JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Ni utando mweupe unaotengenezwa kwenye ngozi ya mtoto kwenye kipindi cha mwisho cha ujauzito, kitaalam huitwa Vernix caseosa.
Huundwa na maji kwa asilimia 80, mafuta kwa asilimia 10 na protini kwa asilimia 10.
Tofauti na jinsi inavyoaminika sana mtaani, utando huu hautokani na kushiriki tendo la ndoa karibu na muda wa kujifungua.
Vernix siyo shahawa, wala haina uhusiano wowote na kitu hicho. Hii inatokana na muundo wa anatomia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke ambao huufunga mji wa uzazi kwa kuta imara zisizo ruhusu kuingia kwa shahawa zinazotolewa wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Pia, ifahamike kuwa watoto waliozaliwa wakati sahihi huwa na kiasi kikubwa cha utando huu huku waliozaliwa kwa kupitiliza siku zao huzaliwa na utando kidogo sana.
Kazi zake
• Kuzuia maambukizi ya magonjwa ya ngozi kwa watoto wakati akiwa tumboni na baada ya kuzaliwa.
• Kupunguza msuguano kati ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
• Kutunza joto la wastani linalofaa kwa ajili ya ukuaji wa siku za mwanzo za mtoto.
• Kuipatia ngozi ya mtoto unyevu unaostahili.
• Kuzuia ngozi ya mtoto isiharibike na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kwa kuwa mtoto huelea kwenye mfuko wa uzazi uliojaa maji (maji ya uzazi) kwa miezi mingi sana, huwa ni lazima utando huu utengenezwe ili kuilinda ngozi ya mtoto kwanza akiwa bado anaelea tumboni kisha baada ya kuzaliwa.
Baada ya kuzaliwa, utando huu huanza kuisha wenyewe taratibu ukichukua siku hadi wiki kadhaa.
Cc: Mr kenice