mjini au vinginevyo, weka tu on (maana yake usione taa kwenye dash board) ndo maana halisi ya automatic-itaamua yenyewe itumie gia gani na wakati/mazingira gani.

Katika hali ya kawaida, dash board haipaswi kuwaka taa yoyote ile. Iwakapo, O/D ama nyinginezo (ABS, (O), etc) fanya kitu kinachopaswa ziondoke/zizime.
 
Kwahiyo ukiwa unaendesha gari siku zote O/D ikiwa On Kwa maana ya kuifanya gari ichague yenyewe gia sahihi kwa wakati husika;je kuna madhara yoyote kwa chombo husika?
 
Ahante kwa elimu hii, sikuwa hata najua maana yake hii, nimetembea O/D ikiwa off kwa maana ya taa kuwa kwenye dash board kwa muda kidogo, leo ndio nimejua nini ni nini
JF na idumu
Karibu mkuu,hii ndio tofauti ya JF na mitandao mingine ya kijamii.
 
Hii ON na OFF inachanganya...
[/QUOTE]

Ikiwa kwenye dash board maandishi mekundu yanasomeka "O/D OFF" basi ujue gia namba 5 unakuwa umeizima. Haitakuja wakati itakapohitajika. Ili iwepo, inabidi ubonyeze kitufe ili maandshi hayo mekundu yatoweke. Umeelewa mkuu?
 
kitu ya kusaidia sana hii maana wengine ni kuangalia maji,mafuta,oil baada ya hapo twende kazi,thanks in advance wakuu mliotupa maujanja haya
 
Baada ya kusoma uzi mzima ndo nimeishia kuchanganyikiwa sasa hasa kuhusu matumizi yake. Kwahiyo ninapokuwa ktk mizunguko ya kawaida hapa mjini hiyo taa ya O/D kwenye dashboard niache inawaka au isiwake? Katika somo lililonikanganya hapa JF basi hili namba moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…