Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Hapo wakuu hupaswi kuchanganyikiwa, kama sio mtaalamu wewe hakikisha hakuna taa inayowaka kwenye dashboard, hizi gari ni full automatic, yote unayofikiria inaweza kufanya yenyewe bila msaada wako, hicho kibatani cha OD/ON waliweka kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa na control zaidi kama gari ya manual.

Ukitaka nguvu zaidi we kanyaga mafuta ghafla yenyewe itatambua kuwa unahitaji nguvu zaidi, itabadilisha gia kutoka ya juu kuja chini, ukiachia mafuta inajua kuwa unapunguza mwendo inabadili gia ili upate engine brake, kwa kifupi hupaswi kufanya chochote zaidi ya kuongeza mafuta, brake na kunyoosha stearing. Hayo mengine waachieni wataalam!
 
Siijui kwa undani zaidi ila nimewahi kuitumia mara kadhaa. Unapobonyeza kitufe cha O/D, itasomeka kwenye dashboard yako O/D OFF. Hapo inakuwa iko ON kwa gari nilizowahi kuendesha. Mara nyingi ninapokuwa kwenye mwendokasi na nahitaji nguvu na mwendo zaidi wa injini, huwa nabonyeza hiyo O/D, kama kuna gari mbele yangi nitaipita kama imesimama. Nadhani matumizi yake yanahusika na mwendokasi pia ila ukiwa na mwendo wa kawaida sidhani kama inafanya kazi, ngoja wenye uelewa waje watujuze vizuri.

Hizo gari huwa unazipita kwa hali ya kawaida tu na sio sababu ya OD kuwa OFF, by default OD kwenye gari yoyote inakua ON. Unapobonyeza button ikaonyesha kwenye dashboard "O/D OFF" maana yake ndio umezima hiyo OD na gari inaanza kufanya kazi katika namna tofauti


Katika maelezo ya kawaida yasiyo ya kiufundi sana ni kuwa OD inatakiwa kiwa ON unapokua unaendesha high speed kuanzia 80km/h na kuendelea.

Kama unaendesha mjini kwenye foleni speed 30, OD inatakiwa kuwa OFF


Kwa maelezo ya kiufundi ni kuwa O/D ON inaruhusu gari kutumia gear zote yaani moja hadi tano kulingana na namna unavyokanyaga mafuta, O/D OFF inaruhusu gari kutumia gear ya kwanza mpaka 3 tu, hata ukikandamiza mafuta hadi mwisho gear haibadiliki tena kwenda 4 na 5

Hii inakusaidia tu kama unatembea mwendo mdogo au unapanda milima au mtu anayejifunza kuendesha, otherwise matumizi ya kawaida ya gari ni O/D ON
 
Hivi gari ikiandika od off on dashboard inamaanisha nini?

Msaada plz
 
Inamaanisha over drive switch imezimwa! izimwapo gari huanza changanya kuanzia gear kubwa 2,3 gari inakua nzito koadi,;na iwashwapo huchanganya kwa haraka kwenda gears 4&5 gari inakua nyepesi.
 
Kwa tanzania OD kuwa on ni bora kwani inapunguza matumizi ya mafuta. Kwa wenzetu kule kwenye snow OD inawekwa off kupunguza uwezekano wa gari kuteleza.
 
OD, means Over Drive.
OD OFF, means Over Drive is off.
OD ON, means Over Drive is on.
How to use these signs..
When it is On means you can drive your car especially on the muddy, sometimes the car stuckys or at the hills when the normal gear fails you press over drive the car starts if it still fails you press drive 1 then it goes smoothly, though fuel consumption will be higher than Off Drive.
But when it is off , means it is on the normal drive as an AT cars needs to be, you use it on the high way drive and this is the best way and safe to drive your car.
 
Magari mengi taa ya OD inapaswa kuwaka Kama Ikimaanisha Over drive iko Off, Na iwe Imezima ikamaanisha OverDrive iko On.

Sasa nimegundua wengi wakiona taa inawaka huminya Button ili izime Kumbe ndio wameweka kwnye OD.
 
Back
Top Bottom