Fahamu kuhusu Scania Buses VS Yutong, Kinglong, Zhongtong, Higer, Golden Dragon, Sunlong Buses

Niandike tu kwa ufupi jao sitaweza kuweka data za utafiti huu hapa jukwaani kutokana na sababu binafsi.

Basi za mchina zinapendwa kwa sasa kutokana na gharama nafuu na hivyo kurudisha faida fasta.

Basi za china zina shida kwenye
1-Engine (zinachoka mapema compared to SCANIA)

2-Chasis zinalamikiwa kupata cracks

3-Gearbox ikianza kusumbua ni shida na tatizo kubwa inakua baadhi ya gear haziingi.

4-Durability ya body ni mbovu kabisa.

Ndio mana huwa wengine wanatumida muda mfupi kisha wanavisha Engine, Gearbox na Difu za Scania.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina hata cha kubisha, maana umeweka full facts. Hongera.
Nafuta maneno yangu yaliyokuwa yanakupinga kuhusu bei ya 500-800ML.

Upande wa pili wa kutafakari, hivi hakuna dalili za utakatishaji pesa hapo?
Maana hao wachaga wanaomiliki hiyo kampuni ya mabasi na hao wahaya wanaomiliki hizo shule ni mabingwa wazuri sana wa kutumiwa katika kutakatisha pesa.
 

refer to saibaba zenye plate number A zile marcopolo zina miaka mingapi mara iende mbeya mara iende arusha mara kampala ila bado zipo zinapiga mzigo
 

Hizi pesa hua zinarudi na faida juu, Mwezi wa nne Dar express analeta Scania G7 Paradisso inayouzwa zaidi ya 1.2billion tzs atakua ni mtu wa kwanza Tanzania kumiliki pia ukiangalia kipindi cha nyuma alikua mtu wa kwanza kuleta Irizar Century, G7 na sasa analeta hizo Paradisso
 
Mkuu ungeweka kapicha hapo tuone huo mchuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu si uandike kwa staha tu, yanini kutoa kebehi, kwani kuna mabishano.

Mtu kama hajaelewa ni kumuelewesha tu kwa utaratibu basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na bei zinaendaje Mkuu, kama hautajali tuwekee na picha kiongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo upande wa pili tutajadili siku nyingine leo tujikite kwenye buses zao kwanza.
Asante
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abood na Kilimanjaro bado wanascania za namba A, tafuta Gari ya mchina yenye namba hata C inayotembea kwenda route ndefu kama Dar to Mbeya, Kahama, Songea au Mwanza.
 
Labda akachonge body na kupachika chassis na eng,
 
Jamani myonge mnyongeni haki yake mpeni mimi kama msafiri unambie nipande dar express au sunlong ya shabiby .. nachagua sunlong sababu seat zina nafasi .. TV nyuma ya seat , usb charger .. kupupwe cha kutosha ... choo ndani ...

Mchina hata kama hadumu sisi abiria tutapanda mchina sababu una relax ukiwa ndani ... mbio za nini ..
 

Hapa tunajadili life span kwanza na kuhusu biashara za haya mabus, tutakuja kwenye comfortability ambayo mchina ndio anapatia mwanya hapo, wala usijali
 
Mtu akinunua kitu genuine anatakatisha fedha?

Kwamba wafanyabiashara wote wana akili na mitazamo inayofanana?

Sawa na ushangae mtu anaenunua simu ya 4M wakati kuna simu ya 500K na inafanya kazi vizuri tu.

Mbona hujasema Scandinavia walikuwa wanatakatisha fedha?

Na isitoshe, hao kina Dar express wamekuwa wananunua Marcopolo miaka nenda rudi, wanajua standards zao.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Scania za Dar express au Kilimanjaro ni next level interms of seating.

Seats za mabasi ya mchina ni ngumu kama za Eicher. Ukipanda zile za kilimanjaro zipo comfortable and spacious.

Tatizo bus halikimbii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio mtaalamu wa magari ila kuna bus linaitwa kisbo safari, nimekuwa nikilisia sana humu Jf kuwa linatembea sana.

Mwezi uliopita nikiwa dodoma pale maeneo ya unapotaka kujengwa uwanjani barabarani, nikapishana na bus za KISBO SAFARI mbili.

Moja ilikuwa saa 7 na dakika 8, na ikawa inatembea taratibu. Nikasema hii bus inawezaje kwa sasa mambo ya tochi barabarani kufika Dodoma saa 7?

Ilipofika 7:30 ikapita KISBO ya pili, hapa nilichoka saana, nikasema hawa jamaa ni hatari.

Yaani hata zile gari za Dodoma kutoka Dar bado haziingii muda huo kwa saa 7 kamili kuwa Dodoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…